May 14, 2018
Usiruhusu Maisha Yako Yatawaliwe Na Mambo Haya Kabisa.
Ikiwa upo kwa ajili ya kutaka maisha ya mafanikio makubwa, yapo mambo ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unapokuwa unaruhusu mambo haya yatawale maisha yako, hiyo inakuwa ni sawa na kuamua kuharibu maisha uliyonayo.
Ni
wajibu na jukumu lako kuyajua mambo haya ambayo tunakwenda kuyajadili na
kuyafanyia kazi. Je, mambo haya ni mambo gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu
yatawale maisha yako? twende pamoja tujifunze;-
Mambo yaliyopita.
Kwenye
maisha yako usifanye kosa ukaruhusu maisha yako ya sasa au yajayo yakatawaliwa
na mambo ambayo yamepita. Mambo ambayo yamepita ni tayari yamepita pasipo
kujali yamekuumiza au hayajakuumiza.
Achana
na kila kitu cha nyuma ambacho tayari kimeshapita, kwani hata ukiendelea
kukibeba sana hakitakusaidia kitu zaidi utaendelea kuumia na kuharibu kesho
yako. iwe kuna makosa ulifanya, ulifanyiwa kitu kibaya na wengine, achana na
hiyo habari.
Kuendelea
kukumbuka mambo ambayo tayari yameshapita hiyo ni sawa na kuendelea kuyapa
nguvu mambo hayo. Kikubwa maisha yako anza kuyatengeneza hapo ulipo na mambo
yaliyopita usiruhusu yatawale maisha yako tena.
Maoni ya watu wengine juu yako.
Jambo
la pili, usiruhusu maisha yako yatawaliwe na maoni ya watu wengine. Watu wanaweza
wakawa na maoni juu ya maisha yako ambayo hayaendani kabisa na malengo yako, kwa
hiyo ikiwa utaamua kuyafata basi utakuwa unajipoteza wewe.
Ndio
maana kabla hujafanya kitu unatakiwa kujiuliza unakifanya kitu kwa sababu yako
au kwa sababu ya maoni ya wengine? Wapo watu ambao hawawezi kufanya kitu mpaka
wasikilize maoni ya wengine wanasema nini.
Umezaliwa
kwa sababu ya makusudi maalumu ambayo unatakiwa uyatimize. Sasa makusudi hayo huwezi kuyatimiza kama maisha
yako unayeendesha kwa kutumia maoni ya watu. Usijaribu kuishi kwa ajili ya
maoni ya wengine sana, utakwama.
Mawazo yako hasi.
Yapo
mawazo ambayo unayo na mawazo hayo yamekuwa yakikuzuai kwa muda mrefu sana
kuweza kufanikiwa. Pengine umekuwa na mawazo ya kusema kwamba siwezi kufanikiwa
kwa sababu hii au ile.
Ukiangalia
mawazo hayo hayana ukweli ila yamekuwa yakikuzuia kufanikwa kwa sababu
unavyojiwazia. Kama unajiwazia kwa ndani huwezi kufanikiwa kwa sababu umezaliwa kwenye ukoo haujiwezi au
kwa sababu huna bahati ni dhahiri hutaweza kufanikiwa.
Kwa
jinsi ilivyo, kama hakuna kinachokuzuia ndani yako kuweza kufanikiwa, basi na
hata nje hakuna kitu ambacho kitaweza kukuzuia kufanikkiwa hata iweje. Uamuzi
unabaki kwako, kutokuruhusu mawazo ya kutokufanikiwa yakutawale, basi.
Mahusiano.
Kati
ya kitu kimojawapo chenye nguvu sana katika maisha ni mahusianao. Ni hatari
sana kujihusisha na mahusiano na mtu yeyote eti kwa sababu huna mtu. Hiyo
nikiwa na maana unaingia kwenye mahusiano kwa sababu furaha pekee unaipata
huko.
Kama
wewe unaona mahusiano ndimo sehemu pekee ya kupata furaha na huwezi kupata
furaha mpaka uwe kwenye mahusiano basi utakuwa kwenye wakati mgumu sana maana
utakuwa unatawaliwa na mahusiano.
Ninachotaka
kusema hapa ni kwamba, unatakiwa uwe imara na kutengeneza furaha yako wewe mwenyewe
bila kujali upo kwenye mahusiano au la. Ni rahisi kuingia kwenye mahusiano mabovu
na kuharibu maisha ikiwa utakuwa na mahusiano ya hovyo.
Pesa.
Tunaposema
usiruhusu pesa itawale maisha yako tukiwa na maana hii, si kwamba pesa ni mbaya
au kwamba hutakiwi kuitafuta, hapana. Hapa kinacholengwa usije ukakubali ukafanya
maamuzi kwa sababu una pesa.
Unachotakiwa
kuelewa ni kwamba usiruhusu pesa, ikawa ndio inatawala maamuzi yako. Fanya
mambo yako si kwa sababu ya pesa. Ifanye pesa ibaki kwako kama kitu cha
kukusaidia na si kwa sababu una pesa kichwa kinaanza kuyumba hovyo hovyo.
Haya
ndio mambo ya msingi ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unaporuhusu
mambo haya yakatawala maisha yako kuna namna ambayo unakuwa una haribu maisha
yako, kuwa makini na fanyia kazi.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.