Jun 12, 2017
Ifahamu Misingi Hii Ya Kuilea Ndoto Yako ili Uweze Kufanikiwa.
Katika
ulimwengu huu wa teknolojia kila mmoja wetu ana ndoto yake, na kila miongoni
mwetu anatamani siku moja ndoto iwe kweli. Ila changamoto kubwa huwa inakuja ni
kwa jinsi gani unaiweza kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli. Wengi wetu ndoto zetu
ni za mdomoni tu, huwa hazina uhalisia wa jinsi ya kuzikamilisha ndoto hizo.
Lakini
siku zote ikumbukwe katika safari ya mafanikio, kuwa makini sana na jinsi
unavyoitunza na kuilea ndoto yako. Kama ndoto yako unaitunza na kuilea katika
hali ya hofu na mashaka sana basi, utavuna magugu na hautaweza kufanikiwa.
Wengi
wetu tumekuwa tumeweka mitazamo hasi juu ya ndoto zetu, wengi tumekuwa
tukiyatazama mambo katika mtazamo hasi, wengi tumekuwa hatujui namna na jinsi
ya kuzitimiza ndoto zetu. Kwa mfano, unaweza ukakuta mtu anatamani kuwa
mfanyabiashara fulani, lakini cha ajabu ukimuuliza mtu huyo ni mikakati gani
ambayo amejiwekea ili kukamilisha ndoto yake hiyo, utakuta hakuna mkakati hata
mmoja.
Lea ndoto yako katika msingi mkubwa wa kujiamini, utafanikiwa. |
Najaribu
kujihoji kwa sauti ya nne, hivi kwa kufanya hivyo ni kuijenga ndoto yako au ni
kuibomoa? Bila shaka kufanya hivyo ni kuibomoa ndoto yako na hatimaye
kujiandalia makazi ya kiumaskini.
Lakini
ukweli ni kwamba ili uweze kutimiza ndoto yako unatakiwa kuitunza na kuilea ndoto
hiyo katika misingi ya imani na matumaini
makubwa ya kimafanikio, lakini pia ni lazima uweze kujiamini kila wakati, hii
ni kwa sababu wapo wengi wanaoshindwa kufikia ndoto zao kwa sababu ya kuzielea
ndoto zao katika mazingira mabovu.
Kama
ulivyo mmea ili ukue ni lazima umwagaliwe maji safi, halikadhalika ndoto yako iko hivyo hivyo. Ni lazima ndoto yako
ituzwe kwa matumaini na imani ya mafanikio na sio kuitunza katika hofu na woga
ambapo mwisho wa siku ni lazima utakwama.
Hivyo
kwa kuwa wewe ndiye mmliki wa ndoto yako hakikisha unaweka mikakati imara
ambayo itakufanya uweze kufika pale ambapo unapopataka, kwani endapo utafanya
kinyume chake ni kushindwa kutimiza kutimiza
kusudio lako hapa duniani.
Hivyo
kila wakati jaribu kutafakari juu ya mambo haya;
Najua
hapo ulipo una ndoto ya aina fulani, jiulize
Unailea ndoto yako katika mazingira yapi?
Je, unajiamini ya kwamba utafanikisha ndoto yako?
Au upo kwenye
mazingira ya mashaka na hofu?
Lakini
ikumbukwe ya kwamba mazingira yoyote yale unayoyatumia kuilelea ndoto yako
yanakupa jibu kama utafanikiwa au hautafanikiwa kuifanikisha ndoto yako. Hivyo
ni vyema ukatafakari kuhusu mazingira uliyopo kwa sasa kama ni kweli ndoto yako
itatimia au haitatimia.
Imeandikwa na
uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com
.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.