May 18, 2016
Kweli Nne (4) Kuhusu Mafanikio, Ambazo Hutakiwi Kuzisahau.
Ili
uweze kufanikiwa ni lazima uzijue kweli zenye uwezo wa kukupa mafanikio.
Haijalishi unafanya nini, ukizijua kweli, kanuni au mbinu zinazotoa mafanikio
ni lazima ufanikiwe. Hivyo haitajalisha una historia gani au unatoka katika
taifa ama familia gani kufanikiwa kwako kutakuwa ni lazima ukielewa kweli au
kanuni hizo. Mara nyingi watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya
kushindwa kuzijua kweli hizo.
Sipendi
uwe miongoni mwao ukashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutokujua mafanikio
yanataka nini. Kwa kusoma makala haya, nitakushirikisha kweli ambazo unatakiwa
kuzijua ili uweze kufanikiwa. Ni kweli ambazo zinatumiwa na wengi ikiwemo mpaka
na watu wenye mafanikio makubwa. Hakuna ubishi ukijua kweli hizi na kuzifanyia
kazi, nafasi ya kufanikiwa kwako itakuwa ni kubwa. Je, kweli hizo ni zipi?
1. Maisha yako yanakutegemea
kwa asilimia zote.
Ukitaka
kufanikiwa kwa viwango vikubwa, elewa kabisa kwamba maisha yako yanakutegemea
wewe kwa asilimia zote. Acha kutegemea kitu au chochote kilicho nje ya maisha
yako, wewe ndiye unayewajibika katika maisha yako kwa asilimia zote. Hata
inapotokea pengine umekosea acha kusukumia makosa hayo kwa wengine, jifunze
kutambua wewe ndiye chanzo.
Kwa
kuwa umeshajua maisha yako yanakutegemea wewe, acha kubeba visingizio
vinavyokuzuia kufanikiwa. Sahau juu ya habari ya wazazi wako eti kwamba ooh
hawakuweza kukusomesha, sahau kila kitu. Wajibu wa maisha yako, unao wewe.
Tenda kazi zako kwa nguvu zote huku ukiamini mtu pekee wa kubadilisha maisha
yako ni wewe. Huu ni ukweli ambao kamwe hupaswi kuusahau kwenye maisha ya
mafanikio.
Wewe ni mshindi. |
2. Mawazo yako ni kila kitu.
Mawazo
uliyonayo ndiyo yanayaoamua maisha yako yawe vipi. Upo hapo kimaisha ni kwa
sababu ya mawazo ambayo ulikuwa nayo siku za nyuma. Kwa hiyo, sisi ni matokeo
ya fikra au mawazo tuliyonayo. Mawazo yetu ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio
kitu kingine. Hivyo kwa kujua hili ni muhimu sana kuwa makini na kile
unachokiwaza kwa sababu utakivuna, haijalishi kiwe kibaya au kizuri.
Kila
siku jifunze kufikiri mawazo chanya. Fikiria yale mambo ambayo unataka
yakutokee. Acha kufikiria yale usiyataka utayapata. Mawazo yako
hayatakudanganya, utavuna kile unachofikiria. Kumbuka kama nilivyoanza kwa
kusema, upo hivyo kwa sababu ya mawazo uliyonayo. Kwa kulijua hili, itakusaidia
kuwa makini na kile unachokiwaza.
3.
Una uwezo mkubwa wa kupata chochote, ukiamua.
Kweli
nyingine ambayo hutakiwi kuisahau katika maisha yako ni kwamba, una uwezo wa
kupata chochote ikiwa utaamua. Kama utaamua kuwa na mafanikio makubwa,
utayapata. Kama utaamua kuwa mwanamziki, mwandishi au kitu kingine chochote,
unauwezo wa kukipata pia. Kitu cha msingi ili kukipata hicho unachokitaka ni
lazima ujitoe kwanza.
Hakuna
ajali kwenye mafanikio. Upo hivyo pia kwa sababu ya maamuzi yako uliyoyafanya.
Kama kuna kitu chochote unachokitaka, fanya maamuzi na kisha chukua hatua. Uwezo wa kufanikisha
chochote katika maisha yako, unao.
4.
Una nguvu kubwa zilizo ndani yako.
Fanya
kazi kwa ubora na juhudi zako zote huku ukiamini nguvu kubwa ambazo unazo ndani
yako. Unao uwezo mkubwa wa kufanikisha jambo lolote ulio ndani yako. Lakini kwa
bahati wengi wetu ni watu wa kutumia nguvu zilizo chini ya viwango vyetu. Ukijua
uwezo ulionao na ukaamua kuutumia, utafanikiwa sana. Huu ni moja ya ukweli
unaotakiwa kuujua kuhusu mafanikio na kukubali kutumia.
Utafika
kwenye mafanikio makubwa ikiwa utaamua kuzitumia kweli hizo, kukusaidia
kufanikiwa.
Tunakutakia
siku njema na endelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila
siku.
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.