May 8, 2018
Chanzo Kikubwa Cha Watu Wengi Kushindwa Kwenye Maisha Kinaanzia Hapa.
Kufanikiwa kwenye maisha, kunategemea sana kwanza wewe ujue unaenda wapi kwenye mafanikio yako. Kama hujui ni wapi unakoenda kwenye mafanikio yako ni ngumu sana kuweza kufanikiwa. Ni lazima ujue ni wapi unakoenda ili kupata mafanikio uyatakayo. Je, jiulize unajua kule unakotaka kwenda kimafanikio?
Kama
unafikiri natania, mtafute mtu yeyote ambaye amefanikisha jambo fulani,
ukimwangalia mtu huyo utagundua alikuwa ana mpango au alikuwa anajua kule anakotaka
kwenda kikamilifu. Na pia watu wanaoshindwa, kiukweli wengi hawajui kisawa sawa
malengo na mipango yao kwa kule wanakotaka kufika kimafanikio.
Watu
hawa wanaoshindwa utakuta ni watu ambao wapowapo tu, wanaamka, wanafanya kazi,
lakini ukiwauliza nini malengo yao baada ya miaka mitano kuanzia leo hawajui.
Kwa mwendo kama huo wa maisha ni ngumu kufika mbali kimafanikio, ndio maana mtu
anayejua kule anakoenda ni rahisi sana kuweza kufanikiwa.
Kwa
hiyo mpaka hapo unaona kipimo pekee ambacho hata wewe unaweza kukitumia kujua
kama kwa baadae utaweza kufanikiwa au hautaweza kufanikiwa ni kwa wewe
kujiuliza swali hili mara kwa mara je, ni wapi unapoenda kimafanikio. Kama
hujui unakokwenda kimafanikio na mbele yako unaona kama giza, itakuwa ni ngumu
kufanikiwa.
Unatakiwa
ujue kule uendako kimafanikio kwa uwazi, kwamba pamoja na kwamba mimi nafanya
kitu hiki kidogo ambacho hata watu wengi wananicheka, lakini nataka mwisho
wangu uwe pale, usiishie kuota tu, baada ya hapo chukua hatua hata kama hatua
hizo ni kidogo sana, lakini chukua hatua.
Unapochukua
hatua na huku ukiwa unajua kwenye akili yako ni wapi unakoenda, utajikuta
unasogea na kuvuta fursa zingine ambazo hukutarajia kuzivuta. Kupoteza mwelekeo
wakati unatafuta mafanikio ni jambo la hatari sana kwako. Hutakiwi kupoteza
mwelekeo ila unatakiwa kujua kule unakokwenda kila wakati ili usipotee.
Chanzo
kikubwa cha watu wengi kushindwa kwenye maisha kinaanzia na wengi kutokujua ni
wapi wanakokwenda. Kwa kutokujua wapi unapokwenda unajikuta huna lengo maalumu la
kukusaidia kufanikiwa. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na lengo maalumu katika
maisha unapoanzia.
Kitu
ambacho nataka uelewe hapa ni hiki, ili kufanikiwa tambua kule unakotaka kwenda
kimafanikio. Njia ya mafanikio yako unatakiwa uijue kwa uwazi ni wapi unatakiwa
uwepo pasipo kujali unakutana na changamoto zipi. Kama utashindwa kujua kule
uendako, ujue ndio kushindwa kwako huko kunapoanzia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.