google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 25, 2016

Tabia Tatu (3) Muhimu Unazotakiwa Kuziendeleza, Ili Kufanikiwa.

No comments :
Mafanikio ni matokeo ya tabia nzuri ambazo unaziendeleza katika maisha yako karibu kila siku. Tabia hizi chanya ama unazoziendeleza na kuzifanya kuwa zako,  ndizo zinazokupa mafanikio. Hivyo, kwa mtu yeyote anayesaka mafanikio ni lazima kwake kuendeleza tabia bora za kimafanikio ili kufanikiwa.
Watu wenye mafanikio wanatambua ukweli huu kuwa mafanikio ni tabia. Na kutokana na kuujua ukweli huu unaowapa mafanikio, huamua kufanyia kazi ukweli huu karibu kila siku. Lakini kwa kusoma makala haya, utajua tabia tatu muhimu unazotakiwa kuziendeleza ili kufanikiwa. Ni tabia ambazo watu wenye mafanikio huzitumia pia kufanikiwa.
1. Tabia ya utendaji.
Haijalishi una mipango au malengo mazuri vipi, kama hakuna utendaji hiyo itakuwa ni sawa na kazi bure. Kuwa mtendaji wa jambo ulilolipanga, ni njia mojawapo bora ya kukupeleka kwenye mafanikio. Mara nyingi wengi huwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kuwa waongeaji sana kwenye mambo yao.
Mbinu nzuri ya kufanikiwa kwenye mambo yako ni kujifunnza kuwa mtendaji. Wakati wengine wanapiga mdomo kwamba watafanya jambo hili kesho au mwezi ujao, wewe tafuta namna ya kulifanya hata kwa kidogo. Watu wote wenye mafanikio ni watendaji. Ukijifunza kuiendeleza tabia hii, uwe na uhakika utafanikiwa.


2. Tabia ya kuanza na kidogo ulichonacho.
Mbali na kuwa mtendaji pia, unatakiwa kujifunza kuanza na kile kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu kikamilike, anza na kile ulichonacho. Hata kama kitu hicho unakiona ni kidogo anza nacho hicho, baada ya muda fulani kitakuwa kikubwa. Jambo la kuzingatia hapa unapoaza na kidogo ni kuhakikisha unanidhamu ya kutosha na kukitunza.
Kwa mfano inawezekana ukawa unataka kuanza biashara ya mtaji wa milioni tano na wewe una milioni moja mkononi, acha kusubiri sana. Unaweza ukaanza na pesa yako hiyo kwa kufanya biashara ndogo ndogo na ukajikuta unakuza mtaji wako hadi pale unapotaka kufika. Kuanza na kidogo ulichonacho ni mbinu mojawapo nzuri ya kukufanikisha.
3. Tabia ya uzingativu.
Ili uweze kufanikiwa ni muhimu sana kuweka nguvu za uzingativu kwa kile unachofanya. Kama nguvu zako utakuwa unazipeleka na kuamua kuzingatia kila jambo ni wazi hutaweza kufanikiwa. Siri ya mafanikio yako ipo kwenye kuzingatia mambo machache, ikiwezekana jambo moja  lenye kukupa mafanikio makubwa.
Katika maisha yako, unaweza ukajikuta upo kwenye wakati mgumu pengine hufanikiwi kwa sababu ya kukosa uzingativu. Wengi huwa wanajikuta hawafanikiwi kwenye maisha kwa sababu hii. Utakuta ni watu wa kujaribu kutaka karibu kila kitu, matokeo yake kunakuwa hakuna kitu kikubwa walichokifanikisha.
Kwa kumalizia makala haya, nifupishe kwa kusema hivi, tabia ya utendaji, kuanza na kidogo ulichonacho na uzingativu ni moja ya tabia muhimu ambazo unatakiwa kuzizingatia kila wakati ili uweze kufanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio yako na endelea kuweka nguvu katika kujifunza kupia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.