Jun 30, 2017
Wekeza Kwa Shilingi Laki Moja, Upate Zaidi Ya Milioni Moja Na Nusu Ndani Ya Siku 90.
Na Boniface
L. Pwele, Songea.
Leo
nataka tuangalie kilimo cha matikiti kibiashara kwa mtaji wa shilingi laki moja
tu(100,000/=). Nimeona niandae hili somo kwa kuwa watu wengi hulalamika kuhusu
mtaji lakini kwa asilimia kubwa watu humililiki zaidi ya hii pesa laki moja,
lakini bado utamkuta analalamika kuhusu mtaji wa kuanzia.
Leo
tutaangalia mchanganuo wa shilingi laki moja ili ikuletee milioni moja na
nusu(1,500,000/=) kwa makadilio ya chini kabisa hayo ni baada ya siku 75-90 na
unaweza pata zaidi ya hapo, ikiwa utaweka juhudi nyingi katika kilimo ambacho
unaenda kufanya.
Hapa
tutaangalia mchanganuo kwa kutumia mbegu bora ya matikiti aina ya PATO F1. Na
eneo linalohitajika ni chini ya robo ekari (yaani nusu ya robo ekari ) ila
katika laki moja sijaweka gharama ya shamba ambayo ni nusu ya robo ekari yaani mita
500 za mraba.
Maandalizi ya shamba.
Andaa
shamba lenye ukubwa wa mita 500 za mraba( 50m×10m).
Baada
ya kuliandaa shamba lako hakikisha una mbolea ya kuku ya kutosha mashimo 500 tu
na uhakikishe hiyo mbolea imeoza vya kutosha.
Chimba
hayo mashimo 500, chukua mbolea ya kuku ichanganye vizuri na udongo. Kisha piga dawa aina ya Colt kwenye mashimo ikae walau siku 14.
Baada
ya siku ya 14 unaweza panda mbegu zako.
Mbegu
ya PATO F1 50g ambayo unaweza kuipata kwa sh 35,000/= tu inatosha kupanda hilo
eneo la mita 500 za mraba.
Panda
kwa nafasi nzuri, mstari hadi mstari iwe mita mbili na shimo hadi shimo iwe
sentimita 50( yaani mita 2 kwa sm 50)
Panda
mbegu mbili mbili lakini hakikisha huziweki sehemu moja humo shimoni.
Baada
ya kuota mmea ukisha fikisha majani matatu punguza mche mmoja kwa kuukata na
siyo kuung'oa.
Matunzo shambani.
Siku
ya 0-15 (Planting and germinating) mbegu itakuwa tayari isha ota na inakaribia kutambaa.
Mmea
wa matikiti hupendwa sana na wadudu, hivyo mara baada ya kuota ukiwa na majani
angalau matatu tumia dawa ya wadudu aina Prosper
720EC (Profenofos 600g/L + Cypermethrin 120,000/=), ikichanganywa na Agrigrow starter NPK 14:28:18, hii
inafanya mmea kuwa na mizizi imara na kuufanya mmea kuweza kufyonza virutubisho
vizuri kutoka kwenye udongo,ikichanganywa na Agrilax .
Na
hapo uwe na mbolea ya Yara Mila Winner
kilo tano ambayo utaweka gramu tano (kisoda kimoja) kwa kila mche
Siku
ya 16-25( Vegetative/Trailing) hapo
tikiti litaanza kutambaa hakikisha una Agrigrow
vegetative NPK 30:10:10, hii itakuza mmea kwa haraka na kuongeza matawi, dawa
ya wadudu Avirmec.
Siku
ya 25-40 (Flowering) hapo mmea utaanza kutoa maua,hakikisha una mbolea ya Yara Mila Nitrabor ambayo utaweka gram 10
kwa mmea mmoja, dawa ya wadudu Colt, Agrigrow flowering and Fruiting NPK 15:5:35 hii itazalisha maua kwa wingi
na kufanya yasipukutike.
Kuwa
makini kwenye upigaji wa dawa wakati wa kipindi hiki, inakubidi upulizie dawa
asubuhi sana au jioni sana,kwa maana hii hatua ndipo kunakuwa na wadudu wa
muhimu shambani kama nyuki,ambaye ni muhimu sana kwa zao hili la matikiti,ndiyo
maana unashauriwa kama unalima zaidi hata kama ni ekari moja unaweza weka
mzinga wa nyuki shambani kwako ili wasaidie katika uchavushaji.
Siku
41-60-90 (Fruiting) hapo hapo mmea utakuwa umeanza kubeba matunda.
Hatua
hii mmea unatakiwa upate maji ya kutosha lakini inatakiwa upunguze kiasi cha
maji siku kumi kabla ya kuvuna kulifanya tikiti liweze kutengeneza sukari ya
kutosha.
Mavuno.
Kwa
eneo la mita 500 mita za mraba (Yaani mita 50 kwa mita 10) utakuwa na miche
1000 kwenye eneo la mita za mraba 500. Kwa kuwa kila shimo itakuwa ni miche
miwili. Kumbuka nilikuambia zikiota inabidi upunguze mche mmoja mmoja.
Hivyo
katika eneo lako utakuwa na miche 500. Na kwa matunzo mazuri mche mmoja huweza
kufikisha hadi matunda matatu. Ila mimi nakupigia kwa hesabu ya tunda moja kwa
mche.
Na
hilo tunda litakuwa ni kubwa sana kuanzia kilo kumi hadi 15. Kwa matunda 500 na
tunda moja kwa kuwa ni kubwa unaliuza kwa bei ya jumla sh 3000/=Matunda
500×3000= 1,500,000/=(Milioni moja na nusu)
Kama
utayauza mwenyewe reja reja utayauza kwa sh 5000 hadi 7000 hadi 10,000 kwa
tunda moja. Hivyo ukiyauza kwa sh 5000 utaweza kupata 5000×500=2,500,000/=Kumbuka
hiyo ni shilingi laki moja imezalisha pesa hiyo ndani ya miezi mitatu (siku 90).
