Apr 27, 2015
Kama Unataka Mafanikio Makubwa, Hakikisha Unabadili Kitu Hiki Haraka Sana.
Habari za leo mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO, nimatumaini yangu ya kuwa umzima na unaendelea vyema katika shughuli nzima ya kuboresha maisha yako. Kama nilivyosema katika makala iliyopita kuwa katika makala ya leo tutajifunza juu ya kubadili fikra zetu ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Ikumbukwe kuwa fikra ni kitu
cha muhimu sana kutuwezesha kufikia mafanikio makubwa tuliyojiwekea. Bila kuwa
na fikra sahihi ni vigumu sana kuweza kufikia mafanikio yoyote yale. Hivyo, hiyo
inatuhakikishia kuwa kama kweli unataka mafanikio makubwa, kitu cha kwanza
unachotakiwa kukibadili kwa haraka ni fikra zako.
Kumbuka,kufikiri ni
kufikiri, wengi ndivyo tunavyamini. Huwa tunachukulia kufikiri kwetu kama jambo
ambalo halituhusu kabisa. Inawezekana kabisa hapo ulipo ulishasahau kwamba huwa
unafikiri hadi hivi sasa unaposoma
kuhusu kufikiri.
Ni ajabu sana kwa sababu, huku
kufikiri ndiko kunakokufanya tuhisi au kutenda kwa namna hii au ile maishani.
Kila tunachofanya na mengi kama siyo yote kati ya yale yanayotutokea kwenye
maisha yetu yanatokana na kufikiri kwetu.
Katika kutafuta kufanikiwa
ni lazima kufikiri kwetu kuwe katika mkabala wa kufanikiwa kwanza. Kama
kufikiri kwetu kuko katika mkabala wa kushindwa, tunakuwa sawa na mtu anayeomba
watu wasukume gari lake kwenda mbele huku akiwa tayari amewaomba wengine
kulisukuma gari hilo kurudi nyuma.
Kama binadamu,
tunatofautiana katika mambo yanayoenda vichwani mwetu na mambo hayo ni mengi
sana. Wataalamu wamethibitisha kwamba, kwa kutwa moja binadamu anapitiwa na
mawazo zaidi ya elfu hamsini. Lakini jambo ambalo hatutofautiani ni ukweli
kwamba, kufikiri kwetu huko kwa namna-kufikiri kuzuri na kufikiri kubaya.
Singependa kuzungumzia
kufikiri vizuri na kufikiri vibaya kwa sababu, inahitaji maelezo mengi na hata
hivyo, haitasaidia sana katika muktadha huu. Bali ninachoweza kusema ni kwamba,
kufikiri vizuri ni ile hali ya kuingiza fikani mwetu yale mambo ambayo
hayatuumizi kihisia, kiroho na kimwili, wala kuwaumiza wengine kwa njia hiyo.
Kufikiri vizuri ni kuingiza
fikirani mwetu yale tu ambayo tunaamini kwamba yatatupa moyo, kutuongezea
matumaini na kutujengea uhusiano mzuri na wengine. Yale tu ambayo ndiyo
tunayotaka , tunayoyatamani na kupenda yatokee maishani mwetu.
Kufikiri vibaya, kwa kifupi
naweza kusema kuwa ni kufanya kinyume na kufikiri vizuri. Pale ambapo kile
tunachokiruhusu kuingia fikrani mwetu ni chenye kutuumiza kihisia, kiroho na
kimwili au kuwaumiza wenzetu kwa njia hiyohiyo, ndipo tunapaswa kujua kwamba,
tunafikiri vibaya. Kufikiri vibaya ni kuingiza mawazoni mwetu yale tusiyoyataka
au kuyatamani ama kuyapenda.
Unachopaswa kufanya kama
kweli unataka mafanikio maishani mwako ni kujiuliza kuhusu mfumo wako wa
kufikiri . je, mawazo yako mara nyingi yanabeba mambo gani?
Inawezekana kabisa huwa
unaamini kwamba wewe ni dhaifu, wewe huwezi kupata cheo, wewe huwezi biashara
fulani kama wengine au wewe ni msindikizaji tu. Kama unajiita ‘mlalahoi’
hujitendei haki. Kama unajiita ‘dhaifu’hujitendei haki. Kama unajiita mnyonge
hujitendei haki. Kama unajiambia una mkosi ndiyo kabisa na kama unajilaumu kila
wakati, tambua kwamba unajifuja kupita kiasi.
Kama unafikiri vibaya
inabidi ubadilike na kuanza kufikiri vizuri, yaani kuingiza fikrani mwako yale
tu ambayo yatakusaidia katika kufika kule unakotaka bila kujiumiza au kuwaumiza
wengine. Kuingiza ffikrani mwako yale tu unayotaka au kuyatamani, na siyo kuingiza yale
usiyoyataka.
Kwamba unaweza kufanya au
kupata kile unachokitaka maishani ni jambo lililowazi kabisa, bila kujali kama
umesoma au hukusoma, un rangi nyeusi au nyeupe, unatoka kwenye familia maskini
au ya kitajiri, unasali au husali. Sifa au vigezo vya kupata kile unachokitaka
vinafahamika, lakini kama nilivyosema sifa ya kwanza ni kufikiri.
Wale wote waliofanikiwa,
ukiwauliza watakwambia kwamba waliamini kuwa watafanikiwa walifanya juhudi
wakijua kuwa iko siku. Kuna wakati rais wa zamani wa marekani Abraham Lincolin(
Alikuwa rais mwaka 1860) ambaye alianguka na kushindwa zaidi ya mara ishirini
katika mambo mbalimbali ikiwemo katika uchaguzi, kufilisika biashara na hadi
kuchaganyikiwa. Lakini aliendelea bila kusema , ‘ninamkosi’ au ‘siwezi’ hadi
akaja kuwa kiongozi maarufu duniani.
Kwenye kitabu chake cha Unlimited power, Anthony Robbins
anamzungumzia mtu ambaye alipata ajali ya barabarani akaumia sana kiasi ch
akuharibika kabisa mwili. Mtu huyu alikuja tena akapata ajali yaa ngege ambapo
alipooza kuanzia kiunoni kwenda chini. Bila kujali ulemevu na uharibifu wa sura
na mwili, mtu huyu alisema, ‘ninawea na nitafanya’. Aliweza na kuwa miongoni
mwa mamilionea wa marekani. Kwa wenzetu wengi, kwa ulemavu wa aina hiyo
hunyoosha miguu na kuanza kuomba wakiamini hawawezi tena.
Anthony Robbins mwenyewe
hakusoma zaidi ya elimu ya kidato cha sita, lakini kwa kuamini kwamba,
inawezekana mtu anapoamua, alifanya maajabu. Kwa kiwango chake hicho cha elimu
aliweza kwa muda mfupi tu, kutoka katika hali ya uhohehahe wa kuishi chumba
kimoja chenye mende, hadi kuaminika katika kuwafundisha watu kuhusu maisha
wakiwemo viongozi wan Nchi.
Sasa hivi Robbins ni
bilionea na hakuiba wala kutumia
ujanjaujanja, bali kanuni za kimaumbile katika kujenga uwezo wa binadamu. Kama
angeamini kuwa, kwa sababu hakusoma sana asingeweza, ni wazi asingeweza, lakini
wa sababu hakujiwekea vizingiti amemudu.
