Jan 26, 2016
Tabia 5 Unazotakiwa Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.
Ili
kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri ni safari inayohitaji
kujituma na uwe mvumilivu hadi kufikia mafanikio hayo. Wengi hujikuta kushindwa
kufikia mwisho wa safari hii kwa sababu mbalimbali zinazowakabili. Lakini moja
ya sababu hizo ni tabia mbaya wanazokuwa nazo hasa pale wanapokuwa na pesa.
Unaweza
ukashangaa kwa nini naziita tabia mbaya? Usipate tabu, hizi ni tabia mbaya kwa
sababu ndizo zinazowakwamisha na kuwarudisha wengi nyuma kimafanikio zaidi.
Sasa wengi wanakuwa ni watu wa kushikiria tabia hizi ambazo wanatakiwa kuziacha
mara moja. Kwa kung’ang’ania huko huwarudisha nyuma sana kimafanikio.
Je,
unajua ni tabia zipi unazotakiwa kuziacha mara moja hasa pale unapokuwa na
Pesa?
Zifuatazo Ni Tabia 5 Unazotakiwa
Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.
1. Kutokupangilia matumizi.
Ili
uweze kufanikiwa na kutunza pesa ulizonazo ni vyema sana ikiwa utapangalia
matumizi yako kila siku. Unapokuwa unapangilia matumizi yako inakuwa inakusaidia
sana kutokutumia pesa zako hovyo. Ni rahisi sana kutumia pesa zako hovyo kama
hujaandika popote. Kutokupangilia matumizi ni moja ya tabia unayotakiwa kuiacha
mara moja ili kufanikiwa.
PANGILIA MATUMIZI YAKO VIZURI. |
2. Kutumia kila pesa unayoipata.
Mara
nyingi watu walio wengi hutumia pesa zao zote walizonazo bila ya kuweka akiba
hata tone. Haya ni maisha ambayo wengi wamekuwa nayo na wanayaishi kila siku. Kila
wanapoulizwa kwa nini iko hivyo, sababu yao ni moja tu kwamba pesa haiwekekiki.
Na kwa imani hiyo hujikuta hakuna akiba wanayoiweka na kubaki kuishi maisha
magumu. Kama nia yako kubwa ni kufanikiwa achana na tabia hii mara moja.
3. Kufanya matumizi yasiyo ya lazima.
Kuna
watu wanapokuwa na pesa huwa zinawasumbua sana. huwa ni watu wasiotulia kwa
kutaka kununua karibu kila kitu wanachokiona mbele yao. Unapokuwa na tabia hii
kwa uhakika unakuwa sio rahisi kuweza kufanikiwa. Kitu ambacho kinakuwa
kinakufanya ushindwe kufanikiwa ni kwa sababu pesa zote unakuwa unazitumia
hovyo na kushindwa kuweka hata akiba ya kukusaidia
4. Kutokuweza.
Utakuwa
upo kwenye hatari sana kwenye maisha haya kama utakuwa unaishi maisha bila ya
kuwekeza. Kuwekeza ni jambo la msingi sana ambalo unatakiwa ulitilie mkazo kwa
kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi. Ili uweze kufanikiwa
unalazimika kuwekeza pesa zako na sio suala kutumia tu. Kutokuwekeza ni moja ya
tabia unayoitakiwa kuicha ili kujenga mafanikio ya kudumu.
5. Kushindwa kulipa madeni yako
mapema.
Yapo
madeni ambayo wengi hutakiwa kulipa mapema, lakini hata hivyo wengi pia
hujikuta wanashindwa kulipa madeni hayo kwa muda mwafaka. Kitu cha msingi hapa
kama kuna madeni unadaiwa kwa mfano ada za watoto, kodi mbalimbali ni vyema
ukalipia mapema na kwa utaratibu ili kujiepusha na usumbufu ambao unaweza
ukjitokeza kwako kwa baadae.
Kama
utachukua hatua na kuamua kuachana na tabia hizo utajijengea mazingira ya
kufikia mafanikio makubwa kwako kwa kadri siku zinavyokwenda kwenye maisha yako.
Nakutakia
siku njema na mafanikio makubwa yawe upande wako. Kumbuka endelea kujifunza
kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.