Sasa
amua kuendelea kutunza pesa benki ambako makato yanaendelea au uwekeze baada ya
miezi mitatu uweze kupata hizo fedha.
Nimeandaa
hili somo kukupa mwanga wewe ambaye unatamani kulima lakini unasema huna mtaji
na wakati una pesa zaidi ya hii niliyo itaja hapo juu.
Lakini
ikumbukwe hyo laki moja sijaweka gharama sijui ya Kukodi hako kakipande ka
shamba,kulima unaweza lima mwenyewe kabisa.
Na
usiseme sina pesa ya kununua mafuta kwa ajiri ya kumwagilia miche mia tano
unaweza chota maji kabisa kwenye ndoo na ukaimwagilia miche yote.
Gharama
ya vitu vyote nilivo vitaja hapo juu
Mbegu
PATO F1 50g 35,000/=
Agrigrow
starter NPK 14:28:18 500g 5000/=
Agrigrow
Vegetative NPK 30:10:10 500g 5000/=
Agrigrow
flowering and fruiting NPK 15:5:35 500g 5000/=
Yara
mila Winner 5kg 10,000/=
Yara
Mila Nitrabor 5kg 10000/=
©Dawa
za wadudu
Prosper
250mls 9,000/=
Colt
250mls 8000/=
Avirmec
50mls 4000/=
Agrilax
500g 9000/=
Mbolea
ya kuku (Omba kwa mtu anayefuga kuku)
Bei
za mbolea hizo za Yara inategemeana na wapi ulipo maana unaweza pata chini ya
hyo bei.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika
kila siku.
Wako mtaalamu wa kilimo, Boniface L
Pwele, bwana shamba nipo kwenye kampuni
ya Agrichem Africa Tz Ltd. Kwa msaada juu ya ushauri kuhusu kilimo tuwasialiane
kwa 0762 567 628 au nitumie e-mail kwenda blugahno95@gmail.com.
Jun 29, 2017
Kile Unachokiweka Kwenye Akili Yako, Ndicho Hicho Kinachokufanya Ufanikiwe Au Ushindwe.
Kile
unachokiweka ndani yako, ndicho hicho unachokitoa nje. Kama unaweka au
unajirisha furaha, basi maisha yako yakatakuwa ya furaha. Kama unaingiza ndani
yako hasira, basi utatoa hasira, kama pia unaweka ndani yako mafanikio, utayapata.
Jiulize,
kuna wakati unakuwa na siku mbaya, siku ambayo hujisikii kufanya kitu kabisa,
lakini hata hivyo ukiangalia nyuma au siku moja kabla kuna mambo ambayo uliyoyaweka
akili mwako ndio yaliyokufikisha hapo ulipo.
Hata
unapoona wengine wanafuraha, wanafamafanikio ni lazima ujue kuna kitu ambacho
walichowekeza ndani yao na kikawapa furaha au mafanikio hayo ambayo unayaona
kwa sehemu kubwa kwa nje.
Kitu
unachotakiwa kuelewa, mawazo yako kila wakati yanaongozwa na hisia zako. Na hisia
zako pia zinaongoza hatua unazotakiwa kuchukua, hatua hizo zinapelekea kukupa
matokeo na mwisho wa siku matokeo hayo yanakutengenezea mfumo wa maisha
uliokamili.
Weka mambo sahihi kwenye akili yako, ili ufanikiwe. |
Kitu
unachotakiwa kukumbuka, mawazo yako hayo, hayaji kwa bahati mbaya, bali
yanatokana na vitu ambavyo unaviingiza akilini mwako mara kwa mara. Kwa vitu
hivyo unavyoingiza ndivyo vinavyokupa mawazo hayo.
Ukijichunguza
vizuri, angalia uhusiano wa taarifa unazoziweka kwenye akili yako na mtazamo
wako juu ya maisha. Hapa sina shaka, utaona ni vitu vinavyofanana. Mtazamo wako
ni lazima utaendana tu na yale mawazo yako.
Huwezi
ukawa unaweka kwenye akili yako umbea umbea au mambo ya hovyo, halafu
ukategemea kuwa na ubunifu au ukatengeneza maisha ya kimafanikio sana, hapo uwe
na uhakika sana utaishia hapo hapo.
Wewe
ni matokeo ya unavyofikiri. Hupendi hali ya maisha uliyonayo, hupendi sana hapo
ulipo, badili sana vitu unavyoingiza akili mwako. Ukibadili vitu hivyo,hata
vile unavyovitoa navyo vitakuwa na utofauti.
Kuwa
na furaha, mafanikio au kuwa mtu wa hasira hasira, ni vitu ambavyo unatengeza
mwenyewe na sio suala la muujiza wowote. Chunga sana kile unachokiingiza ndani ya
akili yako, kumbuka hicho ndicho utakachokitoa kwa baadae.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa, endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; , +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jun 28, 2017
Sio Kila Mtu Anafaa Kupewa Kitu Hiki Cha Kimafanikio…
Sio
kila mfuko unafaa kuwekwa pesa, unaweza ukaweka pesa kila mfuko mwisho wa siku
ukakuta katika mfuko huo hakuna kitu.
Hivyo jitahidi kuwa na mfuko sahihi kwa ajili ya kuwekwa fedha.
Mwenye
utashi wa kawaida anaweza asielewe usemi huu unamaanisha nini, ila mfuko ambao
ninauzungumzia ni mazingira yako yote ambayo yanakuzunguka kwa namna moja ama
nyingine.
