May 18, 2018
Kama Utakuwa Na Kitu Hiki, Kitakufanya Uwe Imara Na Mwenye Mafanikio Ya Kudumu.
Fikiria kama kila kitu unachokihitaji wewe ingekuwa unakipata kila wakati hata pasipo kuweka juhudi kubwa, pasipo changamoto, pasipo kukipigania kitu hicho sana na wala pasipo hata kuweka kazi kubwa yoyote ile inayohitajika, ila kitu hicho unakipata.
Najua kama itatokea hivi, wengi wangefurahi sana na kusema hiyo
itakuwa safi maana mambo yao yatakuwa yamewaendea sawa tena kwa uhakika. Lakini
nikwambie ikitokea hivyo kwako ujue unakwenda kuwa dhaifu sana na mafanikio
yako hayatadumu.
Nimekwambia utakwenda kuwa dhaifu na hautatengeneza mafanikio ya
kudumu nikiwa na maana hii, changomoto yoyote itakayotokea hata kama ni ndogo
kiasi gani hautaweza kukabilina nayo, kwa sababu mafanikio yako uliyapata
kiulaini.
Mafanikio yoyote unayoyapata kwa njia rahisi sana pasipo
kuyapigania uelewe hayana mizizi imara, hayana fundisho, hayana sehemu ambayo
yamekukomaza na ndio maana huwezi kiuhalisia kukua kimafanikio bila kupambana
kikamilifu.
Kama imetokea umepata mafanikio ya moja kwa moja pasipo kupitia
changamoto, unatakiwa kuwa makini sana, la sivyo unaweza kupoteza kila kitu.
Waangalie watu wanaopata bahati nasibu ni kitu gani kinawakuta baadae, wengi
hufilisika tena.
Hiyo yote kama nilivyosema,
inaonyesha huwezi kuwa na mafanikio imara na ya kudumu kama hujakutana
na upinzani au changamoto za kutosha. Kila unapokutana na changamoto hizo hilo
si swala la kuchukia bali ni kujifunza na kusonga mbele.
Maumivu unayokutana nayo wakati huu kwa sababu ya upinzani ama
changamoto, wewe yavumilie kwani ni
rafiki mkubwa sana wa mafanikio yako. Unaweza usione faida yake leo, lakini kesho
utakuja kugundua kile nisemacho na kina ukweli gani.
Tambua kama hujawahi kushindwa, kama hujakosea, kama hujakutana
na upinzani wa kutosha, halafu ukasema unataka mafanikio makubwa unajidanganya.
Hata ukipata mafanikio yataporomoka kwa sababu hakuna kitu kilichokukomaza.
Majasiri na mashujaa
katika maisha ni wale watu wote ambao wamepitia kwenye nyakati ngumu sana ambazo
hata hazieleweki. Nyakati hizi ngumu ndizo ambazo zilizowajenga na kuwapa
jeuri kubwa ya kuweza kufanikiwa.
Watu hawa ukiwaona wana nidhamu na ule uchungu wa maisha. Kuna
kitu ambacho unaona kinachemka ndani mwao yaani wana kiu na hamasa kubwa sana
ya kufanikiwa kwao. Yote hayo yanaletwa na upinzani ama changamoto
walizokutana nazo.
Huhitaji kujilaumu, huhitaji kujuta kila unapokutana na changamoto
kwani hapo ndipo nguvu kubwa ya mafanikio yako ya kudumu ilipo. Changamoto na
upinzani mwingi unakuja kama rafiki wa kukusaidia kukukomaza na kukupa
mafanikio ya kudumu.
Hata watu wengi katika maisha ni watu ambao hawapendi kusikia
sana hadithi za watu ambao walifanikiwa
moja kwa moja kwenye maisha. Hadithi za watu, ambao walifanikiwa moja kwa moja pasipo
kupitia changamoto hazina mvuto.
Kila mtu anapenda sana
kujifunza kwa watu ambao waliumia au watu ambao waliteseka juu ya changamoto
fulani hivi, lakini mwisho wa siku wakaja kufanikiwa. Hivyo elewa, mafanikio ya
moja kwa moja hayakupi nguvu na wala hayakukomazi .
Wewe hapo ulipo una nguvu kuliko unavyofikiri ya kukabiliana na
changamoto yoyote ile. Ukiona umeshindwa wewe umeamua tu. Na changamoto yoyote
unayokabiliana nayo ukiona umeishinda, tambua umepiga hatua fulani kubwa ya
kimaisha.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio kwa undani, karibu
kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO,
kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF
WINNER’S kwenda 0713 048 035,
hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe pia ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.