Uwezo wa mawazo yetu
unaonekana vizuri kwa mtu na wazi kwa zaidi kwa mtu aitwaye Stephen Hawking,
ambaye ni miongoni mwa wanasayansi bora ambao karne iliyopita na karne hii zimeweza
kumshuhudia. Kwa nini mtu huyu ni mfano bora wa namna mawazo yalivyo na nguvu?
Akiwa na umri wa miaka 13
aliugua maradhi yanayofahamika kama amyotrophic
lateral screrosis u lo gehrig’s, hali ambayo hulemaza mwili. Hawking alilemaa
mwili mzima isipokuwa shingo, kichwa na mkono wake wa kushoto. Pia alikuwa hana
uwezo wa kuzungumza.
Akiwa kwenye hali hiyo,
aliweza kufanya maajabu kwenye eneo la fizikia na kutoa nadharia nyingi ambazo
zimesaidia kuibadili dunia katika maeneo mbalimbali. Kwa kuamini kwamba
anaweza, kupania na kujua anataka nini, ameshangaza wengi. Kwa sababu bado yu
hai, atashangaza wengi zaidi.
Ukiweza kuyabadili mawazo
yako, yanauwezo wa kukupa mafanikio makubwa ukiamua. Kitu unachotakiwa ni
kuacha kabisa kujidharau na kujishusha, utafanikiwa.
TUPO PAMOJA KATIKA SAFARI YAKO YA
MAFANIKIO,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Apr 25, 2015
Hii Ndiyo Kanuni Rahisi Kwako Unayoweza Kuitumia Kukupa Mafanikio Makubwa.
Ni hivi. Ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa unayotaka iwe katika masomo, kupata kazi, kuvuna sana mazao shambani, kupata faida katika biashara au kuwa na uhusiano mzuri na ndoa nzuri, ni lazima kwanza ujue kwamba hayo yote yanawezekana na yanakuhusu wewe moja kwa moja kwa asilimia zote na siyo bahati.
Unapotaka mafanikio ambayo
huamini kwamba unastahili kuyapata, huwezi kamwe kuyapata hata kama ungefanya
nini. Unapotaka kupata ajira, lakini ukajiambia kwamba kuna watu wengi wenye
sifa kuliko wewe, ambao watapata kazi hiyo na siyo wewe, ni wazi pia hutapata
kazi hiyo unayoitafuta.
Unapoamini kwamba utapata
kazi hiyo kwa juujuu, lakini ndani kabisa mawazoni mwako unajua ni jambo gumu
litakuwa gumu kweli. Unapoingia kwenye biashara kwa kuamini kwamba hutaweza
kufanikiwa kwa sababu haijawahi kutokea ukafanikiwa au kwa sababu wewe una
mtaji mdogo, hufahamiki na pengine hukusoma sana kama wengine, ni wazi
hutafanikiwa.
Unaposema na kuamini kwamba
una mkosi, utaendelea kuwa na mkosi hadi unaingia kaburini. Sisi binadamu ni
kile tunachoamini. Kwa nini inakuwa hivyo, kwamba tunapoamini kuwa hatuwezi au
tuna mkosi, mambo yanakuwa kama tunavyoamini?
Kwa hiyo, ili kuweza kupata
kile unachokihitaji katika maisha na kuenda sawa na kanuni hii ambayo ni rahisi
kwako kuitumia na kukupa mafanikio, ni lazima kuweza kutambua umuhimu wa
kufikiri vizuri. Kwa kufikiri kwetu vizuri itatusaidia kuweza kumudu na kutenda
kwa mkabala wa kimafanikio na kuweza kuvuta mafanikio makubwa kwa upande wetu
zaidi.
Kwa kufikiri kwamba hatuwezi
au hatustahili, bila wenyewe kujua, tutafanya kwa mkabala wa kutoweza na
kutostahili. Kumbuka kuwa upo uhusiano mkubwa sana kati ya fikra zetu, hisia
zetu na tabia au matendo yetu. Tunapofikiri kwamba hatuwezi, bila kujua,
tutakuwa na tabia zitakazotupeleka mahali ambapo hatutaweza kweli.
Mwandishi na mwanafalsafa
maarufu duniani Shakespeare aliwahi kusema: ‘Hakuna jambo baya au zuri, bali kufikiri kwetu ndiko kunakolifanya
jambo kuwa hivyo’. Huu ndiyo ukweli , kwamba, kufikiri vibaya hutudhuru
sana , tuwe tunajua au hatujui. Ubaya au uzuri wa mawazo yetu, hasa yale ya
kina ni kwamba, kile tunachokifikiri na
kukiamini ndicho kinachotokea au kufanyiwa kazi, hayachagui au kutuhurumia ati
kwa sababu hatujui juu ya ukweli huo.
Kwa hiyo, hatua ya awali
kabisa ya mafanikio ya binadamu yako kichwani au mawazoni mwake. Kuna familia,
koo, hata makabila ambayo yamekuwa na fikra kwamba hayawezi au hayastahili. Mtu
kutoka familia, koo au makabila hayo anaweza kuwa na uwezo mkubwa sana katika
kutenda, kipaji na ufahamu mkubwa ajabu, lakini akabaki kuwa mbumbumbu ambaye
familia , ukoo au kabila lake limefanywa kuaminika kwamba ndilo linalostahili
kuweza au kuwa nacho.
Bila kuanza kukagua namna
tunavyofikiri, inaweza kuwa kazi bure kujaribu kutafuta au kuzungumzia
mafanikio kwa ngazi yoyote, iwe mtu binafsi au taifa. Ni lazima tuanze kwa
kujiuliza kile tunachoamini kuhusu mafanikio, yaani kupata kile tukitakacho maishani.
Inawezekana kabisa, bila sisi wenyewe kujua tulishawekewa mipaka ya mafanikio
tangu wakati tukiwa wadogo. Mipaka kama hii huwekwa vipi?
Inawezekana kabisa wazazi au
jamii yote tulimokulia ilikuwa ikisema na kutenda kwa njia ambayo ilituonyesha
kwamba tunachoweza sanasana ni kuhangaika na kupata ajira mahali, basi. Pengine
ilisema na kutenda kwa njia ambayo ilituonyesha kwamba, ni vigumu kwetu
kumiliki gari. Inawezekana kwamba ilisema na kutenda kwa njia ambayo
ilituonyesha kwamba hatupaswi kuinuka sana kimaisha kwani sisi kwa ukoo au
kabila fulani hatustahili.
Pia kuna wakati tunajikuta
tukitamani kusonga mbele katika kutafuta kile tunachokitaka, lakini tunazuiwa
na uvivu wa aina fulani tu tusioujua sababu yake, tunazuiwa na kuahirisha
kufanya hivyo, bila kujua ni kwa nini. Inawezekana kabisa kwamba hiyo inatokana
na malezi, mazingira tulimokulia au uzoefu wetu maishani.