Mazingira
haya ni mkusanyiko wa vitu vyote vilivyomo ndani yake ikiwemo na mwanadamu
mwenyewe. Na mwanadamu huyu ndiye mwenye uwezo wa kufanya mazingira hayo yaweze
kuwa bora au mazingira hayo kwa namna moja ama nyingine.
Sio
kila mfuko unafaa kuwekwa pesa. Katika safari yako ya kuelekea mafanikio
makubwa, si kila mtu anafaa kumwambia jambo ambalo unalitaka kulifanya. Nasema
hivi kwa sababu wengi wetu tumekuwa hatuwashirikishi watu sahihi katika mambo
ambayo tunatamani kufanya, mwisho wa siku tumekuwa watu ambao maisha hayo
tunayona machungu kama alovera.
Sio kila mtu anafaa kuambiwa kila kitu. |
Hivyo
kwa kila jambo ambalo unalifanya ili uweze kuwa bora na kufanikiwa zaidi,
unachotakiwa kufanya ni kutafuta watu sahihi kwa kile ambacho unakifanya au kwa
kile ambacho unataka kukifanya. Ukiwa na upele hakikisha unamtafuta mtu mwenye
kucha, kwani endapo utamtafuta mtu ambaye hana kucha ni sawa ni kutwanga maji
katika kinu.
Kama
unataka kufanya biashara ya kuuza mchicha usiende kuomba ushauri kwa muuza mkaa
kwani hatakuwa na ushauri wa kutosha kuhusu biashara ya mchicha zaidi atakupa
maoni binafsi kwa kile ambacho anakiona kwa wafanyabiashara wa mchicha. Na
mwisho wa siku atakwambia biashara hii haifai. Hivyo kwa kila chochote
unachotaka kufanya hakikisha unafuta mtu ambaye anakifahamu kitu hicho kwa
undani zaidi.
Hata
wewe ndugu yangu mwenye siri ndani ya moyo wako, epuka kumwambia kila mtu hiyo
siri yako kwani wapo wengine katika
dunia hii, wapo kwa ajili ya kusambaza siri za wengine. Hivyo jitahidi sana
wewe mwenye siri nzito ndani ya nafsi yako, epuka kuweka pesa kila mfuko kwani
mifuko mingine ni mapambo.
Pia
kama wewe ni kiongozi wa serikali au kampuni binafsi, nawe nakwambia sio kila
mfuko unafaa kuwekwa pesa. Kama unataka kufanya uchaguzi wa mtu fulani ambaye
anafaa kusimamia ofisi yako, hakikisha unafanya uchunguzi sahihi kabla
kumchagua mtu fulani. Kufanya hivi kutakusaidia kwa namna moja ama nyingine
kuja kujutia maamuzi yako.
Mwisho
ninamini umenielewa vyama ya kwamba si kila mfuko unafaa kuwekwa pesa.
Ndimi Afisa mipango wa mafanikio, Benson
chonya,
0757 90 99 42,
bensonchonya23@gmail.com
Jun 27, 2017
MAFANIKIO TALK; Siri Sita Za Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio.
U
hali gani mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, tukualike kwa mara nyingine katika kipindi
hiki cha mafanikio talk ambacho
hukujia kila siku ya jumanne, ambapo siku ya leo tupo na ndugu yetu SHABANI SAIDI kutokea pale Dodoma ambapo
atukumbusha mambo ya muhimu ya kuzingatia katika biashara.
Shabani
saidi anasema ya kwamba neno biashara lina maana kuu mbili ambazo ni kitendo
cha kubadilishana bidhaa kwa bidhaa au ni kitendo cha kubadilishana bidhaa na
fedha. Lakini anakwenda mbali zaidi na kusema ya kwamba katika biashara yeyote
ambayo unaifanya ni lazima uweze kuwa na lengo la biashara hii ndiyo siri ya
kufika mbali zaidi.
Ambapo
alieleza ya kwamba katika biashara lengo kubwa ni kupata wateja zaidi, na
katika hili wengi wamekuwa hawafahamu, wamekuwa wakizani ya kwamba lengo la
kufanikiwa katika biashara ni kupata fedha pekee, lakini ukweli ni kwamba ukiwa
na lengo hilo pekee utakuwa unakosea sana.
Kwani
katika biashara ni lazima uweze kuwa mbunifu kila wakati, na ukiwa mbunifu
kutakuwa na ongezeko la wateja na ongezeko la wateja hilo ndilo litalokufanya
uweze kupata fedha, na fedha hizo zitakufanya uweze kuwa bora katika kukuza
biashara yako.
Zifuatazo Ndizo Siri Sita Za
Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio.
1. Kuwa na wazo bora la biashara.
Kuwa
na wazo bora la biashara unayotaka kuifanya ndiyo msingi mkubwa wa kuweza kufanikiwa
katika biashara uifanyayo au ambayo unataka kuifanya. Kuchagua wazo bora la
biashara huenda sambamba na kuangalia mahitaji ya watu katika eneo husika.
Kwa
mfano kama unataka kuanzisha biashara fulani
ni lazima uangalie watu hao wanahitaji
nini. Mara baada ya kujua wanahitaji nini ndipo na wewe utapata wazo la kufanya
biashara husika. Hivyo wazo bora la biashara hutokea kwa watu wanaokuzunguka.
Zijue siri muhimu za kibiashara ili ukuze biashara yako. |
2. Kufanya uchunguzi wa eneo kwa ajili ya
kufanya biashara.
Saidi
anasema kabla ya kuanzisha biashara yeyete ile ni lazima uweze kutafuta eneo
kwa ajili ya kufanyia biashara, na si eneo tu bali ni eneo sahihi kwa ajili ya
kufanya biashara husika.
