Jan 14, 2016
Mambo Ya Msingi Ambayo Ni lazima Uyajue Katika Biashara Yako.
Habari
za siku mpenzi msomaji wangu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Bila shaka
naamini umzima wa afya na unaendelea kuchota maarifa bora kabisa ya kukusaidia
kufikia mafanikio uliyojiwekea. Kumbuka siku zote kujifunza ni msingi mkubwa
sana wa mafaniko yako.
Leo
katika makala yetu tutajifunza jinsi ambavyo unavyoweza kuifanya biashara yako
kuwa ya mafanikio kwa kuangalia mambo ya msingi kabisa ambayo ni lazima uyajue.
Kwa kutambua mambo haya itakuwa chachu kubwa kwako ya kukuwezesha kuendelea
mbele.
Bila
kukupotezea muda naomba nikutajie mambo ya msingi ambayo ni lazima uyajue
katika biashara yako.
1. Kusukuma mambo ambayo hayaendi
sawa.
Siku
zote katika maisha mambo huwa hayendi sawa kwa asilimia mia moja kama
tulivyokuwa tukitegemea. Inapotokea mipango au malengo yako hayajaenda sawa,
kitu kinachofuata kwako ni kutumia mbinu zote na kuhakikisha mipango hiyo
inaenda sawa kama ilivyopangwa na siyo tena kuacha.
Kwa
hiyo unapoona mipango yako haiendi sawa, jukumu la kwanza hakikisha unatafuta
njia nyingine mpaka kila kitu kikae vizuri. Kwa mfano inapotokea wateja unaona
wamepungua jukumu ambalo unatakiwa uwe nalo siyo kuacha hivyo bali ni kutafuta
wateja popote walipo mpaka kufanya kila kitu kiwe sawa ikiwa ni pamoja na kutoa
matangazo.
KUWA KING'ANG'ANIZI WA MALENGO YAKO. |
2. Kuwa king’ang’anizi wa malengo
yako.
Najua
kuna malengo ambayo ni lazima utakuwa umejiwekea kwenye biashara uliyonayo. Labda
unaweza ukawa umejiwekea malengo ya baada ya muda fulani biashara yako itakuwa
imefikisha ukubwa huu au itakuwa ina mtaji wa kiasi fulani. Haya ni malengo
mazuri sana ambayo kila mtu anatakiwa awe nayo ili biashara yake iweze kukua.
Lakini
kwa bahati mbaya kama niliyotangulia kusema hapo awali mambo siku zote huwa
hayaendi sawa kama tunavyotaka. Kuna wakati ni lazima tukutane na changamoto. Inapotokea
changamoto yoyote kwenye biashara yako, jaribu sana kuwa king’ang’anizi wa
malengo yako mpaka ndoto zako zitimie. Acha kuyumbishwa na changamoto hizo na
mwisho wa siku ukaacha malengo yako muhimu.
3. Penda kile unachokifanya.
Itakuwa
ni ngumu sana kufanikiwa ikiwa ndani yako huna mapenzi sana na kile
unachokifanya. Uzoefu unaonyesha hivi mara nyingi wengi wanaofanikiwa wanapenda
yale wanayoyafanya. Unapokuwa unapenda kile unachokifanya inakuwa ni rahisi
sana kwako kusonga mbele hata pale unapokutana na vizuizi vya hapa na pale.
4. Jiandae vizuri.
Silaha
mojawapo ya kukufanya ufanikiwe katika biashara yako ni kufanya maandalizi
mazuri. Unapojiwekea maandalizi muhimu ikiwa pamoja na kujua mapema changamoto
unazokutana nazo katika biashara au washindani wako itakusaidia kufanikiwa kwa
kiwango cha juu katika biashara yako. Kumbuka siku zote mafanikio yanatokea
hasa pale maandalizi mazuri yanapokutana na fursa.
Kwa
mambo hayo manne ukiyajua, yatakujengea msingi mzuri wa kufikia mafanikio
makubwa katika biashara yako.
Nakutakia
siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.