May 7, 2018
Hatua mbili Za Kufuata Ili Kufanya Kile Unachokiandika Kibaki Na Maana Siku Zote.
Inabidi ufike mahali ukubali
na uamue kwamba kile unachokiandika kiwasaidie wengine na kugusa maisha ya
wengine kwa asilimia kubwa. Haitakuwa
na maana kama una andika tu, halafu kupitia uandishi wako huo hakuna ambacho
kinabadili maisha ya wengine.
Kupitia somo hili, nataka
nikuonyeshe jinsi unavyoweza kuwa mwandishi bora, ikiwa utafuata hatua hizi,
kama nilivyozielezea kwa kifupi . Nategemea kwa kuwa pamoja nami hadi mwisho utajifunza
kitu cha maana.
1. Andika kile ambacho kinagusa maisha
ya watu.
Kama
nilivyosema, unapoandika jambo lolote, hakikisha jambo hilo linagusa maisha ya
watu wengine. Usiandike ilimradi umeamua kuandika, andika ukiwa na uhakika hiki
ambacho unakwenda kukiandika kinakwenda kubadilisha maisha ya mtu fulani na
sehemu fulani.
Nikwambie
hivi labda, kazi zako zitabaki kuwa hazina maana kama utaendelea kuandika vitu,
ilimradi tu umeandika. Gusa maisha ya watu, pengine unajiuliza kile
ninachokiandika nitajua vipi kama kinagusa maisha ya watu?
Ni
rahisi tu, utajua tu kwa kuangalia kwanza wewe kitu hicho kimekugusa au
kimekusaidia kwa kiasi gani, kama hakijakusaidia wewe mwandishi na mwingine
huko hakiwezi kumsaidia pia. Kwa hiyo jitahidi kuandika kile kinachogusa maisha
ya watu.
2. Chagua ni aina gani ya uandishi
unaotaka kuutumia.
Hapa
inabidi uchague aina ya sauti unayotaka kuitumia kufikisha ujumbe wako. Unatakiwa
kutambua tu kila mtu ana namna yake ya kufikisha ujumbe kwa jamii na ndio maana
mwandishi mmoja na mwandishi mwingine wanakuwa wanatafautiana.
Hivyo,
inabidi ujiulize je, unataka kufikisha ujumbe wako kwa kutumia aina gani ya
uandishi. Maana zipo aina tofauti za kufikisha ujumbe wako ama ‘platform’
unayotaka kuitumia kufikisha ujumbe wako. Kwa mfano;-
Uandishi wa kiundishi wa
habari/Journalist, hapa kama wewe si mwandikaji mzuri sana,
unaweza ukatumia aina hii ya uandishi kwa sababu, unaweza ukatumia njia kuwauliza watu maswali na maswali yale
ukayachapa na kuyatumia kuyaweka katika mtandao kama unaendesha blog.
Uandishi wa kinabii/Prophecy, katika
aina hii ya uandishi kama utautumia uandishi huu, kila kitu unachokiongea au
kukiandika ndio kinakuwa ukweli wenyewe. Hapa mwandishi unatakiwa uandike
ukweli mtupu kuhusu maisha ya watu bila kupepesa macho kutokana na uzoefu wako.
Kazi za uandishi wa kuhamasisha mafanikio zipo hapa.
Uandishi wa kisanii/Artist, kazi
au uandishi unaokuwa unawasilishwa kwa njia ya kisanii mara nyingi unakuwa
unatumia mvuto fulani hivi ili ujumbe kufika. Kwa mfano, uandishi wa mashairi
au kuandika kazi kwa kutumia katuni ni mojawapo ya uandishi wa kisanii ambapo kupitia
kuchekesha ujumbe unaifikia jamii.
Uandishi wa kitaaluma/professor, kila
kitu kinachoandikwa katika aina hii ya uandishi kinakuwa kinaonyeshwa chanzo
chake. Uandishi wa namna hii hauendi kama hakuna chanzo cha ulichokiandika
kimetoka wapi. Hapa mwandishi hutakiwi kuwa mazoefu tu, bali unatakiwa uwe umesoma
vitabu vingi sana ili uvifanyie rejea.
Hapa
uamuzi ni wako kuchagua ni aina gani ya uandishi ambao kwako unauona unafaa na
kuamua kuutumia. Hata hivyo ingawa waandishi wengi huwa hawajui ni aina gani ya
uandishi wanaoutumia katika kazi zao, hujikuta tu wakiandika.
Kwa kufuata
hatua hizo uandishi wako utabaki kuwa na maana siku zote na utakuwa na sehemu
ya kubadilisha jamii yako siku hadi siku, pia vizazi na vizazi.
Fanyia
kazi hatua hizo mbili muhimu na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.