Kuchagua
eneo sahihi la kufanyia biashara ni sawa na kuchagua mke bora wa kuoa, kwani
endapo utakosea utajilaumu maisha yako yote. Hivyo kila wakati unachotakiwa
kufanya ni kuhakikisha unachagua eneo lenye uhakika katika kufanya biashara
yenye mashiko kwako.
3. Kutafuta mtaji.
Mara
baada ya kupata wazo bora la biashara, na mara baada ya kupata eneo bora kwa
jaili ya kufanyia biashara jambo la tatu, unatakiwa kuanza kutafuta mtaji kwa
ajili ya kukamilisha wazo ulilonalo.
Majibu
ya namna ya kupata mtaji yatapatikana mara baada ya kupata wazo bora la biashara, kwani mahali hapo unatakiwa
kufanya uchunguzi yakinifu. Uchunguzi huo utakusaidia kuona kubuni pia namna ya
kupata mtaji.
4. Kuwa mbunifu.
Kwa
kuwa katika dunia hii kila kitu kinafanana, hivyo ili uweze kujitofautisha na
wengine unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa mbunifu ili uweze kufanikiwa
zaidi katika biashara ambayo unaifanya, au biashara ambayo unatarajia kuifanya.
Unapokuwa
mbunifu inakusaidia sana kujenga biashara yako na kuifanya biashara hiyo
ikaonekana ya mafanikio kwa kupata wateja wengi. Popote pale utakapofanya
ubunifu kwenye biashara yako uwe na uhakika utafanikiwa.
5. Kujifunza kwa waliofanikiwa.
Mara
baada ya kutafuta mtaji unachotakiwa kufanya ni kujifunza kutoka kwa watu ambao
tayari wamekwisha fanikiwa katika biashara husika. Pia Saidi anasema ya kwamba
endapo utajifunza kwa watu ambao wameshafanikiwa unachotakiwa kufanya ni
kuhakikisha ni kuwa mbunifu zaidi ya yule ambao umejifunza kutoka kwao.
Lakini
anazidi kusisitiza ya kwamba kujifunza ni lazima uweze kusoma vitu mbalimbali
ambavyo vitakujenga katika kukuongezea maaarifa katika biashara unayotaka
kuifanya. Kwa mfano unaweza ukatembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio kila
wakati kuna vitu vingi ambavyo vitakujenga sana, endapo utaamua kutenga muda
wako kwa ajili ya kujifunza.
6. Unahitaji uvumilivu.
Mara
baada ya kuyajua hayo yote, jambo la mwisho ambalo unatakiwa kulifanya ni kuwa
mvumilivu. Uvumilivu ndiyo siraha thabiti ya wewe kusonga mbele zaidi. Hivyo ili
uweze kufanikiwa zaidi ni lazima uukumbuke ule usemi usemao mvumilivu hula
mbivu.
Mpaka
kufika hapo sina la ziada niwatakie wasomaji wenzangu kazi njema na mafanikio
mema.
Kwa
niaba ya uongozi wa blog hii ya dirayamafaniko.blogspot.com nipende kumshukuru ndugu yangu Saidi kwa hicho
alichotushirikisha siku ya leo.
Je
ungependa na wewe uweze kutushirikisha somo lolote la mafanikio siku ya jumanne
ijayo? Kama jibu ni ndiyo tuma neno MAFANIKIO TALK kwenda 0757909942
au tuma neno hilo hilo kwenda barua pepe yetu ambayo dirayamafanikio@gmail.com
nasi tutakutafuta kwa ajili ya kufanya mahojiano mubashara.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya,
Jun 26, 2017
Hiki Hapa Ndicho Kinaongoza Mafanikio Yako.
Kitu
kinachoongoza matendo yako au hatua za namna fulani unazochukua kwenye maisha
yako ni zile picha unazoweka kichwani mwako jinsi unavyotaka maisha yako yawe.
Huwezi kuchukua hatua kubwa kama picha ulizonazo ni kidogo.
Ndio
maana, kila wakati tunasisitiza ni muhimu sana kuwa na picha sahihi, maana
picha hizo zitakuongoza pia kuchukua hatua sahihi. Hebu jiulize hapo, picha
ulizoweka kichwani mwako kila wakati ni zipi?
Je,
unaona nini kwenye maisha yako? Unaona kufanikiwa au unaona kushindwa? Kama
unaona kufanikiwa, uwe na uhakika ni lazima utachukua hatua kubwa sana za
kukufikisha kule unakotaka kufika.
Kila
wakati, jitahidi kuongozwa na picha sahihi za mafanikio unayoyataka, ili picha
hizo zikusaidie pia kuchukua hatua kubwa. Hatua anazochukua mtu kwenye maisha
yake, ni ushahidi tosha kwa mtu huyo ana picha gani kichwani mwake.
Huhitaji kupiga ramli, huhitaji muujiza wowote ule. Ukitaka kujua mtu huyo anawaza nini
juu ya maisha yake au atafika wapi kimaisha, angalia hatua anazochukua, hizo
zitakuonyesha mtazamo na picha alizoweka kuhusu maisha yake.
Jun 25, 2017
Jitoe Kikamilifu Na Boresha Maisha Yako Kila Siku Hivi…
Hitaji
lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni
kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea yaani learn, grow and develop. Hili ndio hitaji lako la kwanza.
Kila
wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au hicho
unachokifanya ili kuleta matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo
na hata kesho ili kikupe mafanikio
Unaweza
ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha
tabia, biashara au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi. Unapoboresha
kila eneo unajikuta ndio unazidi kufanikiwa.
Kuendelea
kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako, kila siku jiulize, ni kwa namna
gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha
maisha yako yakawa bora kuliko jana?