Kumbuka kuwa kuna vizuizi
vingi vilivyowekwa kwenye mawazo yetu katika hatua hizo tulizopitia maishani. Lakini
ili uweze kumudu kuondokana na vizuizi hivyo ni muhimu kwako kujua mambo mawili
tu, ambayo ni kuweza kutumia kanuni
tuliyoongelea ya kuamini kuwa katika maisha yetu tutaweza, tutamudu, tutashinda
na tutatekeleza na jambo la pili ni kubadili mtindo wako mzima wa kufikiri.
Unapoamua kubadili mtindo
wako wa kufikiri sio kwamba tu unakuwa unajiondoa kwenye vizuizi vya
kutofanikiwa, bali pia unakuwa unajiweka katika nafasi nzuri ya kupata kile
unachokihitaji. Je, unawezaje kubadili mfumo wako mzima wa kufikiri na
kukuwezesha kukupatia kile unachohitaji ama kufanikiwa kwa ujumla? Kujua hilo hakikisha
unafuatilia makala ijayo katika DIRA YA MAFANIKIO bila kukosa, ili kujua mawazo
yako jinsi yanavyoweza kufanya kazi na kukupa utajiri.
Ansante sana kwa kuwa msomaji
mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO, endelea kuwashirikisha wengine kujifunza zaidi
kupitia mtandao huu. Kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kabisa kufika mbali
kimafanikio na kuufuta umaskini.
DAIMA TUKO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI
NGWANGWALU,
0713048035,
Apr 24, 2015
Hatua Muhimu Zitakazokuongoza Kufanya Maamuzi Yatakayokupa Mafanikio Makubwa.
Ni kitu ambacho kinawezekana
kabisa katika maisha yako kuwa unaouwezo mkubwa wa kuwa na maisha yenye
mafanikio kama unavyotaka iwe kwako. Ili uweze kufikia mafanikio hayo
unayoyataka kwako ni lazima ujifunze kutumia uwezo mkubwa ulionao kuchunguza
maamuzi unayoyafanya kila siku juu ya maisha yako. Maamuzi unayofanya, ndio
msingi mkuu wa mabadiliko ya maisha yako.
Mara nyingi maamuzi
unayofanya kila siku juu ya maisha yako ndiyo yanayotabiri au kukupa picha kamili
ya maisha yako yanaekea wapi. Kama unafanya maamuzi mabovu kila wakati na kila
mara uwe na uhakika maisha yako ni lazima yatakuwa sio mazuri. Kwa kulijua hilo
ni muhimu sana kwako kuwa makini na maamuzi unayofanya kila siku ili uweze
kuboresha maisha yako zaidi.
Ni kweli kwamba kuna wakati
inaweza ikawa ni ngumu kwako kufanya maamuzi yatakayokupa mafanikio makubwa
katika maisha yako, yote hiyo ni kwa sababu pengine ya kutaka kuona matokeo ya
haraka zaidi. Kama umeamua kuwekeza ni muhimu sana kwako ukawa mvumilivu na
kujipa muda ili kuweza kupata matokeo ya kile unachokitaka. Ukifanya hivyo, ule
ugumu wa maamuzi unaouona hautakuwa shida kwako.
Kwa haraka haraka mpaka hapo
unaona kuwa maamuzi ni kitu cha msingi sana katika maisha yako kuliko
unavyofikiri. Unapokesea kufanya maamuzi
hata kama ni madogo vipi, ndivyo unavyozidi kubomoa maisha yako hata kama
hujui. Hivyo basi, ni muhimu kwako kuwa na maamuzi mazuri na sahihi kila siku
yatakayoweza kubadili maisha yako na kuwa ya mafanikio makubwa.
Unapokuwa na maamuzi haya
sahihi, hii itakusaidia wewe kukuwezesha kustawisha uwezo wako wa kuchagua maisha yanayofaa kila siku.
Katika makala hii ya leo utaweza kujifunza hatua muhimu unazotakiwa kuzichukua
katika maamuzi yako ili kuweza kuishi maisha ya mafanikio. Je, unajua ni hatua
zipi zitakazokuongoza kuchagua kuishi maisha ya mafanikio?
Hizi
Ndizo Hatua Muhimu Zitakazokuongoza Kufanya Maamuzi Yatakayokupa Mafanikio
Makubwa.
1.
Fikiria matokeo ya maamuzi
yako.
Kabla ya kufanya uamuzi wowote
ule katika maisha yako, fikiria kwa makini matokeo ya uamuzi wako huo.
Ukichunguza matokeo ya uamuzi wa unaotaka kuuchukua hiyo itakusaidia kuwa
makini sana na uamuzi wowote unaouchukua kwenye maisha yako. Kwani utakuwa
umejua uamuzi huu unaweza kuboresha ama kubomoa maisha yangu kwa kiasi gani.
Pia kabla hujafanya uamuzi
wowote ule jiulize hivi, uamuzi wangu huu utakuwa na matokeo gani katika maisha
yangu baada ya mwaka mmoja, miaka miwili au hata miaka kumi ijayo. Kama uamuzi
huo unaouchukua utaona unaharibu maisha yako kwa sehemu kubwa, ni bora
ukaachana nao na ukafanya uamuzi tofauti utakao boresha maisha yako.
2.
Chunguza kwa makini maamuzi unayohitaji kufanya.
Ni muhimu sana kuchunguza
maamuzi unayotaka kufanya na sio tu kujifanyia maamuzi ambayo wakati mwingine
hayawezi kukusaidia zaidi ya kukugharimu. Wengi wetu huwa ni watu wa kuiga
maamuzi ya wengine kitu ambacho huweza kuathiri maisha yako moja kwa moja. Ni
muhimu kujichunguza maamuzi unayotaka kuyafanya mara kwa mara.
Kwa mfano kama unataka kuwa
na maisha mazuri ni lazima kwako kujiliza na kujichunguza ni kipi ukifanye ambacho kitaweza kukupa hayo maisha
unayoyatamani. Haitawezekana kwako kufikia maisha hayo kama tu utakuwa bado mtu
wa kuishi maisha yaleyale ya kuendekeza marafiki wa uzembe ama kuendekeza
matumizi ya hovyo. Ukiweza kujichunguza kwanza maamuzi unayoyafanya
yatakusaidia kusonga mbele.
Kwa kumalizia makala hii, tambua
kuwa hizo ndizo hatua muhimu ambazo zinaweza kukuongoza kufanya maamuzi ambayo
yatakupa maisha ya mafanikio kwako na sio tu kujifanyia maamuzi ambayo hayawezi
kukusaidia. Kumbuka kabla hujafanya maamuzi yoyote ni muhimu kufikiria matokeo
ya maamuzi yako na kujichunguza kwa makini maamuzi unayoyataka kufanya
yatakusaidia vipi kuboresha maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO ili kuboresha maisha yetu.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Apr 18, 2015
Siri Kubwa Ya Mafanikio Unayoitafuta Katika Maisha Yako ipo Hapa…
Kuna wakati katika maisha
yako huwa unahitaji kuona ndoto zako zikitimia na kuyafurahia maisha katika
uzuri wake. Kuna wakati pia katika maisha yako huwa unatamani kubadili maisha
yako kwa sehemu kubwa na kufikia hata kuwa huru kifedha. Pia kuna wakati katika
maisha yako huwa unatamani ujue ama utambue siri ya mafanikio kwa ujumla ilipo
ili ufanikiwe kwa viwango vya juu kabisa kama unavyotaka. Hata hivyo, umekuwa
ukishindwa kutokana na kutokujua siri hii.
