Jan 28, 2016
Hawa Ndio Watu Ambao Hawadumu Sana Katika Ndoa Zao.
Baada
ya kusemwa kama hadithi, hivi sasa imethibitika kwamba, watu wanaooana kwa sababu
ya kuvutana kimwili, kimtazamo, imani za dini zao na nasaba wanazotoka,
hawawezi kudumu kwenye ndoa kama tabia zinatofautiana.
Kuna
watu ambao huoana kwa sababu tu ni waumi wa dhehebu moja. Wengine huoana kwa
sababu wazazi wao wanatoka kwenye familia za kiwango cha juu kimapato au
kisomi, ama kiwango cha chini. Wengine huona kwa sababu wana mitazamo ya aina
moja kwenye jambo fulani. Huku wengine wakiona kwa sababu ni kabila moja.
Imethibitika
sasa kwamba, nusu ya ndoa zinazofungwa kwa sababu hizo, huwa hazidumu. Tafiti kadhaa
zinaonesha kwamba, ndoa zinazodumu ni za wale watu ambao wameoana kwa sababu
kila mmoja amezijua tabia za mwingine na kukubaliana nazo.
Lakini
kikubwa kilichobainika ni kwamba, wanaooana
na kudumu kwenye ndoa, ni wale ambao wanalingana tabia kwa sehemu kubwa.
Bila kujali kila mmoja anatoka na familia ya namna gani, dini au mitazamo,
tabia zikikaribiana kulingana, uwezekano wa kuishi katika ndoa ya amani ni
mkubwa sana.
TABIA NJEMA KWENYE NDOA NI MUHIMU SANA. |
Kwa
kuwa ni vigumu sana kwa watu kujua tabia zao, kuoana kwingi kumefungwa kwenye
vigezo nilivyovitaja ambavyo ni muda. Baada ya muda fulani kwenye ndoa,
wanandoa hugundua kwamba, vigezo vilivyotumika kuwaunganisha, havina uwezo wa
kuwafanya wadumu tena kwenye ndoa hiyo.
Hii
ina maana kwamba, wapenzi wanapokuwa na tabia zinazokaribiana, ndoa yao pia
inaweza kuwa imara zaidi. Lakini wapenzi kuunganishwa na dini zao, hadhi yao
katika jamii na mitazamo fulani, haiwezi kuwahakikishia wanandoa kuwa na ndoa
imara.
Mitazamo
fulani ya aina moja, imani ya dini au kiwango sawa cha kipato kifamilia,
huwavuta watu awali wanapokutana na kuoana. Hii inatokana na ukweli kwamba,
sifa hizi huonekana haraka na ni sifa muhimu kwa watu wengi katika kuendesha
maisha yao, wakati tabia zimejificha.
Huchukua
muda kwa mtu kugundua tabia halisi za mwingine. Bahati mbaya sana mtu anapohisi
kwamba fulani amempenda, huweza kuficha udhaifu wake kitabia na hivyo kuwa
ngumu zaidi tabia kuchukuliwa kama kigezo, wakati ndicho kigezo halisi
kinachotakiwa kutazamwa kabla watu hawajaamua kuoana.
Lakini
bahati mbaya ni kwamba, kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye ndoa, ndivyo tabia
zinavyojitokeza na kuwa muhimu sana katika kuimarisha ndoa hiyo. Kwa hiyo, kama
tabia hazifanani, ina maana kwamba, kadri siku zinavyoenda, ndivyo wanandoa
wanavyozidi kushindana.
Uhusiano
imara na wenye faraja unahitaji mawasiliano ya mara kwa mara kuhusiana na
shughuli za wanandoa, masuala mbalimbali, matatizo na suluhu za mambo mengi ya
kimaisha. Kama tabia za watu wawili haziwiani katika mambo, ni wazizi kutakuwa
na tatizo.
Baadhi
ya watafiti wanasisitiza kwamba watu wote ambao wanaingia kwenye ndoa huku
wakijua kwamba kitabia hawakaribiani, ni sawa na kupiga mbizi baharini wakati
mtu hajui kuogelea.
Pale
ambapo watu wanataka kufunga ndoa, wanaona wazi wazi kuwa kitabia ni watu wawili
tofauti sana, hawashauriwi kuendelea na zoezi hilo kwani litawaumiza vibaya
sana hapo baadae.
Kama
tabia zinalandana sana, bila kujali kama ni watu wadini moja, uwezo sawa wa
kifamilia, kabila moja na mitazamo fulani ya aina moja, watu hao hao wanaweza
kutabiriwa bila wasiwasi kwamba, ndoa yao itadumu.
Nikutakie
siku njema na mafanikio bora katika ndoa yako. Endelea kujifunza kupitia DIRAYA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri uwe wa kibiashara/maisha, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.