Jan 18, 2016
Mitazamo Mikubwa Mitatu Inayoathiri Maisha Yako.
Kitu
pekee ambacho pengine kitakufanya ushindwe kufanikiwa katika viwango vya juu ni
mtazamo ulionao, hasa usipokuwa makini. Na sio elimu. Sio pesa. Sio jamii inayokuzunguka.
Sio marafiki zako na wala sio bahati au mkosi ulionao. Ni mtazamo tu peke yake
ulionao juu ya maisha yako.
Ukumbuke
mpaka sasa maisha uliyonayo ni matokeo ya mitazamo uliyojijengea siku za nyuma.
Mtazamo ulionao juu ya maisha ndio umekufanya uwe kama ulivyo na kukutofautisha
na wengine. Kwa hiyo ipo athari kubwa
sana ya mtazamo ulionao kwenye maisha yako.
Wengi
huwa hatujui na kujikuta tukibeba mitazamo mingi inayotukwamisha. Ili kuepuka jambo
hilo lisitokee kwako tena ni vyema ukajua mitazamo ambayo ina nguvu kubwa ya
kuathiri maisha yako. Na kwa kawaida katika maisha ipo mitazamo ya aina tatu
ambayo ni muhimu sana kwako kuijua.
1. Mtazamo wa kushindwa.
Siku
zote watu walioshindwa huiona dunia haina usawa. Dunia inawaonea na haiwatendei
haki. Mara nyingi watu hawa huona matatizo waliyonayo ni makubwa kuliko ya
wengine. Hufikiri wao ndio wanaokutana na changamoto nzito za maisha na hufika
mahali hutamani sana kutaka kusaidiwa au kuonewa huruma. Kwa watu wenye mtazamo
huu, maisha yao ni mabaya na ya kushindwa karibu siku zote.
JIJENGEE MTAZAMO WA USHINDI. |
2. Mtazamo dumavu.
Watu
wengi wanaobeba mtazamo huu mara nyingi huona mambo mengi sana hyawezekanai
katika maisha yao. Kila kitu unacho muelekeza juu ya maisha mtu mwenye mtazamo
wa aina hii atakupa sababu haiwezekani. Siku zote ni watu wa kuishi kwa
matumaini kwamba ipo siku mambo yatakuwa mazuri. Pia ni rahisi kwao kukata
tamaa wanapokutana na vikwazo. Watu wengi wenye mtazamo huu huwa hawafanikiwi sana. Kwa kifupi huonekana kama wamedumaa kimafanikio.
3. Mtazamo wa ushindi.
Watu
wenye mtazamo huu huiiona dunia kama sehemu wanayoweza kuitengeneza wao. Wanaamini
sana maisha yapo mikononi mwao na si kwa mtu mwingine. Huweka nguvu na juhudi
zote kuhakikisha wanafanikiwa. Ni watu wa kuchapa kazi. Pia ni watu chanya
ambao huwa si rahisi sana kukatishwa tamaa. Hawa ndio huwa washindi na wenye
mafanikio makubwa.
Unaweza
ukajikagua mwenyewe na kuangalia ni aina gani ya mtazamo ulionao? Je, kama una
mtazamo wa ushindi na je, kesho mambo yakienda
kinyume chake huo mtazamo chanya utakuwa nao tena? Hakuna mtu atakaye
kulazimisha uwe na mtazamo wa aina fulani, bali ni suala la kuamua mwenyewe.
Kumbuka,
kila siku. Kila wakati. Kuna mtazamo unaouchagua.
Kuwa
makini juu ya mitazamo hiyo unayoibeba mara kwa mara.
Tunakutakia
siku njema iwe ya mafanikio kwako.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.