Jan 27, 2016
Mambo Ambayo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kuyafanya Kwenye Maisha Yako Yote.
Habari za siku mpenzi
msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Naamini umeianza siku yako ya leo
ukiwa mzima wa afya na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako kwa kujifunza
na kupata maarifa ya kukusaidia kwenye safari ya mafanikio.
Nakukaribisha kama
kawaida yetu kuweza kujifunza tena. Katika makala yetu hapa leo, tutajifunza
kuangalia yale mambo ambayo tunatakiwa kuwa wa kwanza kila siku kuyafanya
katika maisha yetu. Kwa kadri tutakavyozidi kuwa wa kwanza kuyafanya mambo hayo
yatasaidia sana kuboresha maisha yetu.
Yafutayo Ni Mambo Ya
Msingi Ambayo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kuyafanya Kwenye Maisha Yako.
1.
Siku zote katika maisha yako jifunze kuwa wa kwanza kunyanyuka hasa pale inapotokea
umeshindwa kwa lile jambo unalolifanya. Acha kufanya kosa la kubakia hapo ikiwa
umekosea nyanyuka haraka na endelea na safari.
2.
Kuwa wa kwanza kuomba msamaha inapotokea umewakosea wengine. Ni kweli huwa
tunawakosea wengi, lakini je wewe binafsi huwa ni wa kwanza kuwaomba msamaha,
kama hufanyi hivyo anza sasa kusamehe mapema.
3.
Kuwa wa kwanza siku zote kujifunza inapofika wakati unakosolewa. Jifunze
kwanini wanakukosoa hivyo na kisha chukua kukosolewa huko kama somo au daraja
la kukusaidia kuendelea mbele kimafanikio.
JIFUNZE HARAKA UNAPOKOSEA. |
5.
Kuwa wa kwanza siku zote kuonyesha ukarimu kwa watu wanaokuzunguka. Na
inapotokea wengine wanata msaada wasaidie bila kinyongo, hiyo ni njia bora itakayokutengenezea
maisha mazuri na jamii inayokuzunguka kwa ujumla wake.
6.
Kuwa wa kwanza pia kutaka kuhoji pale unapoona mambo yako mengi hayaendi vizuri
kwako. Inapotokea mipango imekwama jiulize kwa nini iko hivyo kwako. Kwa jinsi
utakavyojiuliza hivyo utapata majibu mengi yakukusaidia.
7.
Kuwa wa kwanza katika maisha yako kung’ang’ania mafanikio yako, mpaka yatokee.
Usikatishwe wala usizuiliwe na kitu chochote. Jiwekee falsafa ya kuwa king’ang’anizi
mpaka uone ndoto zako zote kubwa ulizojiwekea zinatimia.
8.
Jifunze kuwa mtu wa kwanza kufurahia mafanikio unayoyapata hata kama ni kidogo.
Unapofanikiwa ni vyema ukajijengea utamaduni wa kujipongeza kwa kile
ulichokifanikisha. Hapo utavuta nguvu mpya za kutafuta mafanikio mengine tena.
9.
Endelea kujifunza kuwa wa kwanza kufanya lile jambo ambalo unaliogopa sana
kwenye maisha yako. Kwa kulifanya jambo hilo litakusababisha wewe ule woga
uliokuwa nao kupotea kabisa.
10.
Kuwa wa kwanza pia kuamini kwamba ipo nafasi nyingine ya kujaribu tena na tena,
ikiwa umetokea umeshindwa kwa mara ya kwanza. Kushindwa kwako kusikufanye ukaamini
huo ndio mwisho dunia. Jaribu tena kama umeshindwa mpaka utafanikiwa.
11.
Kuwa wa kwanza kufanya yale mambo ambayo wengine wanayatolea sababu kuwa
hawawezi kuyafanya. Mambo yanayochosha, yanayokatisha tamaa, ambayo yanaonekana
kama hayana matumaini tena. Kuwa wa kwanza kuyafanya mambo hayo.
12.
Kuwa wa kwanza kumsaidia yule ambaye hajiwezi, pengine amekosa mtu wa kumsaidia
kabisa. Mtu huyo msaidie kimawazo, mpe moyo na nguvu kubwa ya kuona maisha kwa
upya. Kuwa wa kwanza.
Kwanini
unatakiwa kuwa wa kwanza katika mambo haya? Unapokuwa wa kwanza kwa mambo haya
hii itakusaidia sana kukuweka tofauti kidogo na mazoea ya wanayofanya watu
wengine na pia itakujengea kubadili sana maisha yako na ya wengine kimafanikio.
Nikutakie
siku njema, kumbuka kuendelea kuwashirikisha wengine kuzidi kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.