May 22, 2018
Hivi Ndivyo Watu Wanavyopenda Kushindwa Kwenye Maisha.
Unaweza
ukaona kama ni kitu cha ajabu au kama nimekosea vile kuandika kichwa cha habari
ya makala haya, lakini elewa sijakosea na ninachokimaanisha ndicho, lipo kundi
kubwa la watu linapenda kushindwa kwenye maisha.
Unashangaa,
ndio, kundi hili kubwa ndilo ambalo likiulizwa, lina mipango mizuri sana ya
kimafanikio, lakini maneno na vitendo vya kutaka maisha hayo haviko sawa. Kundi
hili kubwa ambalo labda na wewe upo, hujikuta likipenda kushindwa kufanikiwa
maishani.
Najua
unajiuliza kivipi? Hebu angalia kuna watu ambao muda wao muda mwingi sana ni kuangalia
Tv, utakuta zaidi ya saa tatu mtu amekaa anaangalia Tv, unategemea hapa nini
kitatokea kama si kuanguka tena vibaya kwenye maisha yake.
Ule
muda mwingi unaopotea kwenye kuangalia Tv, naamini ungetumuka kufanya kitu
kingine kama kutafuta maarifa ya aina fulani hivi, basi mtu huyo angekuwa yupo
mbali sana kimafanikio. Kwa bahati mbaya
muda huo unapotezwa mchana kweupe.
Si
Tv tu peke yake, ukiwaangalia watu wengi wanaishi maisha ambayo hayana maana
kabisa, ni watu wa kuishi maisha ya kuwadanganya na kuwapoteza kabisa kwa
kufanya vitu ambavyo haviwastaili. Ni watu ambao dhahiri wanajidanganya.
Kwa
kawaida unapofanya mambo yanayoenda kinyume
na mafanikio, hata kama unatamka mara ngapi kwamba wewe unataka
mafanikio hayo, hiyo haitaweza kukusaidia kitu. Ndio maana unatakiwa
usijidanganye kwenye maisha yako mwenyewe.
Unatakiwa
utafute vitu vya kufanya ambavyo vinakusaidia kukupa mafanikio. Hata hivyo kwa
bahati mbaya unaishi maisha ambayo kiuhalisia kwa maisha hayo hayakusogezi
mbele hata kidogo kuweza kufanikiwa sana sana yanakurudisha nyuma.
Watu
wengi inaonyesha wanajishughulisha na kazi ndogo ndogo ambazo haziwasaidii
kupiga hatua. Kazi hizo zinaweza zikawa kama kupiga stori, kudhurura na
kufatilia habari zizsizo na maana. Mafanikio hayawezi kuja kwa namna hiyo hata siku
moja.
Waangalie
watu waliofanikiwa, wamefanikiwa kwa sababu ya kuishi na tabia za kimafanikio.
Pia waangalie watu ambao wameshindwa nao pia wameshindwa kwa sababu ya kuishi na tabia zile za kushindwa.
Nimekwambia
hata uimbe wimbo mzuri vipi ambao unajisemea kwamba unataka maisha mazuri, ila
kama unaishi maisha yanayokurudisha nyuma utakwama tu. Hakuna muujiza katika
kukupa mafanikio yako. muujiza ni wewe.
Anza
kubadilika ishi tabia za watu wa mafanikio ili ufanikiwe. Ukiendeleza ubishi
nakwambia utakwama sana. Amua kujifunza, acha kudharau yale ambayo kuna watu
walipoteza muda wao kukusaidia wewe.
Kumbuka
matendo yako ya kila siku ambayo unayetenda kinyume na mafanikio ndio yanayotuonyesha
kwamba wewe unapenda sasa kushindwa. Hata kama hutaki kama unatenda kinyume na mafanikio,
ujue basi unapenda kushindwa kwenye maisha yako.
Ishi
kwa kujiamini, amua kusonga mbele kwa kuhakikisha kila unachokifanya, kiwe na
matokeo ya kukusogeza wewe mbele. Ukiona kitu hicho kikimbie na hakina maana ya
kuweza kukusaidia leo na hata kesho.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.