Jun 6, 2017
Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo - 2.
Wiki
iliyopita tuliona mara baada ya mama mjane kumualika mfalme Mhavila nyumbani
kwake na kukubaliwa, lakini alimsubiri sana Mfalme hakutokea,na akajikuta
amegawa chakula kwa mfalme kwa watu wengine, akiwa katika kusubiri huko ghafla
alisikia hodi.
Mama
mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme Mhavila
akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini mfalme Mhavila
kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme Mhavila alifika kwa mama mjane
na kusema asante sana kwa kunijali.
Mama
mjane aliwaza na kusema mfalme Mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati
sijamfanya chochote? wakati mama
akitafakari amemjali kwa lipi mfalme Mhavila mama mjane hakupata majibu, lakini
pili mama mjane aliwaza katika halmashauri yake ya kichwa atampa chakula gani,
na ili hali chakula kulikuwa kimekwisha chote.
Wakati mama mjane unawaza kwa kweli hakupata
majibu, zaidi ya maswali lukuki yaliyokuwa yakizidi kumiminika katika akili yake.
Kabla hajapata jibu hata moja katika maswali yale ambayo alikuwa anajihoji, aliwaza
tena iweje tena mfalme Mhavila kachelewa kiasi kile, lakini alizidi kuwaza
imekuwaje mfalme Mhavila kaja na watu lukuki kiasi kile huku wakiwa katika hali
ya furaha kiasi kile?
Wakati maswali hayo yote yakiwa katika
halmashauri yake ya kichwa cha mama mjane pasipo majibu yake, mfalme Mhavila
alimuamuru mama mjane waingie ndani kwake mama mjane kwa ajili ya kufanya
mazungumzo kidogo, wakati mama mjane akiwa haelewi ni nini cha kufanya, basi
aliingia ndani kwa ajili ya kumsikiliza mfalme Mhavila, japo mama mjane aliwaza
atampa nini mfalme Mhavila kwani chakula kilikuwa kimekwisha liwa na watu
wengine ambao walijitokeza mchana.
Basi ikawa asubuhi ikawa jioni, wakafika ndani
kwa mama mjane, mfalme Mhavila akarudia tena kumshukuru mama mjane kwa kusema
asante sana kwa kunijali, pia asante kwa kushiriki kwa pamoja kwa chakula chako
cha mchana ambacho tulikula kwa pamoja kwa kweli kilikuwa kitamu sana asante
sana mama.
Mama mjane akafungua kinywa chake huku akiona
aibu, iliyojawa na mshangao, kwa kula chakula? Chakula kipi mfalme? mama
mjane alihoji, huku akizidi kusema wakati mimi nilikusubiri hakufika na chakula
nimekigawa chote.
Alipomaliza kuweka nukta mama mjane , mfalme Mhavila
naye akadakia oooh usijali mama wale watu wote walikuja kula chakula pamoja na
maji niliwatuma mwenyewe, hata hivyo nilifanya vile kwa maksudi kabisa, ili
kuona una huruma kiasi gani cha kutoa kwa watu usiwajua? Hivyo majibu ambayo
nimeyapata yamenipa picha nzuri sana, ambayo kimsingi nimeelewa sana ni kwa
jinsi gani ulivyo mkalimu.
Kama uliweza kuwatendea vema vijana wangu wale
usiowajua, nina imani moyo na hali uliyonayo wewe ni mkalimu sana. Hata hivyo
nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa mara nyingine kwa ukalimu wako.
Wakati mfalme Mhavila anasema hayo, mama mjane alishangaa sana, kumbe wale vijana na yule mtoto walikuwa wametumwa na mfalme? Mama mjane aliwaza katika fikra zake.
Wakati mfalme Mhavila anasema hayo, mama mjane alishangaa sana, kumbe wale vijana na yule mtoto walikuwa wametumwa na mfalme? Mama mjane aliwaza katika fikra zake.
Mfalme akaendelea kusema "Hivyo kwa
ukalimu ulionao inaonesha dhahiri shairi ya kwamba wewe ni kiongozi bora! Kwani binafsi
naamini ya kwamba kiongozi bora ni yule aliye mkalimu na mwenye huruma kwa watu
wake.
Hivyo nakushukuru sana, na kwa kuwa ulisema ya
kwamba wewe ni mjane, nitakupa mtaji wa sh. Milionio mia moja kwa ajili ya
kufungua miradi yako, na mradi ambao natamani ufungue ni ule ambao
utawasaidilia watoto waishio katika mazingira magumu hususani watoto yatima!
Nitakupa watalam mbalimbali ambao watakusidia
katika kukamilisha mpango huo, lakini pia nitakutafutia wawekezaji ambao watakusaidia katika jambo hilo.
Baada ya dakika chache mama mjane alimshukuru
mfalme Mhavila kwa kumpa wazo bora pamoja na fedha katika kuwasaidia watoto.
Mfalme Mhavila akamuuliza mama je, unadhani ni jina gani linafaa kwa ya mradi
huo?
Mama mjane aliwaza kidogo kisha akasema jina
ambalo linafaa katika mradi huo ni "mama mjane foundation" . Mfalme Mhavila hakuwa na kipangamizi
juu ya jina hilo hivyo walikubaliana libaki kama lilivyo. Hapo ndipo mwanzo wa
kubadilika kwa maisha ya mama mjane.
Mwisho mfalme Mhavila akamuahidi mama mjane
kwamba utekelezaji wa jambo hilo ungeanza kufanyika mara moja! Hivyo naamini ya
kwamba hutaniangusha katika hili, kwani naamini utafanya ‘wonders,’ wazungu husema hivyo. Basi kabla mfalme hajaondoka mama mjane akamshukuru tena katika
mambo mbalimbali ambayo walikuwa wameongea.
Lakini pia mama mjane akampa mbinu nyingine
ambayo ni njia bora sana mfalme ambayo ingesaidia katika kuleta mafanikio
katika jamii ile. Mama mjane akasema mfalme uongozi ni karama kutoka kwa Mungu
wetu, hivyo kwa kila kitu unachokifanya hakikisha unamshirikisha Mwenyezi
Mungu, lakini pia hakikisha unawashirikisha wananchi mbalimbali katika kutenda
mambo mbalimbali ya mafanikio, kwani kukaa pekee yako na kufanya maamuzi
haisaidii kwani maendeleo ni ya watu wote! Hivyo kuwashirikisha watu ndiyo
mbinu bora zaidi ya kupata mafanikio na maendeleo yenyewe.
Mwisho mfalme akafurahi kusikia kwa ushauri kutoka kwa mama mjane, wakaagana huku siku chache utekelezaji ukifuata.
Mwisho mfalme akafurahi kusikia kwa ushauri kutoka kwa mama mjane, wakaagana huku siku chache utekelezaji ukifuata.
Mwisho; Umejifunza
nini kutokana na hadithi hii, tuma ulichijifunza kupitia 0757-909942. Kwa
kuanza na jina lako na mahali ulipo nasi tutaweka maoni yako hapa wiki ijayo siku
kama ya leo.
Ni wako katika ujenzi wa mafanikio; Benson
chonya,
bensonchonya23@gmail.com
0757909942
dirayamfanikio.blogspot.com
bensonchonya23@gmail.com
0757909942
dirayamfanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.