Jifunze kila wakati kufikia mafanikio yako. |
Kufanya
mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda (Becoming
a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili
kuwa mbobezi kwa hicho unachokifanya.
Hakuna
mpaka wa kuboresha maisha yako. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya
hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa tena kwa viwango vya juu.
Lakini
mafanikio hayo ninayaongelea hapa hayawezi kuja kama upepo wa kipunga au hayawezi kutokea
usiku eti umelala na ukiamka ukawa tajiri, kumbuka inachukua muda hadi
mafanikio yako kujengeka.
Kuwa
mvumilivu katika kipindi ambacho ndoto zako zinapitia kwenye mchakato wa
kuelekea kufanikiwa, vinginevyo hautaweza kufanikiwa kwa kitu chochote zaidi
utaendelea kuacha ndoto zako nyingi zikiwa hewani.
Kujitoa
kikamilifu na kuboresha maisha, fanya iwe ndio kanuni kuu ya maisha yako. Kwa
wenzetu wa Japan kanuni hii wanaiita KAIZEN. Hio ikiwa na maana wao hujifunza
sana katika hili la kuboresha maisha yao
kila siku.
Wajapan
wakiwa tokea vijana wadogo wanajifunza juu ya hili na kuchukua hatua za
kuboresha maisha yao na limejenga na kuwa utamaduni mzuri ambao kila mtu anaufuata
kwenye maisha yao.
Hata
wewe huhitaji kulala, angalia kila eneo la maisha yako ambalo haliko sawa, amua kuliboresha kwa guvu zote na kwa
bidii kila siku. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Chukua
hatua kwa kufanyia kazi haya uliyojifunza leo yawe sehemu ya maisha yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jun 21, 2017
Epuka Kufanya Mambo Haya Katika maisha Yako.
Kwa kawaida, yapo mambo manne tu ambayo yanafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa, lakini si hivyo tu hayo ndiyo ndiyo mambo ambayo karibu maskini wote duniani wanayafanya sana maishani mwao. Na kwa kuendelea kufanya mambo hayo iwe kwa kujua au kutokujua ni chanzo kikubwa sana cha kuvuta umaskini kila iitwapo leo. Ikiwa hata wewe utaendelea kufanya mambo hayo sahau kutoka kwenye umaskini, hata ufanyaje utaendelea kubakia hapo.1. Kulalamika.
Watu wengi tumekuwa ni wazuri sana katika kona hii, hata kwa vitu ambavyo tunavimudu. Ulamikaji huu huenda sambamba na visingizio ambavyo kwa upande chanya havina mashiko kabisa, Hata hivyo inasadikika ya kwamba walalamikaji wengi huwa ni ngumu kufanikiwa katika maisha yao, chunguza hilo kisha uone ukweli juu ya jambo hili.
Endapo utachukua jukumu la kuwauliza watu wengi ni kwa nini wanakuwa hivyo walivyo leo, majibu yao unaweza sema labda dunia haina usawa, kumbe ukweli ni kwamba hakuna aliyewahi kependelewa katika dunia hii, kwa sababu katika sayari hii vitu vilivyopo vipo sawa kwa ajili ya watu wote. Hebu tazama masaa wote tuna masaa sawa. Sasa utafauti wetu unakuja wapi?
Ukweli ni kwamnba utofauti wetu unakuja pale ambapo tunakuja kuyatumia masaa haya, hapo ndipo yanapatengenezwa yale makundi mawili ya waliyonacho na wasionacho. Hivyo ili tuweze kutengeneza makundi sawa ya walinacho pekee, tunachotakiwa kufanya na kuacha kulalamika hasa kwa mambo ambayo hayana msaada wowote katika maisha yetu.
2. Kulaumu wengine.
Kama wewe ni mtu wa kulaumu wengine kwa kila kitu na kujiona ni mtu wa kutokosea , sahau kutoka kwenye umaskini. Huu ni kweli ambao upo wazi, kwa sababu watu wengi tupo katika maisha ya kawaida kwa sababu ya kukaa na kulaamu watu wengine. Kufanya hivi ni kulisindikiza jua kutimiza wajibu wake. Kwa kila kitu ambacho unakifanya acha mara moja kunyooshea kidole watu wengine na badala yake unachotakiwa kufanya fanya kazi kama vile dunia hii unaishi pekee yako.
3. Kutokuwajibika katika maisha yako.
Hutakiwi kulaumu serikali, ndugu, jamaa au wazazi wako ya kwamba wao ndio wamefanya maisha yako yawe hivyo. Wewe ndiye mtu wa kwanza wa kuwajibika na maisha yako. Hivyo unachotakiwa kufanya kila wakati ni kuhakikisha unatoa maaumuzi sahihi hasa katika maisha yako. Hata kama dunia nzima haita tambua mchango wako, mathalani wewe unajua ni nini ambacho unakitaka basi nakusihi uendelee kupana mpaka tone la mwisho.
4. Kutokuwa na shukrani.
Hiki ni kipimo tosha kwamba unafanikiwa au hufanikiwi. Kama huna shukran hata kwa kidogo unachopata, mafanikio makubwa kwako itabaki hadithi. Hivyo kwa kila wakati jambo la kwanza unalopaswa kulipa kipaumbele ni ile hali ya kuwashukuru watu wote walifanikisha wewe kuwa hapo ulipo ukianza na mwenyezi Mungu, kisha watu wengi ndiyo wafuate.
Tunakutakia Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa..
Kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki yako katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com
Jun 19, 2017
Namna Unavyoweza Kuishi Katika Ulimwengu Wa Wakatishaji Tamaa.