Kama hiyo kwako ndiyo nia na
shauku yako kubwa ya kutaka kujua siri kubwa ya mafanikio ilipo ili nawe uweze
kufanikiwa kama hao wengine wanaliofanikiwa, hujakosea kusoma makala hii upo
sahihi kwa asilimia zote. Kupitia makala hii utajua na kuelewa kwa uwazi siri
ya mafanikio ilipo ambayo itakufanikisha. Lakini je? Ulishawahi kujiuliza siri
hii ipo kwenye mambo gani? Sitaki uumize kichwa sana, ukweli ni huu, siri kubwa
ya mafanikio ipo kwenye mambo haya kama utayatekeleza:-
1.
Penda kile unachokifanya.
Hautaweza kufanikiwa katika
maisha yako kama utakuwa unafanya mambo ambayo huyapendi katika maisha yako.
Unapofanya jambo ambalo hulipendi kitu kikubwa kinachokutokea kwanza hutaweza
kufanya kazi hiyo kwa moyo wote, utakuwa unafanya ilimradi tu, kama vile
umelazimishwa na mtu. Lakini, si hivyo tu bali hata utendaji wako utakuwa wa
kiholela ambao ndani yake hauna ubunifu wowote ule.
Siri kubwa ya mafanikio ipo
kwenye kufanya kile kitu unachokipenda na si vinginevyo. Asilimia kubwa ya watu
wenye mafanikio makubwa duniani ni watu ambao wanapenda vitu wanavyovifanya.
Kama unataka kubadili hali yako uliyonayo sasa na kufikia mafanikio makubwa,
kitu cha kwanza unachotakiwa kukifanya ni kuchagua kile unachokipenda na
kukifanya kwa moyo wote, utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako.
2.
Anza kwa kidogo.
Kwa kila unachonza kukifanya ni muhimu kwako kuanza
kufanya kwa kidogo. Hii ina maana gani au inaashiria nini kwako? Unapoanza
kufanya kwa kidogo hiyo inakuwa inakupa uzoefu na ukomavu kwa lile jambo ambalo
unalifanya na hii itakusadia zaidi hasa pale unapokumbana na changamoto inakuwa
ni rahisi sana kwako kuweza kupambana nazo na kuzikabili kwa urahisi zaidi.
Kuanza kwa kidogo hii ni moja ya siri kubwa ambayo
inatumiwa na watu wengi wenye mafanikio kuweza kufika mbali.ieleweke kuwa kabla
hujaanza kukimbia marathoni ni vizuri kuanza kukimbia mita chache ili kuweza
kupata uzoefu zaidi. Hivi pia ndivyo ilivyo katika maisha yetu, unataka
kufanikiwa sana na ukawa ambaye hushikiki anza kujenga uzoefu kwa mambo madogo
ambayo utayamudu kwanza kwa vizuri.
3.
Kuwa na nidhamu binafsi.
Pia huu ndio ukweli
usiouweza kuupinga kuwa, mara nyingi siri kubwa ya mafanikio yetu ipo kwenye
sisi wenyewe kuwa na nidhamu binafsi. Bila kuwa na nidhamu binafsi kupata
mafanikio makubwa katika maisha yako, sahau kabisa na kitu ambacho hakitakuja
kuwezekana. Unapokuwa unajiwekea nidhamu binafsi hiyo inakuwa inakujengea nguvu
kubwa ya kukusadia kuweza kusonga mbele zaidi.
Kama umekuwa kwa muda mrefu
ukihangaika na kutafuta siri gani kubwa iliyojificha ambayo inaweza kukusaidia
kuweza kufikia mafanikio makubwa, tambua kuanzia sasa ni nidhamu binafsi. Kama
unafikiri natania anza sasa kujiwekea nidhamu binafsi kwenye mambo yako halafu
utanipa matokeo yake. Kama kweli upo makini na maisha na unataka kufanikiwa kwa
viwango vya juu jifunze juu ya hili, utabadilisha sana maisha yako.
4.
Kuwa mwaminifu.
Mafanikio yoyote
unayoyatafuta yanakutaka ni lazima uwe mwaminifu. Unapokuwa mwaminifu uwe na
uhakika ni lazima utaweza kutimiza chochote kile katika maisha yake hata iweje.
Kwa nini uaminifu ni kitu muhimu sana kwako? Unapokuwa mwaminifu hiyo inakusaidia kukujengea imani na wengine na
kukuza ushirikiano kwa sehemu kubwa katika biashara unayoifanya ama kitu
chochote.
Pasipo kuwa mwaminifu huwezi
kufanikiwa sana katika biashara yako au
tasnia unayoifanya hata iweje. Kila utakapojaribu kutaka kufanikiwa utapata
tabu sana. Na ninapozungumzia uaminifu na maaninisha ni lazima uaminifu uanze kwako wewe na kwa wengine pia. Ni
muhimu kujijengea uaminifu katika maisha yako pia wewe binafsi. Unaposhindwa kuwa
mwaminifu kwako pia na kushindwa
kutimiza ahadi ulizojiwekea hiyo itakupa tabu sana na utashindwa kutimiza
chochote.
5. Kufanya
kazi kwa bidii.
Siri kubwa ya mafanikio ipo pia kwenye kufanya kazi kwa
bidii na kujituma. Hakuna mafanikio makubwa uatakayoweza kuyapata kama wewe
utakuwa sio mtu wa kuweza kufanya kazi zako kwa bidii, kwa maarifa na kujituma
kwa hali ya juu. Ukichunguza kidogo tu, utagundua kuwa watu wengi wenye
mafanikio makubwa duniani ni watu ambao wamejitoa na kufanya kazi kazi kwa
juhudi zao zote bila kuchoka.
Kama unataka kufikia mafanikio makubwa ambayo umekuwa
ukiyahitaji na kuishi maisha yoyote yale ya ndoto zako, hilo linawezekana
lakini litakuja tu kwa kufanya kazi kwa bidii. Unapofanya kazi kwa bidii bila
kukata tamaa mapema na kuwa king’ang’azi wa ndoto zako uwe na uhakika kwa sehemu
kubwa ni lazima mafanikio utayafikia. Hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia
kufanikiwa hata kidogo kama utakuwa mchapa kazi.
Kwa kuhitimisha makala hii, elewa kuwa utafanya kila
unalofanya katika maisha yako, lakini siri kubwa ya kuweza kutimiza ndoto zako
ulizojiwekea ipo katika hayo mambo na hiyo ndiyo siri ya kufikia mafanikio
makubwa unayatafuta katika maisha yako, vinginevyo utasumbuka sana katika maisha
yako kama utakuwa unaishi kinyume na hayo.
Kwa kujifunza zaidi endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA
MAFANIKIO.
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Apr 14, 2015
Ukishajiwekea Malengo, Kinachofuata Ni Hiki Hapa…Ili Kutimiza Malengo Yako Kwa Urahisi.
