Jun 27, 2017
MAFANIKIO TALK; Siri Sita Za Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio.
U
hali gani mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, tukualike kwa mara nyingine katika kipindi
hiki cha mafanikio talk ambacho
hukujia kila siku ya jumanne, ambapo siku ya leo tupo na ndugu yetu SHABANI SAIDI kutokea pale Dodoma ambapo
atukumbusha mambo ya muhimu ya kuzingatia katika biashara.
Shabani
saidi anasema ya kwamba neno biashara lina maana kuu mbili ambazo ni kitendo
cha kubadilishana bidhaa kwa bidhaa au ni kitendo cha kubadilishana bidhaa na
fedha. Lakini anakwenda mbali zaidi na kusema ya kwamba katika biashara yeyote
ambayo unaifanya ni lazima uweze kuwa na lengo la biashara hii ndiyo siri ya
kufika mbali zaidi.
Ambapo
alieleza ya kwamba katika biashara lengo kubwa ni kupata wateja zaidi, na
katika hili wengi wamekuwa hawafahamu, wamekuwa wakizani ya kwamba lengo la
kufanikiwa katika biashara ni kupata fedha pekee, lakini ukweli ni kwamba ukiwa
na lengo hilo pekee utakuwa unakosea sana.
Kwani
katika biashara ni lazima uweze kuwa mbunifu kila wakati, na ukiwa mbunifu
kutakuwa na ongezeko la wateja na ongezeko la wateja hilo ndilo litalokufanya
uweze kupata fedha, na fedha hizo zitakufanya uweze kuwa bora katika kukuza
biashara yako.
Zifuatazo Ndizo Siri Sita Za
Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio.
1. Kuwa na wazo bora la biashara.
Kuwa
na wazo bora la biashara unayotaka kuifanya ndiyo msingi mkubwa wa kuweza kufanikiwa
katika biashara uifanyayo au ambayo unataka kuifanya. Kuchagua wazo bora la
biashara huenda sambamba na kuangalia mahitaji ya watu katika eneo husika.
Kwa
mfano kama unataka kuanzisha biashara fulani
ni lazima uangalie watu hao wanahitaji
nini. Mara baada ya kujua wanahitaji nini ndipo na wewe utapata wazo la kufanya
biashara husika. Hivyo wazo bora la biashara hutokea kwa watu wanaokuzunguka.
![]() |
Zijue siri muhimu za kibiashara ili ukuze biashara yako. |
2. Kufanya uchunguzi wa eneo kwa ajili ya
kufanya biashara.
Saidi
anasema kabla ya kuanzisha biashara yeyete ile ni lazima uweze kutafuta eneo
kwa ajili ya kufanyia biashara, na si eneo tu bali ni eneo sahihi kwa ajili ya
kufanya biashara husika.
Kuchagua
eneo sahihi la kufanyia biashara ni sawa na kuchagua mke bora wa kuoa, kwani
endapo utakosea utajilaumu maisha yako yote. Hivyo kila wakati unachotakiwa
kufanya ni kuhakikisha unachagua eneo lenye uhakika katika kufanya biashara
yenye mashiko kwako.
3. Kutafuta mtaji.
Mara
baada ya kupata wazo bora la biashara, na mara baada ya kupata eneo bora kwa
jaili ya kufanyia biashara jambo la tatu, unatakiwa kuanza kutafuta mtaji kwa
ajili ya kukamilisha wazo ulilonalo.
Majibu
ya namna ya kupata mtaji yatapatikana mara baada ya kupata wazo bora la biashara, kwani mahali hapo unatakiwa
kufanya uchunguzi yakinifu. Uchunguzi huo utakusaidia kuona kubuni pia namna ya
kupata mtaji.
4. Kuwa mbunifu.
Kwa
kuwa katika dunia hii kila kitu kinafanana, hivyo ili uweze kujitofautisha na
wengine unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa mbunifu ili uweze kufanikiwa
zaidi katika biashara ambayo unaifanya, au biashara ambayo unatarajia kuifanya.
Unapokuwa
mbunifu inakusaidia sana kujenga biashara yako na kuifanya biashara hiyo
ikaonekana ya mafanikio kwa kupata wateja wengi. Popote pale utakapofanya
ubunifu kwenye biashara yako uwe na uhakika utafanikiwa.
5. Kujifunza kwa waliofanikiwa.
Mara
baada ya kutafuta mtaji unachotakiwa kufanya ni kujifunza kutoka kwa watu ambao
tayari wamekwisha fanikiwa katika biashara husika. Pia Saidi anasema ya kwamba
endapo utajifunza kwa watu ambao wameshafanikiwa unachotakiwa kufanya ni
kuhakikisha ni kuwa mbunifu zaidi ya yule ambao umejifunza kutoka kwao.
Lakini
anazidi kusisitiza ya kwamba kujifunza ni lazima uweze kusoma vitu mbalimbali
ambavyo vitakujenga katika kukuongezea maaarifa katika biashara unayotaka
kuifanya. Kwa mfano unaweza ukatembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio kila
wakati kuna vitu vingi ambavyo vitakujenga sana, endapo utaamua kutenga muda
wako kwa ajili ya kujifunza.
6. Unahitaji uvumilivu.
Mara
baada ya kuyajua hayo yote, jambo la mwisho ambalo unatakiwa kulifanya ni kuwa
mvumilivu. Uvumilivu ndiyo siraha thabiti ya wewe kusonga mbele zaidi. Hivyo ili
uweze kufanikiwa zaidi ni lazima uukumbuke ule usemi usemao mvumilivu hula
mbivu.
Mpaka
kufika hapo sina la ziada niwatakie wasomaji wenzangu kazi njema na mafanikio
mema.
Kwa
niaba ya uongozi wa blog hii ya dirayamafaniko.blogspot.com nipende kumshukuru ndugu yangu Saidi kwa hicho
alichotushirikisha siku ya leo.
Je
ungependa na wewe uweze kutushirikisha somo lolote la mafanikio siku ya jumanne
ijayo? Kama jibu ni ndiyo tuma neno MAFANIKIO TALK kwenda 0757909942
au tuma neno hilo hilo kwenda barua pepe yetu ambayo dirayamafanikio@gmail.com
nasi tutakutafuta kwa ajili ya kufanya mahojiano mubashara.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.