Jan 29, 2016
Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa.
Kila
kitu kilichopo dunia kinaongozwa na sheria zake. Sheria hizo zinapotumika
ipasavyo mara nyingi sana huleta mafanikio makubwa. Na inapotokea sheria hizo
zikavunjwa hakuna mafanikio yanayokuwepo zaidi ya kushindwa kwa wale wote
waliovunja sheria hizo.
Haijalishi
upo katika eneo gani sheria ni muhimu sana kuzingitiwa. Iwe katika afya, elimu,
mchezo wa mpira wa miguu, au biashara sheria huwa zipo na zinafanya kazi.
Sheria hizi ndizo zinazotupa mwongozo bila kujali uwe unazijua au huzijui
lakini zipo, ukikosea unahukumiwa.
Katika
makala hii tutajifunza sheria zitakazo kusaidia kufanya biashara yako kwa
ushindi. Bila shaka umekuwa ukiona wengi wakifanya biashara zao kwa mazoea
sana. Kutokana na mazoea hayo hupelekea biashara nyingi kugeuka kuwa kama ‘miradi bubu’ ambayo haina faida yoyote.
Sitaki
hilo lizidi kukutokea sana la kufanya biashara ambayo haikupi faida kubwa
unayoifikiri kwa muda mrefu. Inabidi ukubali umekosea na kaa chini ujifunze
sheria za msingi kabisa ambazo zinaweza kukusaidia kukutoa hapo na kukupeleka katika
hatua nyingine ya mafanikio kibiashara.
Zifuatazo
Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa.
1. Toa huduma bora kwa wateja wako.
Toa
huduma bora itakayowafanya wateja wako waweze kujisikia vizuri na kushawishika
kuja kununua tena kwa wakati mwingine. Kwa kutoa huduma bora itakusaidia sana
kutokuendesha biashara yako kimazoea. Ila ikiwa utajisahau au kusahau sheria
hii basi elewa utajitengenezea mazingira ya kushindwa kiurahisi kwenye biashara
unayoifanya.
TUNZA MTAJI WAKO. |
2. Jijengee mazoea ya kuwa na lugha
ya ukarimu.
Hili
ni jambo litakalokusaidia sana kukuza biashara yako kwa sehemu kubwa. Kuna
wakati unakutana na wateja ambao ni wakorofi hawaeleweki. Tambua hutakiwi
kuwaonyesha chuki wala kuwasemesha kwa lugha ya ukali. Toa lugha ya ukarimu
wakati wote unapokuwa kwenye biashara yako.
3. Jali sana muda wa wateja wako.
Kitu
kizuri kabisa kitakachokufanya uweze kujijengea uaminifu na kukuza wateja wako
ni uwezo wako wa kujaali muda wa wateja. Muda ni kitu cha muhimu sana kwa mteja
wako. Kwa namna yoyote ile usimpotezee mteja wako muda wake. Jitahidi sana
kumhudumia katika muda mwafaka ambao amefika na sio kumchelewesha bila sababu
ya msingi.
4. Mazingira yako yawe safi.
Kila
wakati na kila siku, hakikisha mazingira ya unapofanyia biashara yako yawe safi.
Lakini si mazingira tu hayo yawe safi bali hata wewe na wahudumu wako lazima
muwe wasafi ili kuhakikisha kumvutia wateja katika eneo watakalo kaa. Hii ni
sheria nzuri sana ambayo inaweza kupelekea kukuza wateja wako siku hadi siku.
5. Weka matangazo ya biashara yako.
Ni
vyema ukajitengenezea matangazo ya biashara yako. Hakuna biashara ambayo
inaweza ikakua sana bila kuwa na matangazo. Matangazo ni muhimu sana kwa
biashara yoyote. Matangazo yanaisadia biashara yako kuweza kujulikana katika
maeneo mengi ambayo ilikuwa sio rahisi kuweza kujulikana na kwa muda mrefu.
6. Simamia kauli zako.
Unapokuwa
kwenye biashara muda wako wote hakikisha unafanya kile unachokisema. Simamia
kauli zako, bila kuyumbishwa. Kama uliwaambia wateja wako mzigo utaletwa wiki
ijayo , hakikisha hilo linatekelezeka pia. Kwa kifupi hapa hutakiwi kuwa
mwongo. Toa taarifa sahihi zitakusaidia kukuza wateja wako na kuwa wengi.
7. Kuwa mwangalifu na mtaji wako.
Pamoja
na kwamba biashara yako inaweza ikawa imeanza kukupa ile faida inayotarajiwa,
lakini ili kuikuza na kuifanya kwa ushindi zaidi ni vyema ukawa mwangalifu na
mtaji wako. Acha kutumia pesa zako hovyo sana ambazo zipo kwenye biashara.
Tunza mtaji wako ukusaidie kuweza kuwekeza pia katika maeneo mengine muhimu.
8. Jenga mazoea ya kujifunza siku
zote.
Hapa
nikiwa na maana jifunze kutoka kwa wenzako wanafanya nini? Jifunze kwako pia
hasa kile kipindi unapotokea umekosea. Ukikosea acha kujibebesha hasira ambazo
zinaweza kukubomoa na kukuharibu. Badala yake kaa chini, kisha jifunze kwa nini
umekosea katika hili. Na baada ya hapo rekebisha na endelea na safari.
Kwa
kuzijua sheria hizi zitakusaidia sana kuweza kuendesha biashara yako kwa
ushindi na mafanikio makubwa.
Nikutakie
siku njema na pia napenda kukumbusha endelea kuwakumbusha wengine kuendelea
kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.