Ni ukweli uliowazi, mara nyingi ukishajua unataka kwenda wapi katika safari yako ya mafanikio ina maana kwamba kila kitu kwako ni rahisi. Kama unataka kuwa muuza ndizi maarufu, kuwa dereva mkuu, mpiga kiwi mwenye sifa mjini kote, mwanamziki wa kimataifa, ni rahisi kujua ufanye nini kufika huko unakotaka kwenda.
Inakuwa kwako ni rahisi
kuweza kuvumilia shida, kusubiri, kutokata tamaa, kujipa moyo na kuwa na
matumaini yasiyofifia kwa kuwa unajua unachokitafuta . Unaweza kuuingiza mtaani
ndizi zisinunuliwe hata moja, lakini kwa kuwa unajua unachokitafuta, yaani kuwa
muuza ndizi maarufu baadaye, kikwazo hicho kimoja hakitakuvunja nguvu. Kwanini?
Kwa sababu hapa utakuwa unaangalia picha kubwa, badala ya kapicha kadogo.
Hii ya kuangalia picha kubwa
badala ya ndogo, pia ndiyo siri kubwa ya mafanikio mengine maishani. Kuangalia picha
kubwa badala ya ndogo ina maana kwamba, unapoingia kwenye matatizo au changamoto,
itakusaidia kukabiliana na changamoto hizo kwa urahisi. Kama umeanzisha
mgahawa, lakini lengo lake ni kuja kuwa na hotel kubwa ya hadhi, unapopata
matatizo, chukulia hayo ni mafunzo unayoyapata kuelekea kwenye hilo jambo kubwa
unalolitaka.
Kila unapokuwa unafikiri
kuwa kuna jambo kubwa sana ambalo ni lazima uweze kulitimiza na ndilo lengo
lako kuu, hutaweza kukatishwa tamaa na matatizo katika hiki kidogo unachoanza
nacho. Hata kama utafungua biashara fulani kwa muda, halafu ukaja kuifunguka
kutokana na matatizo au changamoto hizo, lililo muhimu kwako ni kujifunza kwa
changamoto hizo na kuanza upya mpaka kufikia lengo ulilojiwekea.
Mtu anayejua anaelekea wapi
kwenye safari yake haamui kuvunja safari hiyo kwa sababu basi limeharibika. Atasubiri
mpaka litengenezwe ili aendelee na safari. Lakini kama hajui hasa anaelekea
wapi, lakini yumo kwenye basi liloharibika, likipita lori kuelekea kule
alikotokea, anaweza kulidandia, kwani anachotaka yeye ni kuonekana tu yuko
safarini, bila kujali anaelekea wapi hasa.
Kwa kawaida tukishachagua
tunataka kuwa nani au kufanya nini, tutajiuliza namna tutakavyoanza kuelekea
huko. Kwa bahati mbaya, wengi wetu tunataka tunapoamua leo, basi asubuhi
inayofuata tuwe tumeshakamilisha kila kitu au kufanikiwa. Kama tumeamua
kumiliki duka au kufanya biashara ya mazao au kuja kuwa madaktari, ni lazima
tujiulize kama tuna chochote cha kutusaidia kuanza safari ya kuelekea huko. Ukishajua
una chochote au tayari umejiwekea
malengo kinachofuata kwako ili kutimiza malengo hayo ni:-
1.
Kwanza, ni lazima uwe na elimu na
maarifa.
Kuna malengo fulani yanahitaji
tuwe na elimu fulani, mengine yanahitaji tuwe na uzoefu fulani na mengine
yanahitaji muda kwani yana hatua kadhaa ambazo ni lazima tuzipitie kwanza. Kama
mtu anapenda sana na ameamua kuwa mpambaji wa maharusi na mpishi wa keki za
harusi, itabidi asomee utaalamu huo.
Kwa mfano kama mtu atakuwa
ameamua kwamba, atakuwa anasafirisha vyakula kutoka mikoani na kuvipeleka
jijini Dar es salaam, ni lazima ajue vyakula gani na vinatokea maeneo gani ya
nchi, vinasafirishwa vipi na msimu upi ambao unafaa kupelekwa jijini Dar es salaam
na sababu gani? Kama ni mwanafunzi anataka kuja kuwa mwandishi wa habari, ni lazima
tangu awali ajue ni masomo gani anatakiwa kuyazingatia.
Elimu na maarifa siyo lazima
viwe vitu vya darasani kama unavyoweza kufikiri. Kama tumegundua jambo au mambo
ambayo tunataka kuyafanya maishani, ufahamu kuhusu jambo au mambo hayo ni muhimu
sana kwako. Ufahamu huu huweza kupatikana kwa njia mbalimbali na kwa kawaida
upo, ni juu yetu kuutafuta.
2.
Pili, ni lazima uwe na ushirikiano na wengine.
Kuna shughuli nyingine
inabidi tuwe na watu ambao tayari wamo humo kutuelekeza. Inawezekana kabisa
tunataka kuwa wafanyabiashara, inabidi muda mwingi kutafuta ushirikiano na
wafanyabiashara ili kuweza kutuonyesha mwanga wa kile ambacho tunataka
kukifanya.
Ni jambo la kushangaza
kugundua kwamba mtu ana kipaji fulani, ana ujuzi fulani ana maarifa fulani,
lakini hana uwezo kuonyesha na pengine kuyatumia kwa faida kutokana na ukosefu
wa rasilimali. Wakati huohuo inawezekana kwamba kuna watu wenye raslimali ambao
wanatafuta mtu au watu wa kipaji chake, lakini hawawaoni.
Kama unataka kufika mbali ni
lazima tukubali kushirikiana na wengine kwa njia moja au nyingine. Tukiwa wachoyo
kamwe hatutamudu. Wakati mwingine siyo uchoyo, bali hatujui kwamba vipaji,
maarifa na uwezo tulionao tunaweza kutafuta watu wa kushirikiana nao na kwa
pamoja tukamudu. Tunakaa na kusubiri hao wengine watubaini ili watutembelee
katika kufanya nao mambo fulani. Ni sisi ndiyo tunaotakiwa kuwatafuta wengine
ili tufanye nao.
Hakikisha unaendelea
kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa maarifa na elimu bora itakayoboresha maisha
yako.
TUNAKUTAKIA USHINDI KATIKA
SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo.
Je, huwa unaingia kwenye
msongo wa mawazo haraka au kirahisi? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini usijiulize ni
kwa vipi unaingia kwenye kusongeka? Kitu ninachoamini kwa kujiuliza ni kwa nini
mtu anasongeka, kunakuwa kuna mengi ya kujifunza, lakini wakati mwingine, mengi
ya kushangaza pia.
Kusongeka humfanya mtu kuona
kwamba, kila kitu kinakwenda hovyo, kila kitu kiko shaghalaghabala, kila kitu
kiko hovyo. Wanaoingia kwenye kusongeka kiakili hujiambia siku zote kwamba,
kila kitu hakina maana, yakiwemo maisha yao pia.
Je, kitu cha kujiuliza hapa
kama itatokea nikaingia kwenye kusongeka kiakili nitakuwa nazungumza vipi,
yaani kwa sauti namna gani? Bila shaka nitakuwa nazungumza kwa sauti ya chini
na pia ya kuburuza. Siyo kuzungumza tu, bali hata kusimama au kutembea kwangu
kutakuwa ni kwa kujiinamia na kuona kila kitu kwangu kimeharibika.
