May 13, 2016
Usiruhusu Magumu, Kukuzuia Kufanikiwa.
Ni
vigumu sana kusikia kile ambacho wengine wanakukosoa ikiwa kweli umejitoa
kufanya kazi kwa bidii zote bila kuangalia mtu. Kukosoa huko hakutasaidia kitu,
kwa sababu utajali na kuangalia matokeo yako yaliyo mbele yako.
Ni
vigumu sana kujenga tabia ya kuamka asubuhi na mapema ikiwa unachelewa kila
wakati kulala na kulala kidogo. Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuamka asubuhi
hutaweza kama umejijengea tabia hii.
Ni
vigumu kutabasamu na kufurahia maisha yako ikiwa ndani mwako tayari
umejitengenezea huzuni ya kutosha.
Ni
vigumu pia kufikia mafanikio makubwa ikiwa ndani yako, unaona huwezi kufikia
mafanikio hayo.
Ni
vigumu kuwaongoza wengine kama hata wewe mwenyewe unashindwa kujiongoza.
Ng'ang'ania mafanikio. |
Ni
vigumu kuwa king’ang’anizi na nidhamu ya kufikia mafanikio makubwa ikiwa kile
unachokifanya hakikupi matokeo unayoyataka.
Sio
rahisi pia kuanza upya kwa haraka kwenye jambo ulilokuwa ukilifanya ikiwa
umeanguka, hiyo itakuwa ni ngumu kidogo.
Ni
vigumu kwenda mbele zaidi ikiwa ndani yako unaona umefika mbali kimafanikio.
Kwa
kawaida njia ya mafanikio ina mambo na vizuizi vingi sana ambavyo kila mtu anatakiwa
kukabiliana navyo ili kushinda. Hakuna urahisi katika kutafuta mafanikio.
Wenyewe wanakwambia ‘No easy road’.
Magumu
yanajitokeza wakati unatafuta mafanikio yapo na hayakwepeki. Hakuna ujanja wa
kuyakwepa , jambo la muhimu ni kukabiliana nayo mpaka kuyashinda.
Acha
kuogopa kukosea, kumbuka bila kukosea huwezi kufanikiwa sana na kufika mbali
kimafanikio.
Kwa
chochote unachofanya hata kama kuna magumu vipi hakikisha unasonga mbele. Acha
kutoa visingizio havitakusaidia kitu zaidi, vitakukwamisha. Usiruhusu magumu
yakakuzuia kufanikiwa hata kidogo. Chukua hatua na utabadili maisha yako.
Nakutakia
siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;0713 04 80 35,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.