Jan 5, 2016
Hii Ndiyo Hasira Kubwa Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kufanikiwa.
Naamini
umzima wa afya mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO na unaendelea kujifunza kila
siku ili kuboresha maisha yako. Katika makala yetu ya leo naomba nianze kwa
kukuuliza swali hili, hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini simba anaua?
Unaweza
ukawa unaashangaa au kwako ukaona ni swali la kawaida, lakini pamoja na hivyo je,
umeshawahi kujiuliza kwa nini sImba anaua? Bila shaka wengi wetu tunatambua
sifa alizonazo mnyama huyu kuwa ana nguvu, hasira na anauwezo mkubwa wa kuua
vitu vingi sana. Sasa je, ni kwa nini huwa anaua?
Hivyo
ni rahisi kusema anaua kwa sababu ana nguvu, hasira na pengine kutaka kujionyesa
kwamba yeye ndiye mbabe wa wanyama wote ndiyo maana akikutana karibia na kila
kitu ni halali yake. Lakini je, huu ndiyo ukweli ulio ndani ya simba anaua kwa
sababu hizo tu?
Ukweli
wa mambo ulivyo siku zote simba anaua siyo kwa sababu ana hasira sana au ana nguvu
nyingi ameamua kuzitumia, hapana. Siku zote shauku ya simba kuua inaongozwa na
njaa aliyonayo. Mara nyingi njaa aliyonayo ndiyo inayomwongoza kufanya chochote
kile na kuhakikisha mpaka anapata
mawindo yake.
LAZIMA UWE NA HASIRA YA MAFANIKIO |
Kila
anapokuwa ana njaa anakuwa ana hasira, nguvu na uwezo mkubwa wa kuraua kitu
chochote kinachojitokeza mbele yake bila kuogopa kitu chochote. Kwa hiyo utaona
siyo ubavu au nguvu zake nyingi ndizo zinazomuongoza kuua bali ni njaa
aliyonayo.
Kupitia
maisha haya ya simba bila shaka moja ya jambo muhimu sana ambalo tunaweza
kujifunza la kimafanikio ni lazima kuwa na hasira ya mafanikio ili kufanikiwa.
Bila kuwa na hasira hii ni ngumu sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Watu
wengi wana hulka au tabia ya kutafua mafanikio huku ndani yao wakiwa hawana ile
hasira inayowaongoza kutafuta mafanikio hayo. Matokeo yake wamekuwa na hasira
na vitu vidogo vidogo ambavyo haviwasaidii badala yake kuelekeza hasira zote
kwenye kutafuta mafanikio.
Hebu
jaribu kujiuliza je, una hasira, hamu na njaa ya kutosha kuhakikisha kuona
ndoto zako zinatimia? Kama una hasira hii ya mafanikio hongera sana, upo kwenye
njia sahihi ya kufikia mafanikio yako makubwa..
Mara
nyingi unapokuwa na hasira ya mafanikio ndani yako unakuwa king’ang’anizi
usiyekubali kushindwa kwa sababu unajua kuna kitu ambacho unakitafuta. Hata
inapotokea umeshindwa utajaribu tena na ntena mpaka kufikia mipango na malengo
yako.
Suala
la kuahirisha au kujishusha linakuwa halipo kwako maana unacholenga kwako ni
matokeo chanya. Hii ndiyo hasira kubwa unayotakiwa kuwa nayo ili kufanikiwa.
Achana na hasira za kipuuzi ambazo zinakuumiza na kukurudisha nyuma, kuwa na
hasira na maisha yako utafanikiwa.
Kama
tulivyoona simba siku zote anaua kwa sababu ana hasira/njaa ya mafanikio. Hivi
ndivyo unavyotakiwa kuwa na wewe. Leta matokeo chanya ya maisha yako kwa sababu
una hasira au njaa au hamasa ya kufikia mafanikio yako. Ukiweza kufanya hivyo
utafikia mafanikio yako makubwa unayoyahitaji.
Nakutakia
siku njema sana rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO. Kikubwa kwako endelea
kuwashirikisha wengine kuweza kujifunza.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.