Dunia
ya leo imejaa maneno mengi kuliko watu waliopo katika dunia hiyo. Hebu fikiria
ya kwamba tafiti za wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza
maneno 16000 kwa siku, wakati wanaweke wote duniani kwa kila mmoja mmoja
huzungumza maneno 25000 kwa siku, kwa tafiti hizi najaribu kuwaza hivi tuna watu wangapi? Na kila mmoja
akizungumza maneno yake tutakuwa na maneno mangapi?
Najaribu
tu kuwaza kwa sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya
watu. Nasema hayo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na
katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao
huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyohivyo sawa na kusema.
Hata
hivyo maneno ya watu ambayo yapo katika dunia hii ni yale ambayo yanatengeneza
ulimwengu mpya, ulimwengu huo huitwa ulimwengu wa taarifa,
katika ulimwengu huo yapo mengi ambayo utayasema na mengine utayasikia, na
katika ulimwengu huohuo taarifa hizo hizo ambazo utakuwa unazisikia, yapo yale
yatakayokujenga, lakini yapo yale ambayo yatakufanya uvurugike kabisa.
Na ukweli ni kwamba maneno ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson hii ni kwa mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa zimejaa tarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele kimaisha.
Na
mara kadhaa hali hii hutokea na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye
maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe.
Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho
kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa
wewe jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo,
tunachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia
kuendesha maisha yako, kwa sababu kama ukifanya hivyo utaumia sana na utaiona
dunia chungu. Hivyo ni vyema ukaamua kuishi
wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma kukufanya. Kufanya
hivyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
Tumalizie
kwa sema ya kwamba endapo utamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza
wakatishaji tamaa katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku
zote za maisha yako. Lakini pia faida nyingine ambazo utazipata pale ambapo
utamua kuishi maisha ya kujitolea hukumu, utakuwa na uhuru mkubwa katika kutoa
maamuzi yako.
Asante
sana kwa kuwa nasi, tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya
mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
dirayamafanikio.blogspot.com.
Jun 16, 2017
Faida Utazozipata Mara Baada Ya kuacha kufanya Mambo Ya Msingi Kimazoea.
Wakati
nikiwa mdogo niliwahi kusikia wakubwa wangu wakisema ya kwamba mazoea yana
tabu, kwa kipindi kile sikujua walikuwa wanamaanisha nini, ila kadri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kuelewa walikuwa wanamaniisha nini.
Nilichokuja
kukigundua juu ya msemo huu ni kwamba mawazo ya binadamu ni mawazo ya mgando,
naweza nikasema hivyo kwa sababu akili zetu tumezielekeza katika kufanya mambo
katika mazoea. Kama mtu amezoea kula ugali muda wa mchana basi mtu huyo ukimpa
wali muda wa mchana basi utamsikia mtu huyo akisema kwa kweli mimi kula wali
mchana zijazoea.
Kwa
mfano huo, angalia watu ambao wanafanya biashara fulani ambazo hazilipi, ukimwambia
wafanyabiashara hao wafanye biashara nyingine watakwambia ya kwamba hawawezi
kufanya biashra ambayo hawaijaizoea. Kwa majibu ya aina hiyo ndipo
nianapokubaliana na usemi ule usemao ya kwamba mazoea yana tabu, hii ni kwa
sababu watu wengi tunashindwa kufanya vitu vingine tofauti na tulivyovizoea.
Zijue faida za kutokufanya kazi kimazoea. |
Lakini
kama kweli unataka mafanikio ya kweli ni vyema kwa jambo lolote ambalo
unalifanya acha mara moja tabia kufanya vitu kwa mazoea kwani mazoea ni dalili
za uvivu, unashangaa huo ndio ukweli ambao upo wazi. Hivyo kwa kila jambo
ambalo unalifanya hakikisha ya kwamba unatafuta mbinu nyingine za kuweza kuwa
bora zaidi.
Lakini
pia unashauriwa ya kwamba Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo haja
na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale mazoea
uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa
mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri.
Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea
yako.
Hivyo
kila dakika na kila sekunde, kama kweli unataka kuondoka katika hali uliyopo
kwa sasa unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuachana mara moja ile tabia ya
kuishi katika misingi ya kimazoea (comfort zone) ambayo umeyazoea, na kufanya
hivi itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa
ya kukuwezesha kufika mbali zaidi kimafanikio.
Endapo
utandokana na hali ya kufanya vitu kwa mazoea tegemea kupata mambo makubwa ya
fuatayo;
1 1. Utapata
mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, hii ni kwa sababu utaongeza uwezo na muda wako wa kufanya kazi.
2. Lakini
pia kama utaondokana na ile tabia ya kufanya kazi kwa mazoea basi jiandae kuwa
mtaalamu kwa jambo ulifanyalo.
Hivyo
tumalize kwa kusema ya kwamba unatakiwa kuachana mara moja tabia yako ya
kufanya vitu kwa mazoe.
Tukushuru
sana kila wakati kwa kuwa sehemu ya mafundisho
haya kila siku, endelea pia
kuwashirikisha wengine.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya
mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com.
Jun 15, 2017
Aina Kubwa Tatu Za Watu Na Nafasi Zao Katika Mafanikio.
Wewe ni Mtu wa aina gani?
Hili ni swali ambalo kimsingi kila
mmoja lazima ajihoji kwa wakati wake.
Ukisoma
katika vitabu mbalimbali vya dini vinasema ya kwamba binadamu wote ni sawa, hii
ikiwa na maana ya kwamba ukiangalia katika mfano wa vitu kijinsia, organi
pamoja homoni.
Lakini
ukija katika ulimwengu wa mafanikio binadamu hatufanani hata chembe na hii
ndiyo maana kuna watu maskini na wengine ni matajiri, na nilichokigundua ni
kwamba utofati wetu huanza rasmi katika fikra.
