May 17, 2018
Ili Ufanikiwe, Maisha Hayataki Wewe Uwe Na Kitu Hiki…
Kama una lengo la kujiongezea kipato, acha kuogopa kufanya kitu chochote. Kama kuna kitu fulani ambacho unatakiwa ukiuze, hebu uza kitu hicho. Acha kujisikia vibaya kwa sababu unauza kitu fulani eti ambacho hakina hadhi yako.
Maisha hayataki aibu, fanya kitu chochote cha
kukukiingizia kipato ilimradi kitu hicho kiwe halali na hakiwaumizi wengine.
Maisha ya kuona aibu kufanya jambo fulani yatakufanya uzidi kukosa pesa kila
kukicha.
Acha kuwa na
ndoto za kufanya mambo makubwa saana na halafu ukadharau kufanya hata vidogo
ambavyo huna. Kumbuka, jiwekee ndoto kubwa sana lakini anza na hapo ulipo, anza
na kidogo ulichonacho pasipo kujali ni kitu gani.
Hutaki kufanya kitu kwa sababu ya kuona aibu,
jiandae kufikia ndoto zako hutaweza kufanikiwa. Kwa nini uone aibu kwa kile
ambacho kinakupatia kipato? Shida yako iko wapi na hapo unatakiwa ujiulize.
Ukiona unaona aibu kwa kile unachotaka kukifanya
ujue kabisa hujaamua kujitoa kabisa kuweza kufanikiwa. Huna sababu ya kuendelea
kuona aibu, ni ukweli uliowazi wewe hapo huna kitu, sasa aibu ya nini?
Inawezekana zipo sababu ambazo zinakufanya uone
aibu, sanasana pengine labda umesoma kwa hiyo unaona ukiweka genge mtaani kwako
unakuwa ni mtu kama wa kujizalilisha yaani genge sio hadhi yako.
Naweza nikakubalia sawa, sasa kipi unachoweza
kufanya ambacho ni hadhi yako? hapo ulipo najua unaweza ukawa una tai vizuri
lakini unashindwa kutatua tatizo la shilingi elfu mbili tu, lakini na tai
yako shingoni. Sasa kwa hali hiyo aibu ya nini?
Hapo yaani inaonyesha unashindwa kutatua tatizo dogo
la shilingi elfu mbili na usomi wako. Jiulize tu mwenyewe je, ni akili kweli kuona
aibu kufanya kitu cha faida yako? Kipi bora uendelee kulala au uzunguke mtaani
na kuamua kufanya kitu cha faida.
Nikwambie tu, kwa sasa nyakati zimebadilika sana,
kuendelea kujishaua wakati maisha yanataka uyabadilishe huwezi kufanikiwa. Kama
unaendelea kupaka rangi kwenye maisha yako, nakwambia endelea kupaka rangi, kuna
watu wanajenga ujue na hawapaki rangi.
Mambo hayakusubiri ili yabadilike, ila wewe ndio
unatakiwa kuyabadilisha mambo hayo hatua kwa hatua. Huhitaji kufanya kitu
maalumu sana ili ufanikiwe, anza na kitu chochote tu, ambacho kinakuingizia
kipato bila kujali ni nini, ila kiwe halali.
Acha kusikiliza maneno ya watu, funga masikio na kuamua
kufanya jambo lolote mahali popote na eneo lolote, ilimradi jambo hilo liwe ni
la kukuingizia kipato. Tafakari kwa kina na fanya uamuzi wa busara wa kuacha
kuona aibu zisizo na msingi.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.