Jan 21, 2016
Mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.
Sasa
baada ya utafiti wa muda mrefu imegundulika kwamba macho yetu yana uwezo wa
kutufundisha mengi sana ikiwa tutakuwa tunayachunguza kwa umakini. Wataalamu
hao wamegundua macho yetu yana uwezo wa kutuonyesha mambo mbalimbali kama tunasema uongo au ukweli, kutuonyesha jinsi tunavyofikiri na hata kutoa
mustakabali wa afya zetu.
Kwa mujibu wa wataalamu hawa wanadai kwamba yapo
mambo mengi yaliyofichika kwenye macho yetu bila hata sisi wenyewe kuelewa. Hii
ni sayansi ambayo inaweza ikawa ya kustaabisha kidogo kwako, ingawa ukweli wa
mambo ndivyo ulivyo na utabaki hivyo. Ni vyema sana kama ukafahamu vizuri mambo yaliyofichika
kwenye macho yako.
Yafutayo
Ni mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.
1. Magonjwa uliyonayo.
Kwa
mujibu wa tafiti zilizofanyika zinaonyesha kwamba rangi za macho yetu
zinauhusiano mkubwa wa moja kwa moja na baadhi ya magonjwa yanayotupata. Kwa mfano
watu wengi wenye macho yanayoonyesha rangi ya ‘bluu’ hawa hupatwa sana na magonjwa ya kisukari, mabaka mabaka mwilini
na kansa ya ngozi.
Lakini
hata hivyo kuna wengine wanakuwa wana macho yana rangi za aina mbili kwa mfano
labda ‘bluu’ na ‘brown’. Kwa watu kama hawa magonjwa yanayowakumba ni kama vile
ngozi kukakamaa maeneo ya usoni. Kwa hali hiyo ukichunguza watu wenye macho ya
rangi ya ‘bluu’ wengi wanasumbuliwa sana na magonjwa hayo.
MACHO RANGI YA 'BLUU' |
2. Haiba yako.
Macho
yako pia yana uwezo mkubwa wa kuonyesha haiba uliyonayo. Kwa mujibu wa utafiti
uliofanyika Australia na jopo la
waataalamu lililoshirikisha watu 366,
utafiti huo unaonyesha kwamba watu wenye macho hasa ya mng’ao (bright
eyes) mara nyingi hawa wana mvuto mkubwa sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na
kwenye masuala ya kimapenzi.
Na
wakati huo watu wenye macho meusi (dark eyes) utafiti huu unaonyesha hawa ni
watu ambao hawana mvuto sana katika jamii, mara nyingi huwa ni wa kimya na
mambo yao kwa ujumla usipowachunguza hata kidogo huwa yanayoonekana ni kama
vile hayaeleweki na ni ngumu kuwatambua kirahisi.
UGONJWA WA MABAKA MABAKA (VITILIGO) |
3. Maumivu unayobeba.
Pia
utafiti unaonyesha macho yana uwezo wa kuonyesha kwamba wewe ni mtu mwenye
uwezo wa kubeba maumivu ya aina gani. Kwa mfano wanawake wenye macho ya mng’ao
(bright eyes) utafiti unawaonyesha kwamba hawa hupata maumivu kidogo pale
wanapojifungua tofati na wanawake wenye macho ya ‘dark blue’.
Wanawake
hawa wenye macho ya mng’ao ( bright eyes)
si tu kwamba wanakuwa wana maumivu madogo wakati wanajifungua lakini pia
ni watu wenye hofu kiasi, hawana msongo wa mawazo mkubwa na pia si watu wa
kuwaza hasi sana. Pia hiyo haitoshi inapotokea wakanywa pombe kwao huwa sio
rahisi sana kulewa.
MACHO RANGI YA 'BROWN' |
4. Maumbile yako.
Ni
ukweli ulio halisi pia macho yako yana uwezo wa kututambulisha maumbile (Genetics)
ulizonazo. Kwa mfano mwaka 2008 wanasayansi waliweza kugundua kwamba watu wote
wenye macho ya ‘bluu’ wamerithi
maumbile au genetics moja kwa moja kutoka kwa baba zao. Kwa hiyo ni watu
wanaofanana na baba zao.
Pia
si hivyo tu, watu hawa wenye macho ya ‘bluu’
wamerithi pia mambo mengi kutoka kwa babu zao. Wana vitu vinavyofanana na babu
zao na pia kutoka kwa baba zao. Kwa msingi huo utagundua watu hawa wenye macho
ya ‘bluu’ mambo mengi warithi sana
kutoka kwa baba au babu zao.
MACHO RANGI YA MNG'AO (BRIGHT EYES) |
5. Namna gani unavyoaminika.
Macho
ulionayo yana uwezo wa kutuonyesha jinsi unavyoamika. Utafiti unaoyesha watu
wengi wenye macho ya ‘brown’ ni watu wa kuaminika sana katika jamii kuliko watu
wenye macho tofauti na hayo.
Hivyo
basi, macho yako yanauwezo wa kubeba haiba, maumbile, uaminifu, maumivu na hata
magonjwa. Hayo ndiyo mambo yanakuwa yamefichka mara kwa mara kwenye macho yetu.
Nikutakie
siku njema sana na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.