Fikra
ndiyo inayotufanya tuweze kuwa tofauti. Hivyo ili binadamu tuweze kuwa sawa ni vyema kila mtu aweze
kutafakari yeye ni mtu wa aina gani? Ukishapata majibu ndipo utapojua wewe ni wa aina gani na unawezaje kusonga
mbele kimasha.
Ili
mkupata majibu ya swali hilo, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia
kuweza kujua wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo yafutayo ni makundi ya watu ambao
wapo hapa duniani katika kuyasaka mafanikio.
Watazamaji.
Aina
ya kwanza ya watu wanaopatikana katika duniani hii ni watazamaji. Tabia za watu
hawa huwa kama ifuatavyo;
Wao
ni waoga katika kujaribu kufanya kitu kipya.
Wao
huamini zaidi katika kushindwa kuliko kufanikiwa.
Wao
ni wazungumzaji wazuri kwa yale ambayo yanatokea katika jamii. Watu hawa huzungumza zaidi masuala ambayo huwa
hayawasaidii mfano wa mambo hayo ni mpira, siasa na matukio mbalimbali
yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mambo ya nje ya mitandao ya
kijamii.
Lakini
kubwa kabisa watu hawa huwa hawana
ubunifu wowote, na huwa wanaishi katika misingi ya kuwaangalia watu wanaopenda
(role model), kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba aina hii ya watu huishi
maishi ya ganda la ndizi, kwa sababu husubiri mtu afanye jambo fulani ili na
wao waanze kufanya.
Wapotezaji.
Kundi
hili lina watu lukuki sana. Na watu ambao wapo katika kundi hili huwa wana
tabia zifuatazo;
Kazi
yao kubwa huwa ni kuwangalia watu wengine wanafanya nini katika maisha yao.
Hata hivyo katika kundi hili, watu wengi huwa wapo kwa ajili ya kuwakosa
wengine kwa yale wayafanyao, na katika kukosoa huko huwa ni katika kukatisha
tamaa zaidi kuliko kujenga.
Watu
ambao wapo katika kundi hili ni wale ambao wameathiriwa kwa kiwango kikubwa
ugonjwa wa wa kuahirisha mambo ya msingi.
Washindi.
Kundi
la tatu la mwisho ni kundi la washindi, kundi hili ndilo lenye watu wachache na
wenye mafanikio. Na kundi hili lina watu wachache kwa sababu watu wengi
wameng’angana’ katika makundi mengine ambayo nimekwisha yaelezea hapo awali.
Watu
ambao ambao wapo katika kundi hili huwa
wanasifa zifutazo;
Wao
hujua ni nini wanachokitaka katika maisha yao.
Wao
hupanga na kukamilisha yale waliyoyapanga kwa wakati.
Lakini
kubwa zaidi watu ambao wapo katika kundi hili huwa si wabinafsi kama walivyo
makundi wangine, wao huwa wapo tayari kuwasaidia wengine.
Pia
ni watu ambao wamewekeza muda mwingi
sana katika kujifunza na kutafakari.
Hayo
ni machache kati ya mengi yaliyopo katika kundi hili.
Hayo
ndiyo makundi matatu yaliyopo katika ulimwengu huu, Mara baada ya kuona makundi
matatu ya watu yanayotufautisha hapa duniani. swali linakuja wewe mwenzangu na
mimi upo kundi gani? Kama unahisi upo kundi ambalo hustahili, unachotakiwa
kufanya ni kuhama mara moja na kuhamia katika kundi lenye mafanufaa kwako.
Asante
kwa kuwa pamoja nasi kila wakati nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson
Chonya.
0757909942,
dirayamafanikio.blogspot.com
Jun 14, 2017
Hapa Ndipo Chimbuko La Mafanikio Yako Linapoanzia.
Mara
zote tunakumbushwa ya kwamba ajianavyo mtu ndivyo alivyo. Miongoni mwetu
tumekwisha kukataa tamaa ya maisha kabisa, wengi tumeshapoteza matumaini kwa
kiwango kikubwa, hatuamini kama ipo siku ambayo tutatafanikiwa, wengi tumejiona
hatuna mamlaka ya kupata kile tunachokitaka.
Na
hali hii imejitokeza ndani yetu baada ya kuanza kuishi mawazo ya watu wengine,
wengi tumekuwa tukiwatazama wengine hasa pale ambapo wameshindwa hivyo, kujiona
ya kwamba na sisi hatuwezi. Ila ninachotaka kukwambia ya kwamba kushindwa kwa
wengine liwe somo kwako ili uweza kufanikiwa zaidi.
Hii
ni kwa kwa sababu hali yoyote ile ambayo inatoka nje ya wewe haina mchango
mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio
yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani
mwako tu.
Piga kazi mpaka kieleweke kuleta mafanikio yako. |
Hali
hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha
yako. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona
ni kwamba utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Ni
vyema kutafakari hivyo kwa sababu haijalishi watu wanasemaje au watasema nini
juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani
yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba
wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio
basi ni lazima utafanikiwa.
Kitu
kikubwa hapa unachotakiwa kujifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje
katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Hii ni kwa sababu wengi wetu ni wazuri sana
katika kulaum watu wengine ya kwamba wao wamesababisha wewe kuwa hivyo ulivyo
leo na inawezekana sababu hiyo ukaiona
ina mashiko sana kwa upande wako, ila ninachopaswa kukwambia ni nyanyuka upya
kwa kuanza kufikiri upya na pia dawa ya wapuuzi ni kuwapuuza.
