May 12, 2018
Anza Na Hatua Hii Muhimu Ili Ikusaidie Kufikia Mafanikio Yako.
Kama huwezi kuchukua hatua kubwa za kuelekea kwenye malengo yako uliyojiwekea, basi chukua hatua ndogo tu. Kama unashindwa kuchukua hatua ndogo pia, basi ujue hujaamua kujitoa kuweza kufanikisha malengo yako hayo.
Utakuwa
ni mtu wa kushindwa sana kama huchukui hata hatua ndogo. Unapochukua hatua
ndogo ndogo ukumbuke, hatua hizo ni
muhimu na zinakusogeza sana kukupeleka kwenye malengo yako kila unapozichukua.
Acha
kudharau hatua zozote zile ndogo. Anza kuchukua hatua ndogo kwani zinakuwa ni
mwanzo wa safari ya mafanikio yako na zinaonyesha kweli umejitoa kuhakikisha
ndoto zako zinatimia hata kama upo kwenye changamoto nyingi za kimaisha.
Watu
wenye mafanikio makubwa wengi wao hawakuanza na hatua kubwa za kimafanikio kama
unavyofikiri. Wengi wao walianzia chini sana na mpaka ilifika wakati
walidharauliwa vya kutosha na kutamani kuacha kile wanachokifanya.
Hata
hivyo pamoja na kuanza hivyo hawakukata tamaa, kila siku waliamua kuchukua
hatua hizo na hatua hizo ziliwapa nguvu ya kuendelea kusogea au kuongeza
hatua zingine na hadi kufika mbali kabisa kimafanikio.
Hebu
jiulize sasa kama wewe hutaki kuanza na hatua ndogo ni kipi ambacho unakitaka kwako.
Ukumbuke, ushindi mkubwa wowote unaanza na kidogokidogo tu. Hili si swala la
bahati mbaya bali naweza nikasema ni kama kanuni ya kimafanikio ndivyo ilivyo.
Hata
ukiangalia mimea huwa inaanza kidogo kidogo na mwisho wa siku inakuwa ni miti
mikubwa sana ambayo hata hukuweza kufikiri kama ingekuwa miti ya namna hiyo, hicho
ndicho kitu kinaweza kutokea hata kwako pia.
Pale
ulipo anza na kidogo chochote kile ulichonacho na kidogo hicho uwe na uhakika
kitakusaidia sana katika kutengeneza kikubwa. Jambo la msingi usiwe na hofu,
anza na hapo hapo ulipo na utashangaa jinsi kidogo hicho kinavyoongezeka.
Je, upo tayari sasa kuanza sasa na hatua ndogo hata kama
upo kwenye changamoto nyingi za kimafanikio? Hutakiwi kusitasita, nikwambie tu
anza sasa kuchukua hatua hizo ndogo, wakati utafika utachukua hatua kubwa za
kuweza kukusaidia kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.