Jan 15, 2016
Acha Kusahau Kufanya Mambo Haya Kwenye Maisha Yako.
Habari
rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO ni imani yetu kubwa ya kwamba
umzima wa afya na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako. Kama ilivyo kawaida
yetu tunakukaribisha tena ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kujifunza juu ya
mafanikio.
Katika
siku ya leo tutaangalia mambo ya msingi ambayo hutakiwi kusahau kuyafanya
kwenye maisha yako. Kabla hatujaendelea naomba nikukumbushe kwamba, mara nyingi
wengi wetu kuna wakati hujikuta tuna nia kubwa ya kutoa au kusaidia wengine
waliokaribu nasi.
Hata
kama sio kila siku ila kutoa msaada kwa wengine hasa pale nafasi inapopatikana
ni kitu ambacho wengi wanakipenda. Hebu jaribu kufikiria zile nyakati za sikuu
kubwa kama mwaka mpya ama ‘valentine day’,
bila shaka wengi wetu hutaka kutoa zawadi kwa wale waliokaribu zetu.
Je,
unafikiri ni kwa nini hali hii huwa iko hivyo, kwa karibu kila mtu kujisikia
mhemuko wa kutaka kutoa zawadi fulani kwa aliyekaribu naye? Ni kati gani
ambacho huwa kinasababisha? Kwa kawaida huwa zipo sababu nyingi, lakini mojawapo ya sababu hizo ni kama zifuatazo;-
§ Tunakuwa
tunatoa kwanza ili kuonyesha kwamba tunajali…
§ Tunatoa
ili tuweze kuona furaha ya kukubaliwa…
§ Pia
tunatoa kwa kutegemea faida ya baadae kwa wale tunawaotolea mambo hayo…
Kama
nilivyosema sababu zake huwa zipo nyingi kulingana kati ya mtu mmoja na
mwingine na ni jambo zuri kuonyesha kwa wale waliokaribu nao.
MAONO NI LAZIMA KWENYE SAFARI YA MAFANIKIO. |
Pamoja
na uzuri wote huo ambao huwa tunauonyesha sana kwa wale waliokaribu yetu kuwa
tunawajali na tunawapenda. Lakini kuna mambo ambayo huwa tunasahau sana kujipa
sisi wenyewe kwanza. Haya ndiyo mambo yaliyotakiwa tuwe tunajipa sisi wenyewe
kwanza ili kufanikiwa.
Unaweza
ukasema ‘Aaah sasa Imani unataka kuleta
ubinafsi’ sio hivyo haya ni mambo ya lazima kujipa na kujitolea wewe kila
wakati bila kuchoka kwani ndio msingi wa maisha yako ya mafanikio. Naamini una
nia ya kufanikiwa, kama ni hivyo, acha kusahau kufanya mambo haya kwenye maisha
yako.
Jambo la kwanza.
Kitu
ambacho hutakiwa kusahau kujipa kwenye maisha yako kila siku ni Hamasa.
Unatakiwa kujifunza kujipa au kujitolea hamasa kila siku bila kuchoka. Kwa kadri
unavyozidi kuwa na hamasa kubwa ndivyo ule ‘moto’ wa mafanikio unakuwa unawaka
ndani yako.
Wengi
wanakuwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa ile hamasa kubwa ambayo
inaweza ikawafanya wakasonga mbele. Hamasa inakuwa ni kama mafuta ya kukusaidia
kuweza kuendelea na safari ya mafanikio bila kuchoka siku zote. Hili ni jambo
la kwanza ambalo hupaswi kulisahau kujipa.
Jambo la pili.
Mbali
na hamasa jambo lingine ambalo unatakiwa kujipa na kutolisahau katika maisha
yako ni maono (Vision). Ni lazima siku zote uwe na maono makubwa juu ya maisha
yako. Ni lazima ujue baada ya miaka fulani utatakuwa wapi. Bila maono maisha
yako yanapotea bure.
Kwa
hiyo kila wakati jipe tathmini kwa kuangalia maisha yako. Hiki ni kitu kizuri
sana kitakachoweza kukusaidia kujiweka katika nafsi nzuri ya kufanikiwa. Watu
wote ambao mara nyingi ni wabeba maono maisha yao huwa ni ya mafanikio makubwa
sana.
Jambo la tatu.
Najua
tayari umeshajifunza juu ya umuhimu wa kujipa hamasa na maono. Jambo la tatu
ambalo unatakiwa kujipa kila siku ni ukarimu. Siku zote katika maisha yako
jaribu kuwa mtu wa ukarimu. Acha kuishi maisha kama dumbwana fulani hivi ambalo
halina maana, hiyo haitakusadia sana.
Ishi
maisha ya kuwajali na kuwakarimu wengine. Kwa kadri utakavyozidi kufanya hivyo
utajikuta unazidi kujenga uaminifu mkubwa na mafanikio yatakuwa upande wako
daima.
Kila
siku kumbuka kujikumbusha mambo hayo kwani ni mambo ambayo unatakiwa kujipa
kila siku bila kuchoka.
Nikutakie
siku njema na mafanikio mema yawe kwako daima.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.