Hivi ndivyo wengi
wanavyojiona wanapokuwa wamesongeka kimawazo, ingawa kuna wakati mwingine
huweza hata kuonyesha nyuso za huzuni na simanzi, hiyo yote huweza kutusaidia
sisi kubaini na kutambua wazi kinachoendelea kwenye akili zao kuwa wana mawazo
mengi au kusongeka sana ndiko kunakowasumbua.
Kama upo kwenye kusongeka na unaendeleza mawazo hayohayo kila mara ambayo yanakupekea wewe kusongeka hiyo inakuwa sawa na wewe kuamua kujichanganya kwenye maisha yako. Na unapoamua kujichanganya mwenyewe kwenye maisha yako, tambua kabisa hakuna utakachoweza kufanikisha, zaidi ya kuharibu maisha yako tu.
Ni vizuri kwako kujua kuwa
unaouwezo wa kuweza kubadili kusongeka kwako kimawazo na kuishi huru kabisa.
Najua inaweza ikawa kwako sio rahisi kuelewa, lakini ninachotaka kukwambia kuwa
unaweza kuondokana na kusongeka kwako, ikiwa tu utaweza kubadili namna ya
kuyatazama mambo au matukio katika maisha yako.
Ni kweli kwamba, kusongeka
kiakili husababishwa na mambo mbalimbali, lakini sisi huweza kufanya kusongeka
huko kushika mizizi kwa namna tunavyokaa, kusimama au hata kwa namna yetu
tunavyofikiri na kutafsiri mambo. Tunapokaa au kufikiri kwa namna ya kinyonge,
tunafanya mawazo yanayotupitia kuwa ya kinyonge pia.
Kwa kuhakikisha hili zaidi,
hebu jaribu kumuuliza au kumchunguza mtu anayetembea huku akiwa ameinama na Yule
anayejiinamia kama atakwambia kuwa anafikiria mambo mazuri. Ni wazi kabisa mtu
kama huyu ni lazima atakuwa anafikiria mambo mabaya yanayopelekea kusongeka
kwake kimawazo.
Kufikiri kwetu kukiwa nako
ni kule kunakotutia hofu, mashaka na kutuingiza kwenye kijicho, ni lazima
tutajikuta tukianza kusimama au kutembea kwa njia yenye kuonesha kukata tamaa,
wanyonge na hata tusiojiweza. Kwa nini tusibadili mambo hayo ili tuweze
kuondoka kwenye huzuni kali au kusongeka? Kwa kujiambia mambo yenye kutia
huzuni na simanzi tunajiingiza kwenye huzuni bila kujua.
Lakini kumbuka kuwa kwa
kujiambia mambo mazuri na yenye kutia moyo ndivyo tunajikuta ambavyo tunaingia
mahali ambapo tunayaona au kuyatazama maisha katika mwanga mkubwa zaidi. Na
hivi ndivyo tunavyoweza kuondokana na msongo wa mawazo kwa kujiambia mambo mazuri
kila mara katika maisha yetu na si vinginevyo.
Kwa kuwa tunaweza kufikiri
kwa namna isiyoumiza, tunaweza kwa hali hiyo kujitoa kwenye kusongeka. Kuna wakati
mtu mwenye msongo wa mawazo anahitaji tabasamu tu au kujiambia kimoyomoyo
kwamba, kila kitu kiko sahihi na kinakwenda kama kilivyotarajiwa. Halafu, ni
kweli, ataanza kuhisi tofauti, kuhisi ukamilifu na uwezo zaidi katika maisha
yake na kuondokana na kusongeka ambako kunaweza kuwa kunamtesa.
Ninaomba nikutakie mafanikio
mema, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA DEVOTA KAUKI WA MANYONI, SINGIDA.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA DEVOTA KAUKI WA MANYONI, SINGIDA.
Kama una maoni au ushauri
unaweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa email truesuccess89@gmail.com
Apr 2, 2015
Hivi Ndivyo Nguvu Ya Mawazo Yako Inavyoweza kukuepusha Na Matatizo.
Umewahi kupata hisia ama mawazo fulani kuhusu jambo fulani, lakini usijue hisia hizo zina maana gani na wala zinatokana na nini? Basi hisia hizo ndiyo hasa nguvu ya ufahamu wako au ‘intuition’, kama wataalamu wanavyoita. Nguvu za ufahamu ni nini? Fikiria ufahamu kama mshauri wako aliye karibu nawe akitaka kukusaidia na kukuongoza katika kila jambo.
Tatizo kubwa la mshirika
wako huyu ni kwamba huwa hazungumzi lugha uliyoizoea wewe. Hii ni kwamba si
wakati wote mshirika huyu hutoa kauli na kutoa maelekezo katika lugha uliyoizoea
kuisikia na kuielewa kirahisi. Ili kuweza kukuza nguvu za ufahamu wako,
unawajibika kuielewa lugha yake na huu ndio mtihani mkubwa katika hilo.
Unaweza vipi kujua namna
ufahamu ufanyavyo kazi, au jinsi ya kuilewa lugha yake? Ufahamu unatumia ujumbe
katika miundo tofauti wakati wote, kila siku. Wakati mwingine ufahamu huenda
ukawa ni hisia hiyo niliyoilezea hapo mwanzo, yaani wakati unajua jambo fulani,
lakini huna njia ya kufafanua kile unachofahamu.
Kwa mfano, unaweza ukawa uko
barabarani unaendesha gari, na mara gari lingine likakupita kwa kasi. Gari hilo
baadaye linapunguza mwendo na kuonekana kukuziba usiendelee vema na safari
yako. Unaamua kulipita, lakini unasita ghafla na kuamua kuliacha liendelee kuwa
mbele yako, ingawa unaliona kama linakuchelewesha na safari yako uliyonayo.
Muda mfupi baadaye,
unalishuhudia gari hilo lililo mbele yako, likigonga gari lilolo mbele yake kwa
kushindwa kusimama wakati lilipolikaribia. Unawaza akilini kwamba , kama
ungeamua kulipita gari lile, bila shaka wewe ndiye ungekuwa umegongwa saa hizi.
Hii yote inadhihirisha uwezo au nguvu kubwa ya ufahamu jinsi inavyoweza kufanya
kazi kwako.
Mfano mwingine, tuchukulie
unatembea kandokando ya barabara ukiwa unazungumza na mtu. Mazungumzo yenu
yanakuwa ni ya wewe kuomba kitu Fulani kwake na kusisitiza. Ghafla mtu unayezungumza
naye anabadilika na kuonekana kukasirika. Anaamua kukuacha na kuongeza mwendo.
Ukiwa katika hali ya
kushangaa kwanini amekuacha kuna wazo linakujia kuwa umfuate ili uendelee
kuzungumza naye, lakini ghafla wazo linakujia usifanye hivyo bila kukupa
sababu, ni kwa nini usifanye hivyo. Mita chache baadaye, gari linalokuja kwa
kasi linaacha njia na kumgonga Yule jamaa yako uliyekuwa ukizungumza naye aliye
mbele yako.
