Jun 15, 2017
Aina Kubwa Tatu Za Watu Na Nafasi Zao Katika Mafanikio.
Wewe ni Mtu wa aina gani?
Hili ni swali ambalo kimsingi kila
mmoja lazima ajihoji kwa wakati wake.
Ukisoma
katika vitabu mbalimbali vya dini vinasema ya kwamba binadamu wote ni sawa, hii
ikiwa na maana ya kwamba ukiangalia katika mfano wa vitu kijinsia, organi
pamoja homoni.
Lakini
ukija katika ulimwengu wa mafanikio binadamu hatufanani hata chembe na hii
ndiyo maana kuna watu maskini na wengine ni matajiri, na nilichokigundua ni
kwamba utofati wetu huanza rasmi katika fikra.
Fikra
ndiyo inayotufanya tuweze kuwa tofauti. Hivyo ili binadamu tuweze kuwa sawa ni vyema kila mtu aweze
kutafakari yeye ni mtu wa aina gani? Ukishapata majibu ndipo utapojua wewe ni wa aina gani na unawezaje kusonga
mbele kimasha.
Ili
mkupata majibu ya swali hilo, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia
kuweza kujua wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo yafutayo ni makundi ya watu ambao
wapo hapa duniani katika kuyasaka mafanikio.
Watazamaji.
Aina
ya kwanza ya watu wanaopatikana katika duniani hii ni watazamaji. Tabia za watu
hawa huwa kama ifuatavyo;
Wao
ni waoga katika kujaribu kufanya kitu kipya.
Wao
huamini zaidi katika kushindwa kuliko kufanikiwa.
Wao
ni wazungumzaji wazuri kwa yale ambayo yanatokea katika jamii. Watu hawa huzungumza zaidi masuala ambayo huwa
hayawasaidii mfano wa mambo hayo ni mpira, siasa na matukio mbalimbali
yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mambo ya nje ya mitandao ya
kijamii.
Lakini
kubwa kabisa watu hawa huwa hawana
ubunifu wowote, na huwa wanaishi katika misingi ya kuwaangalia watu wanaopenda
(role model), kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba aina hii ya watu huishi
maishi ya ganda la ndizi, kwa sababu husubiri mtu afanye jambo fulani ili na
wao waanze kufanya.
Wapotezaji.
Kundi
hili lina watu lukuki sana. Na watu ambao wapo katika kundi hili huwa wana
tabia zifuatazo;
Kazi
yao kubwa huwa ni kuwangalia watu wengine wanafanya nini katika maisha yao.
Hata hivyo katika kundi hili, watu wengi huwa wapo kwa ajili ya kuwakosa
wengine kwa yale wayafanyao, na katika kukosoa huko huwa ni katika kukatisha
tamaa zaidi kuliko kujenga.
Watu
ambao wapo katika kundi hili ni wale ambao wameathiriwa kwa kiwango kikubwa
ugonjwa wa wa kuahirisha mambo ya msingi.
Washindi.
Kundi
la tatu la mwisho ni kundi la washindi, kundi hili ndilo lenye watu wachache na
wenye mafanikio. Na kundi hili lina watu wachache kwa sababu watu wengi
wameng’angana’ katika makundi mengine ambayo nimekwisha yaelezea hapo awali.
Watu
ambao ambao wapo katika kundi hili huwa
wanasifa zifutazo;
Wao
hujua ni nini wanachokitaka katika maisha yao.
Wao
hupanga na kukamilisha yale waliyoyapanga kwa wakati.
Lakini
kubwa zaidi watu ambao wapo katika kundi hili huwa si wabinafsi kama walivyo
makundi wangine, wao huwa wapo tayari kuwasaidia wengine.
Pia
ni watu ambao wamewekeza muda mwingi
sana katika kujifunza na kutafakari.
Hayo
ni machache kati ya mengi yaliyopo katika kundi hili.
Hayo
ndiyo makundi matatu yaliyopo katika ulimwengu huu, Mara baada ya kuona makundi
matatu ya watu yanayotufautisha hapa duniani. swali linakuja wewe mwenzangu na
mimi upo kundi gani? Kama unahisi upo kundi ambalo hustahili, unachotakiwa
kufanya ni kuhama mara moja na kuhamia katika kundi lenye mafanufaa kwako.
Asante
kwa kuwa pamoja nasi kila wakati nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson
Chonya.
0757909942,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.