May 20, 2018
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maneno Mabaya Yana Mwangwi Mkubwa Kuliko Maneno Mazuri.
Mbali na kanuni za kimafanikio ambazo tumekuwa tukijifunza mara kwa mara, lakini unapaswa kujua kwamba pia maisha ya mafanikio yametawaliwa sana na hekima. Hiyo yote inaonyesha hekima ni za msingi sana katika maisha yetu pia.
Hekima zinatufunza busara,
hekima zinatufunza namna ambavyo tunatakiwa kuishi na jamii inayotuzunguka na
hekima pia zinatusaidia kuweza kujifunza kanuni kwa ujumla za mafanikio
zilizopo kwenye maisha yetu.
Kwa mantiki hiyo, katika siku hii ya leo, nikukaribishe, tuweze kujifunza kwa pamoja baadhi ya hekima za
maisha na mafanikio. Ni kusudio langu utatoka na kitu cha kuweza kukusaidia na ambacho
utakifanyia kazi.
1. Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.
1. Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.
Katika hekima hii
inatuonyesha katika maisha, unaweza ukamfanyia mtu kitu ambacho kitagusa maisha
yake pasipo kujali kitu hicho ni kibaya au kizuri, lakini kumbukumbu inakuwa
inabaki sana kwa yule aliyeguswa na alichofanyiwa.
Ndio maana unaweza
ukamsaidia mtu usikumbuke, unaweza ukamfanyia mtu ubaya usikumbuke, lakini yule
aliyefanyiwa ubaya huo anakuwa anakumbuka sana. Hapa ukumbuke tunaaswa kuwa makini yale yanayogusa maisha ya wengine.
Jiulize ni mara ngapi au kuna
wakati uliwahi kumfanyia mtu kitu fulani ambacho kilimsaidia, utakuta muda
unakuwa umepita na wakati huo umesahau, lakini unapokutana na mtu yule anakukumbusha
na kukwambia unakumbuka ulinifanyia kitu hiki.
Mara nyingi wengi wetu
hubaki tukishangaa kwa kukumbushwa kitu kile. Kwa hiyo unaona hata ubaya
ukimfanyia mtu ni hivyo hivyo. Kwa wewe ukiyefanya ni rahisi kusahau lakini si
kwa ,mtu aliyefanyiwa ubaya huo hata kidogo hawezi sahau.
Hapa ndipo unaweza ukapata
picha kwa nini shoka halikumbuki mti liloukata na kwa nini mti uliokatwa
hulikumbuka shoka. Unaona mti unakumbuka shoka kwa sababu shoka liligusa
maisha ya mti huo kwa namna fulani.
2.
Maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri.
Ni kawaida sana maneno mabaya
kuweza kuenea kwa haraka kuliko maneno mazuri. Unaweza ukafanya mengi mazuri
lakini ukikosea kidogo maneno hayo yatasambaa sana kuliko ambavyo hukutarajia
iwe hivyo.
Hapa kupitia hekima hii inatunaonyesha
wazi kwamba maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri, hilo ni la ukweli na halina ubishi. Mwangwi wa
kitu kibaya unasikika zaidi kuliko mwangwi wa kitu kizuri.
Angalia kipindi ambacho
ulifanya ubaya, mwangwi wake ulisikika vipi na kipindi ambacho ulipofanya mazuri
mwangwi wake ulisikikaje pia. Hapo utagundua kipindi ambacho ulifanya mabaya
mwangwi wake ulionea sana.
Tahadhari kubwa unayopewa
hapa ni kuwa makini sana na maneno mabaya. Kwa tafsiri nyingine inaonyesha tenda
wema unavyoweza wewe ila uelewe maneno mabaya siku yakija kukuibukia yana
mwangi sana kuliko maneno mazuri.
Fanyia kazi hekima hizi
naamini kwa sehemu zitakuwa zimekusaidia kutoka hatua moja na kulekea hatua
nyingine ya maisha yako. Kila wakati hekima zinakupa busara, hekima zinakuza
uelewa wako kwa namna fulani.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.