Si hivyo tu, kuna wakati
unaweza ukajikuta unataka kusafiri. Mipango ya safari unakuwa umeiweka sawa,
kinachokuwa kimebakiwa ni wewe tu kuondoka. Lakini, kitu cha kushangaza unaanza
kujihisi mzito, unajivuta mpaka lile gari linakuacha. Muda mfupi tokea uachwe
na gari lile unakuja kupigiwa simu kuwa gari lile limepata ajali mbaya sana.
Akili mwako sasa unaanza
kujiuliza nini kingetokea kama ningepanda lile gari. Bila shaka utaanza kuwaza
ni lazima pengine ningekuwa nimepoteza maisha. Lakini ni nini kilichokuokoa
basi hadi ukashindwa kupanda lile gari bila kujijua, wewe mwenyewe unashangaa
na unashindwa kupata majibu hasa yaliyokamili kwako.
Pamoja na kuwa unaweza ukawa
hujui kitu kinachokuokoa, lakini ni ukweli kwamba kinachokusaidia ama kukuokoa
ni nguvu zako za ufahamu ulizonazo. Nguvu hizi za ufahamu kuna wakati zinaweza
kuokoa maisha yako ikiwa utasikiliza kile zinachosema. Watu wengi wamewahi
kuokolewa na nguvu za ufahamu wao bila kujijua.
Kuna wakati katika maisha
yako kabla ya jambo baya halijaweza kukutokea, nywele za nyuma ya kichwa huwa
kama unahisi zinasimama. Hii yote ufahamu wako huwa unataka kukuonyesha kuwa
mbele kuna hatari. Ikiwa unataka kuvuka
barabara kwa mfano, basi ujue zinakuonya usivuke, kama unataka kwenda mahali
basi ujue zinakuonya usifanye hivyo.
Nguvu hizi za ufahamu
pia huweza kukuokoa pale ulipotaka
kwenda mahali na kusita ghafla, halafu huko ambako ungeenda kukatokea ajali ama
mtu kupoteza maisha. Hivyo, huwezi kulijua hilo kwa sababu hukwenda huko,
lakini kikubwa kinachokuwa kimekuokoa ni uwezo wa nguvu zako hizi. Ni nguvu
hizi za ufahamu ambazo hufanya kazi kwa njia ambayo ni ya kushangaza kidogo.
Ufahamu huu huja kwa sura
tofauti. Fikiria ufahamu kama mshirika wako, kuna wakati mshirika huyu
atazungumza na wewe kwa hisia tu, kuna wakati atazungumza kwa maneno kupitia
mtu mwingine, kuna wakati atakupa ishara, kuna wakati atajaribu kukuzuia
kufanya jambo fulani ambalo sio zuri kwako. Uko umuhimu wa kujua namna
anavyoweza kuzungumza na wewe.
Kwa mfano, kama nguvu hizi
za hisia zitazungumza nawe kupitia hisia, zinaweza kuwa hisia nzito zinazokutaka ufanye kitu fulani ama uache
kitu na kufanya kile kwa nguvu zako zote.
Kuna wakati nguvu za ufahamu
zaweza kuzungumza nawe kupitia mtu mwingine. Kwa mfano, unaweza kuwa unafikiria
kununua nyumba mpya, lakini huna uhakika ununue eneo gani. Mtu wa kwanza
unayezungumza naye anakutajia eneo fulani.
Mtu wa pili unayejaribu
kuzungumza naye anakutajia eneo hilohilo, wa tatu naye anakutajia eneo
hilohilo. Unatazama kwenye gazeti na kukuta makala inayolisifia eneo hilo
ambalo marafiki zako walikutajia kuwa ni eneo bora na linalokufaa kwa kuishi.
Hadi hapa, ni wazi nguvu za ufahamu wako zitakusaidia kulifikiria eneo hilo na
huenda sasa ukaamua kwenda kuliona.
Kuna wakati nguvu za ufahamu
wako zitakuongoza kwa kukupa ishara. Zitakuongoza kwa kukupa ishara kwa kuona
kitu kinachofanana na kile unachokitafuta. Kwa kuona kitu ambacho kipo sawa na
kile unachokitafutia jibu hiyo moja kwa moja ni ishara tosha kwako.
Kuna wakati nguvu za ufahamu
wako zitajaribu kukuzuia kuchukua hatua fulani. Huenda unataka kununua nyumba
kwenye eneo fulani, lakini unagundua kwamba si ya hadhi unayotaka ama ni ya bei
ya juu sana. Hii ni ishara ya kutaka utafute eneo jingine, ama kuwa na subira
mpaka utakapopata nyumba kwenye eneo sahihi, ama kufikiria eneo lingine.
Huenda unataka kazi mahali fulani,
lakini unakuta hakuna mwelekeo hata wa namna ya kuifatilia kazi hiyo ama wapi
pa kuanzia. Hapa huenda nguvu za ufahamu zinakuelekeza utafute kwingine na
kutokuendelea kuifatilia kazi hiyo tena uliyoelekeza mawazo yako. Katika
matukio yote, ujumbe sio utakuwa wazi kama unavyotaka uwe.
Namna nguvu za ufahamu
zinavyozungumza nasi, si siku zote unaeleweka kiurahisi. Lakini ikiwa
utaendelea kuupima na kuendelea kutafuta jibu, jibu litakuwa wazi. Hisia
zitakuwa nzito. Ishara zitaendelea kurudiwa na kuwa wazi. Ujumbe kutoka kwa
watu wengine utarudiwa tena na tena na hatimaye ujumbe utakuwa wazi.
Kuna wakati huenda usielewe
ujumbe mpaka miaka kadhaa baadaye. Lakini kuna siku utaonesha maana
itakayoonekana katika wakati mwafaka utakapotimia. Kwa kifupi hivyo ndivyo,
nguvu ya ufahamu inavyofanya kazi kwako na kukuongoza katika mambo mengi ambayo
kuna wakati hata wewe hujui.
Nakutakia mafanikio mema katika
safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
IMANI
NGWANGWALU,
- 0713 048 035,
- dirayamafanikio@gmail.com.
Apr 1, 2015
Hawa Ndio Watu 5 Hatari Wanaoweza kuharibu Maisha Yako.
Ni ukweli na imedhibitishwa katika taaluma mbalimbali ikiwemo ya malezi na dini zetu, kwamba huwa tunaambukizwa tabia nzuri au mbaya na wale watu ambao kwa muda mrefu tuko nao na tunawaamini kwa kiasi fulani. Watu hao wanaweza kuwa wazazi, marafiki, wafanyakazi wenzetu, wanafunzi wenzetu, jirani zetu na wengine.
Nimeona siyo vibaya kwa hali
hiyo, kukushauri kwamba, unapaswa kuwa makini sana na watu ambao kwa namna moja
ama nyingine wanaweza kuharibu maisha yako kwa sehemu kubwa hata kama
tunawapenda vipi. Hili si jambo la mzaha
kama unavyoweza kulitazama kijuu-juu. Ni jambo la dhati. Kwa haraka haraka
naomba nikutajie watu hawa, wanaoweza kuharibu maisha yako.
1.
Watu wanaofikiri, kusema na kutenda hasi.
