Jun 21, 2017
Epuka Kufanya Mambo Haya Katika maisha Yako.
Kwa kawaida, yapo mambo manne tu ambayo yanafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa, lakini si hivyo tu hayo ndiyo ndiyo mambo ambayo karibu maskini wote duniani wanayafanya sana maishani mwao. Na kwa kuendelea kufanya mambo hayo iwe kwa kujua au kutokujua ni chanzo kikubwa sana cha kuvuta umaskini kila iitwapo leo. Ikiwa hata wewe utaendelea kufanya mambo hayo sahau kutoka kwenye umaskini, hata ufanyaje utaendelea kubakia hapo.1. Kulalamika.
Watu wengi tumekuwa ni wazuri sana katika kona hii, hata kwa vitu ambavyo tunavimudu. Ulamikaji huu huenda sambamba na visingizio ambavyo kwa upande chanya havina mashiko kabisa, Hata hivyo inasadikika ya kwamba walalamikaji wengi huwa ni ngumu kufanikiwa katika maisha yao, chunguza hilo kisha uone ukweli juu ya jambo hili.
Endapo utachukua jukumu la kuwauliza watu wengi ni kwa nini wanakuwa hivyo walivyo leo, majibu yao unaweza sema labda dunia haina usawa, kumbe ukweli ni kwamba hakuna aliyewahi kependelewa katika dunia hii, kwa sababu katika sayari hii vitu vilivyopo vipo sawa kwa ajili ya watu wote. Hebu tazama masaa wote tuna masaa sawa. Sasa utafauti wetu unakuja wapi?
Ukweli ni kwamnba utofauti wetu unakuja pale ambapo tunakuja kuyatumia masaa haya, hapo ndipo yanapatengenezwa yale makundi mawili ya waliyonacho na wasionacho. Hivyo ili tuweze kutengeneza makundi sawa ya walinacho pekee, tunachotakiwa kufanya na kuacha kulalamika hasa kwa mambo ambayo hayana msaada wowote katika maisha yetu.
2. Kulaumu wengine.
Kama wewe ni mtu wa kulaumu wengine kwa kila kitu na kujiona ni mtu wa kutokosea , sahau kutoka kwenye umaskini. Huu ni kweli ambao upo wazi, kwa sababu watu wengi tupo katika maisha ya kawaida kwa sababu ya kukaa na kulaamu watu wengine. Kufanya hivi ni kulisindikiza jua kutimiza wajibu wake. Kwa kila kitu ambacho unakifanya acha mara moja kunyooshea kidole watu wengine na badala yake unachotakiwa kufanya fanya kazi kama vile dunia hii unaishi pekee yako.
3. Kutokuwajibika katika maisha yako.
Hutakiwi kulaumu serikali, ndugu, jamaa au wazazi wako ya kwamba wao ndio wamefanya maisha yako yawe hivyo. Wewe ndiye mtu wa kwanza wa kuwajibika na maisha yako. Hivyo unachotakiwa kufanya kila wakati ni kuhakikisha unatoa maaumuzi sahihi hasa katika maisha yako. Hata kama dunia nzima haita tambua mchango wako, mathalani wewe unajua ni nini ambacho unakitaka basi nakusihi uendelee kupana mpaka tone la mwisho.
4. Kutokuwa na shukrani.
Hiki ni kipimo tosha kwamba unafanikiwa au hufanikiwi. Kama huna shukran hata kwa kidogo unachopata, mafanikio makubwa kwako itabaki hadithi. Hivyo kwa kila wakati jambo la kwanza unalopaswa kulipa kipaumbele ni ile hali ya kuwashukuru watu wote walifanikisha wewe kuwa hapo ulipo ukianza na mwenyezi Mungu, kisha watu wengi ndiyo wafuate.
Tunakutakia Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa..
Kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki yako katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.