Jun 30, 2017
Wekeza Kwa Shilingi Laki Moja, Upate Zaidi Ya Milioni Moja Na Nusu Ndani Ya Siku 90.
Na Boniface
L. Pwele, Songea.
Leo
nataka tuangalie kilimo cha matikiti kibiashara kwa mtaji wa shilingi laki moja
tu(100,000/=). Nimeona niandae hili somo kwa kuwa watu wengi hulalamika kuhusu
mtaji lakini kwa asilimia kubwa watu humililiki zaidi ya hii pesa laki moja,
lakini bado utamkuta analalamika kuhusu mtaji wa kuanzia.
Leo
tutaangalia mchanganuo wa shilingi laki moja ili ikuletee milioni moja na
nusu(1,500,000/=) kwa makadilio ya chini kabisa hayo ni baada ya siku 75-90 na
unaweza pata zaidi ya hapo, ikiwa utaweka juhudi nyingi katika kilimo ambacho
unaenda kufanya.
Hapa
tutaangalia mchanganuo kwa kutumia mbegu bora ya matikiti aina ya PATO F1. Na
eneo linalohitajika ni chini ya robo ekari (yaani nusu ya robo ekari ) ila
katika laki moja sijaweka gharama ya shamba ambayo ni nusu ya robo ekari yaani mita
500 za mraba.
Maandalizi ya shamba.
Andaa
shamba lenye ukubwa wa mita 500 za mraba( 50m×10m).
Baada
ya kuliandaa shamba lako hakikisha una mbolea ya kuku ya kutosha mashimo 500 tu
na uhakikishe hiyo mbolea imeoza vya kutosha.
Chimba
hayo mashimo 500, chukua mbolea ya kuku ichanganye vizuri na udongo. Kisha piga dawa aina ya Colt kwenye mashimo ikae walau siku 14.
Baada
ya siku ya 14 unaweza panda mbegu zako.
Mbegu
ya PATO F1 50g ambayo unaweza kuipata kwa sh 35,000/= tu inatosha kupanda hilo
eneo la mita 500 za mraba.
Panda
kwa nafasi nzuri, mstari hadi mstari iwe mita mbili na shimo hadi shimo iwe
sentimita 50( yaani mita 2 kwa sm 50)
Panda
mbegu mbili mbili lakini hakikisha huziweki sehemu moja humo shimoni.
Baada
ya kuota mmea ukisha fikisha majani matatu punguza mche mmoja kwa kuukata na
siyo kuung'oa.
Matunzo shambani.
Siku
ya 0-15 (Planting and germinating) mbegu itakuwa tayari isha ota na inakaribia kutambaa.
Mmea
wa matikiti hupendwa sana na wadudu, hivyo mara baada ya kuota ukiwa na majani
angalau matatu tumia dawa ya wadudu aina Prosper
720EC (Profenofos 600g/L + Cypermethrin 120,000/=), ikichanganywa na Agrigrow starter NPK 14:28:18, hii
inafanya mmea kuwa na mizizi imara na kuufanya mmea kuweza kufyonza virutubisho
vizuri kutoka kwenye udongo,ikichanganywa na Agrilax .
Na
hapo uwe na mbolea ya Yara Mila Winner
kilo tano ambayo utaweka gramu tano (kisoda kimoja) kwa kila mche
Siku
ya 16-25( Vegetative/Trailing) hapo
tikiti litaanza kutambaa hakikisha una Agrigrow
vegetative NPK 30:10:10, hii itakuza mmea kwa haraka na kuongeza matawi, dawa
ya wadudu Avirmec.
Siku
ya 25-40 (Flowering) hapo mmea utaanza kutoa maua,hakikisha una mbolea ya Yara Mila Nitrabor ambayo utaweka gram 10
kwa mmea mmoja, dawa ya wadudu Colt, Agrigrow flowering and Fruiting NPK 15:5:35 hii itazalisha maua kwa wingi
na kufanya yasipukutike.