Hawa ni watu ambao siku zote
huwa hawaoni suluhu ya jambo, bali kuona matatizo tu. Ni watu ambao huzingatia
zaidi mambo yasiyopendeza na siyo yale yanayopendeza. Mtu anaweza kufanikiwa
kupata zabuni ya shilingi milioni 20 na kukosa ile ya milioni 100. Badala ya
kushukuru na kuangalia ile zabuni aliyoipata, atazingatia na kuumizwa kichwa na
kile alichokikosa.
Hawa huwa ni watu ambao hata
wakifanikiwa kivipi kimapato,bado maisha yao yanakuwa yamezingwa na hofu
zisizoisha, kutoridhika na kutamani tena na tena bila ukomo. Kwao kushindwa
kupata wakitakacho, bila kujali ni kitu gani, ndilo jambo linalopewa uzito
badala ya kile walichokipata.
Lakini kwa bahati mbaya,
watu wa aina hii huwa ni vigumu pia kufanikiwa kimapato katika Nyanja
waitakayo. Ni kwa sababu, kwao matatizo madogo kuyaongeza chumvi nyingi na
kuonekana kuwa makubwa sana. Kwao kushindwa jambo wanakutazama kama msiba
mkubwa ajabu. Hukata tamaa haraka kwenye matatizo na hivyo hawapati nafasi ya
kujifunza kupitia katika matatizo yao.
Ukiwa karibu na watu wa
namna hii, ni wazi utadhani maisha ni tahadhari na mashindano ambayo mshindwa
hapaswi kuishi. Lakini hata kama nawe uko hivyo, inabidi ujue kwamba, una
safari ndefu kuelekea kwenye mafanikio kama kweli unayataka. Watu wa aina hii
wana nguvu hasi za kuweza kuambukiza maradhi yao kirahisi kwa wengine.
2.
Watu ambao ni wafujaji wa mali.
Bila shaka umewahi kusikia
watu wakisema ‘ponda mali kufa kwaja’. Sina uhakika watu wanaoamini katika
usemi huu wana maana gani? Inawezekana ukawa na ukweli kama mtu anaamini kwamba
yeye ni huo mwili wake na maisha yake huisha pale mwili wake unapoachana na
mawazo au roho yake. Lakini hata kama mtu anaamini hivyo, bado kuna swali la
msingi kwamba, maisha ni yeye peke yake?
Kuna wengine wanaoamini
hivyo ambao wamesomeshwa kwa fedha za mifuko ambayo waanzilishi wake
walishakufa zamani. Ni watu waliohangaika kutafuta, wakapata na kuweka ili
wateja waje wawasaidie wengine. Sasa unashindwa kujua inakuaje mtu huyu
anayeamini katika kuponda mali kufa kwaja asijiulize mchango wake kwa wengine
ambao atawaachia nyuma.
Hatukuletwa duniani ili kula
na kuvaa vizuri na kufanya mapenzi sana, halafu tufe. Tuliletwa kwa kusudi
maalumu na kusudi hilo kwa sehemu kubwa ni mchango wetu kwetu na kwa wengine
hapa duniani. Elewa tu, unapaswa kuwaepuka watu ambao hawaamini kwamba
wanapaswa kuweka akiba ili kufanya mambo ambayo yatawasaidia wengine baadaye.
Wengine wao wanaweza kuwa ni familia zao, ndugu au jamaa zao, ama jamii nzima
kwa ujumla. Bila shaka huko ndiko kufanikiwa kwa juu kabisa, tunapokuzungumzia
kufanikiwa kwa upana wake.
3.
Watu wasiojua cha kufanya baadaye.
Kuna watu ambao ukweli ni
kwamba hawajui cha kufanya muda ujao. Watu hawa hula chakula tu, kunywa pombe
tu, kucheza bao au karata tu, lakini wafanye jambo gani la kuwasaidia wao au
wengine inawawia vigumu. Ni afadhali mtu ambaye hana malengo lakini kuna jambo
au mambo anafanya, hawa hawana wanachofanya kabisa.
Kazi yao ni kutafuta mtu wa
kumlaumu kwa kushindwa kwao kuwajibika. Hata wakipewa shughuli, watashindwa na
kurejea kwenye kuishi kama mawe au kuku wa kufugwa bandani. Wanajua sana watu
hawa kusingizia serikali au viongozi wa nchi. ‘wanaiba sana, ndiyo maana
wengine hatuna cha kufanya’. Ni hodari sana kulaumu ndugu, ama jamaa zao.
Hawa ni watu ambao kwa
kawaida ukiwaendekeza wanakufikisha mahali ambapo unaweza kuamini kwamba maisha
yana kasoro na wanaweza kukufanya uamini kwamba hata wewe hutendi mema kufanya
shughuli na kuingiza kipato kingi. Dawa ni kuwakwepa kwa mbali na wala
usikubali ‘kuwafuga’, watakuharibia sana maisha yako.
4.
Watu wanaoharibu majina ya wengine.
Siyo rahisi kwa mtu
kufanikiwa kama ana kijicho, dhidi ya watu waliofanikiwa. Kuna watu ambao ni
maadui wa watu wote wanaofanya vizuri. Hutumia kila wanaloweza kuwaharibu ama
kuwazuia ili wasiende mbali. Wanaweza kukuza majungu au sifa mbaya kwa watu
ambao wanaonyesha kuelekea kwenye mafanikio au hata kufanya njama tu ili
waanguke. Badala ya kuwa karibu na hao wanaoelekea kwenye mafanikio ili
wajifunze kitu, hutaka kuwaona wameanguka, hivyo muda wao mwingi huupoteza
katika kutafuta na kumharibia yule au huyu na sio katika kutafuta mafanikio.
Kufuatana au kuwa karibu na
watu hawa ni sawa na kutaka kuambukizwa bure nguvu hizi hasi ambazo zinadhuru
sana bila mhusika kujua. Kwa nini tusijaribu kuiga na kujifunza kupitia
mafanikio ya wengine katika kutafuta mafanikio yetu, badala ya kuwachukia? Kwa
nini tusiamini kwamba wengine wakifanikiwa, nasi bila kujua tumefanikiwa pia?
Kama kweli tunataka mafanikio ni lazima tuwaepuke watu hawa wenye kijicho na
chuki.
5.
Watu wasipenda shida wala usumbufu.
Hawa huwa ni watu ambao
idadi yao inazidi kuwa kubwa kila kuchao. Ni watu ambao mara nyingi wakishasoma
basi kila kitu huishia hapo na hutamani ama hupenda zaidi kila kitu kiletwe
miguuni mwao. Ni watu ambao hawana juhudi wala ubunifu kwa kile wanachokifanya
katika maisha yao. Watu hawa huwa ni watu wa jua kucha, jua kuzama siyo zaidi
ya hapo. Matokeo yake ni kupata shida katika maisha. Pia hawa ni watu hatari
sana kwako unaotakiwa kuwaepuka sana.
Hao ndio watu hatari ambao
usipokuwa nao makini wanaweza kuharibu maisha yako kwa sehemu kubwa sana.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza
kila siku.
IMANI
NGWANGWALU,
- 0713 048 035,
- dirayamafanikio@gmail.com
.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)