Jun 7, 2017
Jinsi ya kuondoka katika utumwa wa fikra.
Habari za muda huu mpendwa wangu, bila shaka u zima wa afya tele kabisa, kama ipo hivyo nashukuru sana, japo mimi afya yangu haipo vyema, ila hainizuii kuleta kusudio langu ambalo nimelipanga kusema nawe siku ya leo. Na siku ya leo nataka tuzungumze jambo moja amabalo limekuwa ni kikwazo sana katika maisha yetu kwa ujumla. Na jambo hili hili limekuwa likileta majuto sana hapo baadae.Jambo hili si jambo jambo geni bali ni jambo ni utumwa wa fikra. Utumwa wa fikra zetu ndio adui namba moja wa maisha yetu naweza nikasema hivyo, kwa sababu tumeshindwa kutambua mchango sahihi wa fikra zetu, hata kupelekea kukosa uhuru wa kifkra na kuwa ni watumwa wa fikra.
Utumwa wa fikra huanza katika kuwaza hadi kutenda. Wengi wengi tumekuwa ni watu legelege sana katika kutenda mambo ya msingi. Wengi tumekuwa tukiwaza waza juu juu tu katika kuwaza. Kutokona hali hiyo ndipo nipojumuika na yule ambaye alisema katika dunia hii hakuna kazi ngumu kama kazi ya kufikiri.
Aliyesema hivyo nafikiri alikuw yupo sahihi, kwa sababu tumekuwa watumwa wa fikra zetu. Wengi tumekuwa tukiongozwa na akili zetu, badala ya sisi kuziongoza akili zetu. Wengi tumekuwa tukikurupuka katika kuchukua maaumizi ya ghafla pasipo kutafakai, na kitendo hiki huja kuwa majuto mbeleni.
Siyo hilo tu, utumwa wa fikra zetu umeegemea zaidi katika kuambiwa zaidi, fanya hiki fanya kile, sisi tumekuwa na wapewa maaumuzi zaidi, kuluko kutoa maaumuzi. Najaraibu kuwaza kwa sauti hivi kweli tumeshindwa kuamua katika maisha yetu mpaka mtu mwingine afanye maaumuzi juu ya maisha yetu? Nawaza nakosa majaibu.
Kushindwa kuwaza vyema juu ya maisha yetu kumetufanya tushindwe kufanya mambo ya msingi ambayo tunayataka. Na kufanya mambo tusiyoyapenda ni utumwa wa fikra ambayo ni njia ambayo husaidia kulekea umaskini.
Hivyo ili uweze kuepukana na utumwa wa fikra ingefaa ufanye mambo yafuatayo;
1. Jipe nafasi ya kuwaza kuhusu maisha yako kwa kujiuliza maswali yafuatayo?
-unataka nini?
- unataka kufanikiwa katika jambo lipi?
- unataka kutimiza jambo hili kwa njia zipi?
- ni nani atakuwa msaada kwako.
Ukishapata majibu juu ya maswali hayo jaribu kutafuta majibu ya kweli, na majibu ya kweli haya ni vyema ukayafanyia kazi. Lakini mwisho kabisa hakikisha unatafuta kitu ambaho unachokipenda zaidi ndo ukifanye. Kwani kufanya kitu ambacho unakipenda ndiyo njia sahihi ya kuondoka katika kifungo cha umaskini.
By afisa mipango; Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.