Nasema
hivyo kwa sababu anakuzuia kupata
mafanikio yako ni wewe mwenyewe pamoja na mawazo hasi unayozidi kuyabeba kila
wakati. Narudia kusema tena uduni wa maisha yako hausababishwi na mtu mwingine bali wewe mwenyewe. Hivyo ni
jambo lenye busara sana ambalo ni vyema kuanzia leo, amua kujenga hali bora
ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
Hivyo
ni malize kwa kusema ya kwamba huwezi kutokea kwa jirani bila kuanzia kwako,
hii nikiwa na maana acha kulamu watu wengi anza kuona maisha yako mkoseaji
mkubwa ni wewe ni si mtu mwingine, hata kama ni kweli mtu mwingine ndiyo sababu
ya wewe kuwa hivyo ulivyo ninachotaka kukusihi ni kwamba ni tafuta mbadala wa
kutatua changamoto inayokukabili na si kuwa walaam watu wengine.
Asante
kwa kuwa msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio nakusihi
uwashirikishe na wengine kadri uwezavyo.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya
mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com
Jun 13, 2017
MREJESHO; Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo-03
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini
yetu u mzima wa afya tele, kwa upande watu sisi hatujambo kabisa. Wiki
iliyopita tulipata kusoma kisa kimoja mahala hapa ambacho kilimuhusu mfalme Mhavila
pamoja na mama mjane. Kisa hiki kilikuwa ni cha kusisimua sana.
Ambapo
tulikisimulia kwa siku mbili na watu wengi walitutumia ujumbe mzuri ya kwamba
wamejifunza mengi sana kupitia kisa kile. Hivyo kwa kuwa tunatambua mchango
wako kwetu , hivyo tukaamua kukupa nafasi wewe msomaji wetu uweze ulichojifunza
kutokana na hadithi ile;
Watu
wengi sana walitutumia maoni yako miongoni mwa maoni hayo ni;
Naitwa FURAHA MWIKOMBO kutoka Uyole Mbeya.
Kwanza
kabisa nipende kuwapongeza waheshimiwa kwa elimu mnayotupatia katika kundi la
whatsapp, facebook na blog yenu ya DIRA YA MAFANIKIO.
Mimi nilichojifunza kwenye hadithi
hii ni;
1. Kudharau
kazi ya mtu hakuna faida yeyote.
2. Kushukuru
kwa kile kidogo unachokipata na kuwasaidia wengine. Ni jambo la busara.
3. Mungu
anapotupima heshima na upendo wetu huwatumia wale walio chini yetu, mfano
viwete, vilema, vichaa na wenye shida kama ambavyo alitumia njia hii mfalme
mhavila.
4. Mara
nyingi bahati, riziki na mafanikiohuwa ni vitu vilivyojificha sana, tukivumilia
na vitatokea baadae sana.
Karibu tuongee mafanikio kila JUMANNE hapa DIRA YA MAFANIKIO. |
Naitwa SHABANI SAIDI kutoka Dodoma
Mambo makubwa matatu ambayo
nimejifunza kutoka kwenye hadithi hii ni;
1. Anayewashweshea
wengine kwa ukarimu na yeye pia atanyweshwa kwa ukarimu.
2. Usiwanyime
watu mema watu wanayostaili ikiwa mkono wako una uwezo wa kufanya.
3. Usimwambie
mwenzako nenda kasha urudi na kesho nitakupa kumbe una kitu unachokihitaji.
Naitwa SIMONI MAPUNDA kutoka mbinga.
Mimi nilichojifunza kwenye hadithi
hii ni;
Kwamba kuwa mkarimu kwa watu wote ni siraha, hata
kama huna kitu fanya kitu kwa msaada wa wengine, kupitia ulichonacho hajalishi
wewe ni maskini, mjane, yatima, kilema au una madaraka amini una uwezo wa
kufanya makubwa.
Naitwa ISRAEL NDANG, kutoka Mwanza –Tanzania
Kupitia
hadithi ya mfalme mhavilia nimejifunza
mambo yafutayo;
1.
Nimejifunza
kutoa pasipo kutegemea malipo, hivyo kila wakati toa mazuri kwa wengine kadri
uwezavyo huku ukijua Mungu ndiye mlipaji wa fadhira zako.
2.
Fursa
zinaweza kukujia kwenye hali ngumu na utata mwingi ama katika mazingira magumu,
hivyo usiyatilie maanani mazingira hayo bali wewe pambana mpaka uweze kupata
mafanikio.
3.
Tuwe
wakarimu, wanyenyekevu na hata wasikivu pia ili kuelewa hisia za binadamu
mwenzetu pia.
TANGAZO MUHIMU
Asante sana kwa wale wote ambao
walituma maoni yao kwa namna moja ama nyingine, maoni yako tuliyapenda na kuyapokea kwa mikono miwili.
Tulichokigundua ya kwamba watu wengi wana mambo mengi sana ambayo yatausaidia
sisi pamoja na wewe kuweza kufanikiwa na kufika mbali zaidi..
Hivyo kwa kulitambua hilo uongozi wa
mtandao wa DM tumeamua kuanzisha kitu kinachoitwa Mafanikio Talk (M.T), hiki ni kipindi maalumu kabisa
ambacho kitakuwa kinahusisha mahuzungumzo baina ya uongozi wa mtandao huu wa
dira ya mafanikio pamoja na wewe msomaji
wetu.
Tutakochokifanya ni kwamba
tutakupigia simu na kufanya mazungumzo na kile ulichokizungumza tutakwenda
kukiweka hapa siku ya jumanne Ili watu wengine wajifunze kutoka kwako.
Je ungependa kuwa wa kwanza kufanya kipindi
hicho cha Mafanikio Talk (M.T)
siku ya jumanne ijayo? Kama jibu ni ndiyo tuma ujumbe mfupi wa maandishi
ukianza na neno Mafanikio Talk
kisha jina lako na mahali ulipo kwenda-0757909942/ au email yetu dirayamafaniko@gmail.com nasi tutakutafuta kwa ajili ya kufanya
mazungumzo hayo.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya
mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)