Jun 29, 2017
Kile Unachokiweka Kwenye Akili Yako, Ndicho Hicho Kinachokufanya Ufanikiwe Au Ushindwe.
Kile
unachokiweka ndani yako, ndicho hicho unachokitoa nje. Kama unaweka au
unajirisha furaha, basi maisha yako yakatakuwa ya furaha. Kama unaingiza ndani
yako hasira, basi utatoa hasira, kama pia unaweka ndani yako mafanikio, utayapata.
Jiulize,
kuna wakati unakuwa na siku mbaya, siku ambayo hujisikii kufanya kitu kabisa,
lakini hata hivyo ukiangalia nyuma au siku moja kabla kuna mambo ambayo uliyoyaweka
akili mwako ndio yaliyokufikisha hapo ulipo.
Hata
unapoona wengine wanafuraha, wanafamafanikio ni lazima ujue kuna kitu ambacho
walichowekeza ndani yao na kikawapa furaha au mafanikio hayo ambayo unayaona
kwa sehemu kubwa kwa nje.
Kitu
unachotakiwa kuelewa, mawazo yako kila wakati yanaongozwa na hisia zako. Na hisia
zako pia zinaongoza hatua unazotakiwa kuchukua, hatua hizo zinapelekea kukupa
matokeo na mwisho wa siku matokeo hayo yanakutengenezea mfumo wa maisha
uliokamili.
Weka mambo sahihi kwenye akili yako, ili ufanikiwe. |
Kitu
unachotakiwa kukumbuka, mawazo yako hayo, hayaji kwa bahati mbaya, bali
yanatokana na vitu ambavyo unaviingiza akilini mwako mara kwa mara. Kwa vitu
hivyo unavyoingiza ndivyo vinavyokupa mawazo hayo.
Ukijichunguza
vizuri, angalia uhusiano wa taarifa unazoziweka kwenye akili yako na mtazamo
wako juu ya maisha. Hapa sina shaka, utaona ni vitu vinavyofanana. Mtazamo wako
ni lazima utaendana tu na yale mawazo yako.
Huwezi
ukawa unaweka kwenye akili yako umbea umbea au mambo ya hovyo, halafu
ukategemea kuwa na ubunifu au ukatengeneza maisha ya kimafanikio sana, hapo uwe
na uhakika sana utaishia hapo hapo.
Wewe
ni matokeo ya unavyofikiri. Hupendi hali ya maisha uliyonayo, hupendi sana hapo
ulipo, badili sana vitu unavyoingiza akili mwako. Ukibadili vitu hivyo,hata
vile unavyovitoa navyo vitakuwa na utofauti.
Kuwa
na furaha, mafanikio au kuwa mtu wa hasira hasira, ni vitu ambavyo unatengeza
mwenyewe na sio suala la muujiza wowote. Chunga sana kile unachokiingiza ndani ya
akili yako, kumbuka hicho ndicho utakachokitoa kwa baadae.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa, endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; , +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.