Jun 2, 2017
Kufanikiwa Huenda Sambamba Na Kitu Hiki.
Ukisikia
neno kufanikiwa , katika akili yako kwa harakaharaka huwa kinakujia nini? Maana
watu wengi tumekuwa hatafahamu juu ya neno kufanikiwa. Wengi wetu hudhani ya
kwamba neno kufanikiwa, ni mafanikio yako binafsi tu, hivyo ndivyo ambavyo
wengi wetu hudhani.
Lakini
ukweli ni kwamba ili yaitwe mafanikio ni lazima kufanikiwe kwako kuwe na
matokeo chanya kwa watu wengine, huwezi sema umefanikiwa kama jamii na watu
wengine waliokuzunguka wakiwa bado katika shida,hayo siyo mafanikio.
Ila
mafanikio ni ile hali ya wewe kuweza
kuwasaidia watu wengine pia, huko ndiko tunakosema kufanikiwa. Wengi wetu
tumekuwa wabinafsi sana katika mambo yetu mbalimbali tunayoyajua, tumekuwa
tukiyona mafanikio katika maisha yetu tu, lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo
si sawa hata chembe.
Lengo lako kubwa la maisha liwe ni kusaidia wengine. |
Ukweli ni kwamba neno kufanikiwa ni lazima kuwe na mahusiano ya wazi baina yako
na watu wengine. Jaribu kuchukua dakika chache kisha uwaze je watu wengine
wamekuwa wakinufaika nini kutoka kwako? Usinipe jibu. Kwa maana majibu unayo
wewe.
Ila
naomba nikusisitize kwa kusema ya kwamba jijingee nafasi ya kuwasaidia wengine
kama unataka kufanikiwa zaidi, kwani unapofanya hivyo, ndivyo ambavyo
unavyopata Baraka za kimafaniko zaidi. Kwani katika hili kuna usemi ambao
husema anayetoa ndiye anayepokea zaidi.
Hivyo
kila wakati jijengee uwezo ndani yoke kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine
haijalishi ni hali gani ambayo unayo. Najua
hapo bado njia panda kwamba nazungumzia nini? Usiajali nipo kwa ajili
yako.
Ninachotaka
kukwambia ni hivi jamii inayokuzunguka ni lazima inufaike kupitia wewe, nawe
utanufaika zaidi kupitia jamii hiyo. Huwezi kusema unataka kufanikiwa wakati hauna
mahusiano mazuri na watu wengine. Hivyo kila wakati kama kweli unataka
kufanikiwa jitahidi kuwasaidia watu wengine kwa kutoa mchango wako, ili siku
moja watu hao waje watamke kwa vinywa vyao kwamba mafanikio yangu yamechngiwa
na mtu fulani.
Lakini
pia kufanikiwa huenda sambamba na utoaji wa sadaka. kwani kuna mahali niliwahi
soma, mwandishi alisema ya kwamba kutoa sadaka ni kumkopesha
mwenyezi Mungu, huwezi kuema hufanikiwi wakati hutoi sadaka kwa
ajili ya kuwasaidia watu wengine. Hivyo kila wakati kama unataka kufanikiwa
zaidi jitahidi kutoa sadaka kadri uwezavyo.
Na daima ili uweze kufanikiwa yakumbuke maneno haya ya kwamba mkono
unatoa zaidi ndiyo mkono upokea mara dufu.
Hivyo
jijengee mazoea ya kutoa sadaka na kuwapa mawazo watu wengine ambayo
yatawajenga kwa namna moja ama nyinyine. Hivyo ni vyema ukafikiria na kuona na
kwa jinsi gani unavyoweza kuinufaisha jamii yako kwa hicho kidogo ilichonacho.
Mpaka
kufikia hapo ndugu yangu sina la ziada ya kusema hakikisha ya kwamba unakuwa
ngao zaidi ya watu wengine kwa kutoa mchango wako kwa namna moja ama nyingine. Nikiutakie siku njema na utekelezaji mwema.
Ni wako : afisa mipango Benson Chonya
0757909942
dirayamanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.