Kuwa
makini kwenye upigaji wa dawa wakati wa kipindi hiki, inakubidi upulizie dawa
asubuhi sana au jioni sana,kwa maana hii hatua ndipo kunakuwa na wadudu wa
muhimu shambani kama nyuki,ambaye ni muhimu sana kwa zao hili la matikiti,ndiyo
maana unashauriwa kama unalima zaidi hata kama ni ekari moja unaweza weka
mzinga wa nyuki shambani kwako ili wasaidie katika uchavushaji.
Siku
41-60-90 (Fruiting) hapo hapo mmea utakuwa umeanza kubeba matunda.
Hatua
hii mmea unatakiwa upate maji ya kutosha lakini inatakiwa upunguze kiasi cha
maji siku kumi kabla ya kuvuna kulifanya tikiti liweze kutengeneza sukari ya
kutosha.
Mavuno.
Kwa
eneo la mita 500 mita za mraba (Yaani mita 50 kwa mita 10) utakuwa na miche
1000 kwenye eneo la mita za mraba 500. Kwa kuwa kila shimo itakuwa ni miche
miwili. Kumbuka nilikuambia zikiota inabidi upunguze mche mmoja mmoja.
Hivyo
katika eneo lako utakuwa na miche 500. Na kwa matunzo mazuri mche mmoja huweza
kufikisha hadi matunda matatu. Ila mimi nakupigia kwa hesabu ya tunda moja kwa
mche.
Na
hilo tunda litakuwa ni kubwa sana kuanzia kilo kumi hadi 15. Kwa matunda 500 na
tunda moja kwa kuwa ni kubwa unaliuza kwa bei ya jumla sh 3000/=Matunda
500×3000= 1,500,000/=(Milioni moja na nusu)
Kama
utayauza mwenyewe reja reja utayauza kwa sh 5000 hadi 7000 hadi 10,000 kwa
tunda moja. Hivyo ukiyauza kwa sh 5000 utaweza kupata 5000×500=2,500,000/=Kumbuka
hiyo ni shilingi laki moja imezalisha pesa hiyo ndani ya miezi mitatu (siku 90).
Sasa
amua kuendelea kutunza pesa benki ambako makato yanaendelea au uwekeze baada ya
miezi mitatu uweze kupata hizo fedha.
Nimeandaa
hili somo kukupa mwanga wewe ambaye unatamani kulima lakini unasema huna mtaji
na wakati una pesa zaidi ya hii niliyo itaja hapo juu.
Lakini
ikumbukwe hyo laki moja sijaweka gharama sijui ya Kukodi hako kakipande ka
shamba,kulima unaweza lima mwenyewe kabisa.
Na
usiseme sina pesa ya kununua mafuta kwa ajiri ya kumwagilia miche mia tano
unaweza chota maji kabisa kwenye ndoo na ukaimwagilia miche yote.
Gharama
ya vitu vyote nilivo vitaja hapo juu
Mbegu
PATO F1 50g 35,000/=
Agrigrow
starter NPK 14:28:18 500g 5000/=
Agrigrow
Vegetative NPK 30:10:10 500g 5000/=
Agrigrow
flowering and fruiting NPK 15:5:35 500g 5000/=
Yara
mila Winner 5kg 10,000/=
Yara
Mila Nitrabor 5kg 10000/=
©Dawa
za wadudu
Prosper
250mls 9,000/=
Colt
250mls 8000/=
Avirmec
50mls 4000/=
Agrilax
500g 9000/=
Mbolea
ya kuku (Omba kwa mtu anayefuga kuku)
Bei
za mbolea hizo za Yara inategemeana na wapi ulipo maana unaweza pata chini ya
hyo bei.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika
kila siku.
Wako mtaalamu wa kilimo, Boniface L
Pwele, bwana shamba nipo kwenye kampuni
ya Agrichem Africa Tz Ltd. Kwa msaada juu ya ushauri kuhusu kilimo tuwasialiane
kwa 0762 567 628 au nitumie e-mail kwenda blugahno95@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.