Jan 11, 2016
Mambo Matatu Ya Lazima Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
Kila
mtu ana malengo yake ambayo anakuwa anajiwekea mara kwa mara katika maisha
yake. Wengi kati yetu tumekuwa ni watu wa kujiwekea malengo siku hadi siku,
bila shaka hili halina ubishi. Wapo ambao hujiwekea malengo madogo na wengine
kujiwekea malengo makubwa. Kwa hiyo utaona kila mtu ana malengo ya aina fulani
ambayo amejiwekea.
Lakini
pamoja na kujiwekea malengo hayo, kitu cha kushangaza kwa wengi wamekuwa ni
watu wa kushindwa kufikia yale malengo yao. Najua umeshawahi kuona watu ambao
hawafanikiwi kwa sababu ya kushindwa kuyafikia malengo yao. Kitu cha kujiuliza ni
kwa nini wengine waweze kufikia malengo yao na wengine washindwe?
Je,
kwa wale wanaoshindwa kufanikiwa, malengo yao huwa ni magumu sana kuyafikia au
hayawezekani kabisa au kuna sababu nje na hapo?Ni jambo unalotakiwa kulijua na
kulifanyia kazi ili na wewe usiingie kwenye mtego wa kushindwa kufikia malengo
yako mara kwa mara.
Kwa
wengi wanaoshindwa, mbali na kukosa mipango na malengo au kuchukua hatua, kitu
kingine kinachowafanya washindwe kufikia malengo yao ni kule kushindwa kujua
mambo ya lazima wanayotakiwa kuwa nayo wakati wanajiwekea malengo. Ukiyajua mambo hayo
ni njia ya uhakika kufikia malengo yako yoyote uliyojiwekea.
Yafuatayo
Ni Mambo Matatu Ya Lazima Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
1.
Jijengee mawazo chanya.
Muda
wote wakati umejiwekea malengo yako ni muhimu sana kuwa na mawazo chanya. Acha kuwaza
kwamba utashindwa, jenga picha ya mafanikio unayoyataka ikiwa utatimiza malengo
yako. Kwa kufaya hivyo itakujengea kujiamini sana na mwisho wa siku utatimiza
malengo yako. Hili ni jambo la lazima sana kwako unalotakiwa ulijue ili kufikia
malengo yako.
KUWA NA MAWAZO CHANYA MUDA WOTE. |
Wakati
unaweka malengo yako ulijipa ahadi na kupanga kabisa utaachana na mawazo hasi,
hutafikiri kushindwa na utajituma. Kama hicho ndicho ulichojiahidi endelea
kukifanyia kazi bila kuchoka. Fanya mabadiliko yote ya muhimu na yaweke kwenye
utekelezaji mara moja bila kuacha kitu. Hiyo itakusaidia sana kufikia malengo
yako makubwa.
3. Endelea kufanyia kazi mabadliko.
Kwa
kawaida tunapoweka malengo kuna chanagamoto na mambo mengi tunayokutana nayo.
Changamoto hizo na mabadiliko yoyote endelea kuyafanyia kazi siku zote bila
kuchoka. Kama ni kuwa na mawazo chanya endelea nayo. Kama ni kufikiri ushindi
endelea hivyo hivyo mpaka mafanikio yatokee upande wako.
Kwa
jinsi utakavyozidi kutumia njia hizo, ndivyo malengo yako yatazidi kutimia kwa
uhakika mkubwa.
Nikutakie
siku njema iwe na mafanikio makubwa sana.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.