Jun 25, 2017
Jitoe Kikamilifu Na Boresha Maisha Yako Kila Siku Hivi…
Hitaji
lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni
kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea yaani learn, grow and develop. Hili ndio hitaji lako la kwanza.
Kila
wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au hicho
unachokifanya ili kuleta matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo
na hata kesho ili kikupe mafanikio
Unaweza
ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha
tabia, biashara au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi. Unapoboresha
kila eneo unajikuta ndio unazidi kufanikiwa.
Kuendelea
kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako, kila siku jiulize, ni kwa namna
gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha
maisha yako yakawa bora kuliko jana?
Jifunze kila wakati kufikia mafanikio yako. |
Kufanya
mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda (Becoming
a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili
kuwa mbobezi kwa hicho unachokifanya.
Hakuna
mpaka wa kuboresha maisha yako. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya
hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa tena kwa viwango vya juu.
Lakini
mafanikio hayo ninayaongelea hapa hayawezi kuja kama upepo wa kipunga au hayawezi kutokea
usiku eti umelala na ukiamka ukawa tajiri, kumbuka inachukua muda hadi
mafanikio yako kujengeka.
Kuwa
mvumilivu katika kipindi ambacho ndoto zako zinapitia kwenye mchakato wa
kuelekea kufanikiwa, vinginevyo hautaweza kufanikiwa kwa kitu chochote zaidi
utaendelea kuacha ndoto zako nyingi zikiwa hewani.
Kujitoa
kikamilifu na kuboresha maisha, fanya iwe ndio kanuni kuu ya maisha yako. Kwa
wenzetu wa Japan kanuni hii wanaiita KAIZEN. Hio ikiwa na maana wao hujifunza
sana katika hili la kuboresha maisha yao
kila siku.
Wajapan
wakiwa tokea vijana wadogo wanajifunza juu ya hili na kuchukua hatua za
kuboresha maisha yao na limejenga na kuwa utamaduni mzuri ambao kila mtu anaufuata
kwenye maisha yao.
Hata
wewe huhitaji kulala, angalia kila eneo la maisha yako ambalo haliko sawa, amua kuliboresha kwa guvu zote na kwa
bidii kila siku. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Chukua
hatua kwa kufanyia kazi haya uliyojifunza leo yawe sehemu ya maisha yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.