May 9, 2018
Hili Ndilo Darasa La Kudumu La Mafanikio Yako Wakati Wote.
Maisha yana kitu cha kukufundisha leo, kitu hicho kinaweza kuwa kizuri kwako au kitu kibaya kwako ambacho hata kinakuumiza lakini kipo kitu cha kukufundisha kwenye maisha yako ambacho unatakiwa ukifanyie kazi.
Kila
mtu unayekutana leo ana kitu cha kukufundisha wewe. Haijalishi mtu huyo amekupa
hasira au amekufanya kitu gani, lakini kipo kitu cha kujifunza kwa mtu ambaye
unakutana naye, pasipo kujali umri wake
au nini alichonacho
Pia kila
hali unayokutana nayo leo kwenye maisha yako, hali hiyo ina kitu muhimu cha
kukufundisha. Hata kama unapitia kwenye hali ngumu au hali nzuri lakini hali
hiyo ina kitu cha kukufundisha na kukufanya uwe imara kimaisha.
Maisha
yatakuwa ya maana kwako sana kama utakubali kujifunza kwa kila unachokutana nacho
kwenye maisha yako. Ukikubali kujifunza utakuwa katika busara na pia itakuwa ni
rahisi kuweza kukabiliana na kila magumu unayokutana nayo.
Wengi
wanaona maisha hayaeleweki au maisha hayana maana, hiyo yote ni kwa sababu ya
kukaza shingo zao na kukataa kujifunza kutokana na maisha yanavyokwenda. Maisha
peke yake yalivyo unatakiwa kujua kwamba ni shule tosha.
Sasa
kama unasubiri mpaka uandikiwe ‘notisi’ ndio uelewe kile ambacho maisha
yanataka kwako, hapo ndipo unapojikuta unajiangusha wewe. Unatakiwa kila hali,
tukio na kila mtu unayekutana naye ukubali kujifunza kupitia yeye.
Kwa hiyo
iwe katika magumu, katika hali za kukatisha tamaa au katika mazuri yoyote
unayokutana nayo maisha yanakupa kitu cha kukufundisha. Hata kama huna kitabu
kupitia mazingira na matukio, kuna kitu unatakiwa ujifunze juu ya maisha yako.
Chagua
kujifunza kitu kila siku katika maisha yako, changua kuisikiliza dunia inasema nini
juu ya wewe. Usiishi tu kwa mazoea kwa kuishi kama vile wewe utakavyo au uwazavyo. Tambua kabisa
kila siku unayokutana nayo ina kitu cha kukufundisha.
Usiwe
miongoni mwa watu ambao wanashindwa kwa sababu ya kugoma kujifunza. Kila siku
ifanye liwe darasa kwako la kujifunza kitu kipya juu ya maisha yako. Ukifanya
hivyo baada ya muda utakuwa mbali sana kwani kila wakati utakua unabadilika na
kukua kimafanikio.
Sehemu
sahihi na darasa sahihi la mafanikio wakati wote ni kwa wewe kuamua kujifunza
kila siku kutokana na chochote unachokutana nacho. Ukiamua kujifunza kweli kuna
kitu vitu vingi utavikipata na utafanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
Je,
jiulize upo tayari kukaa kwenye darasa la mafanikio la kudumu kwenye maisha
yako na ambalo litakupa mafanikio? Kama jibu ni ndiyo endelea kujifunza kila
siku kutokana na kile ambacho unakutana nacho kwenye maisha iwe ni watu,
mazingira au chochote kile.
Hebu leo fanyia
kazi darasa hili la kudumu la mafanikio na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.