May 9, 2016
Kama Unafanyia Kazi Mambo Haya Kila Wakati, Hakuna Wa Kukuzuia Kufanikiwa.
Ili
kupata mafanikio siku zote unahitaji kuwa makini sana na kuzingatia mambo
yanayoleta mafanikio. Bila kuwa makini na mambo hayo, suala la kupata mafanikio
kwako linaweza likawa ni ndoto au hadithi kabisa, tena hadithi isiyo na mwisho. Wengi
kwa kutokujua wanashindwa kupata mafanikio kwa sababu ya kuupuza au kushindwa
kufanyia kazi mambo yanayosababisha mafanikio kutokea kwao.
Naamini
kama wewe ni msomaji wa dira ya mafanikio umekuwa ukijifunza mbinu nyingi kila
wakati za kukusaidia kufanikiwa. Katika makala yetu ya leo, tutakwenda
kukumbushana mbinu au mambo muhimu ambayo unatakiwa kuyafanyia kazi kila wakati
ili kufanikiwa. Ni mambo ambayo wengi wanayajua, lakini wamekuwa wakiyapuuza
pengine kwa kutokujua. Bila kukupotezea muda, fuatana nami katika makala haya
tujifunze pamoja.
1. Kujiwekea vipaumbele.
Haijalishi
una malengo na mipango mizuri vipi. Kitu cha msingi ili uweze kutimiza malengo yako ni kwa wewe kuwa na vipaumbele ambavyo umejiwekea ili kutumiza malengo uliyojiwekea. Ni lazima na muhimu sana kujua mambo ambayo unatakiwa kuyapa vipaumbele.
Si kila jambo una uwezo wa kulifanya kwa uzito ule ule. Usipoweka vipaumbele ni rahisi kushindwa ama naweza
kusema hutaweza kufanikiwa kabisa.
Ikiwa
hujanielewa vizuri hapa kwenye kujiwekea vipaumbele ngoja nikupe mfano. Tuchukulie
una malengo ya aina tatu yaani unataka kufungua duka, kufuga kuku na wakati
huohuo unataka kulima vitunguu kwa sababu umesikia kuna sehemu vinalipa sana.
Sasa kwa malengo yako hayo yote matatu ili yaweze kutimia na kutekelezeka kwa
uhakika ni lazima uchague lengo moja tu utakalo toa nguvu zako zote hadi
kulifanikisha.
Tatizo
la baadhi ya watu iwe kwa kujua au kijifanya wajuaji huwa wanataka
kukamilisha mambo mengi sana kwa pamoja, kitu
ambacho baadae huwashinda tena. Jiulize una vipaumbele vipi ambavyo
unataka kuvitimiza. Usipoweka vipaumbele na ukajifanya una tamaa, Ooooh! utaishia
kugusa gusa mambo na hakuna makubwa utakayofanikisha. Kama unataka kufanikiwa
tambua unatakiwa kuweka vipaumbele na si vinginevyo.
Jiwekee vipaumbele kila wakati. |
2. Kufanya maboresho.
Kila
kitu katika hii dunia kina badilika tena kwa kasi sana. Hata wewe hapo ulipo
kuna mabadiliko yanayotokea ndani yako ya kimwili na akili uwe unataka au
hutaki. Kwa kuwa dunia ina badilika
hivyo unalazimika na wewe kubadilika vivyo hivyo. Kama upo kwenye dunia
hii ya mabadiliko na hutaki kubadilika kitu kimojawapo kitakachokukuta ni
lazima utaachwa nyuma sana. Kwa kifupi utashangaa hufanikiwi na kushuhudia
wengine wakifanikiwa tena kwa kasi.
Sasa
kitu unachotakiwa kufanya ili uendane na madiliko kasi ya dunia ili usije
ukadumaa na kuachwa kimafanikio ni lazima kila wakati kufanya maboresho kwenye
maisha yako. Ni lazima kuboresha kila eneo lililo la muhimu sana kwako katika
maisha yako. Yapo maeneo mengi ambayo ni lazima kuyafanyia maboresho kama kuwa na mahusiano bora na wengine, afya, kujisomea mambo ya mafanikio na mengineyo mengi
ambayo yana msaada kwetu mkubwa.
Kumbuka
bila kuwa na lengo la kuwa bora kila siku kufanikiwa itakuwa ni ngumu sana. Je,
unataka kujua hiyo yote inatokana na nini? Ni kwa sababu utakuwa unaishi
kimazoesa sana na kusahau kwamba mabadiliko na kuboresha maisha yako kila siku
kuna hitajika. Kama unataka kuboresha eneo la afya fanya hivyo kila siku kwa
kufuata kanuni za afya. Kama unataka kuwa na mafanikio jifunze kila siku mafanikio
kupitia vitabu au semina. Ukifanya mabadiliko au ‘improvement’ kila siku,
mafanikio utayapata.
3. Kuweka kumbukumbu.
Kwa
chohote unachokifanya kiwekee kumbukumbu. Kama kuna jambo unataka kulifanya
kesho au wiki lijalo weka kumbukumbu. Unapoweka kumbukumbu inakusaidia sana
kuiamsha akili yako kulazimisha utekelezaji kuliko ungeacha hivi hivi. Hili ni
moja kati ya jambo rahisi ambalo wengi hawalifanyi lakini katika maisha ya
malengo ni muhimu sana. Najua kwa wale wanaofanya hivi wananielewa kitu ambacho
ninakisema hapa kwa vizuri sana.
Siku
zote malengo au kitu ambacho hakipo kwenye maandishi huwa hakina maana sana.
kwa hiyo, ili uweze kufanikiwa na kujihakikishia ushindi wa malengo yako. Anza
kujiwekea kumbukumbu kila siku kwa unachokifanya au unataka kukifanya. Na kila
inapofika jioni jikumbushie kwa kupitia kijitabu chako cha kumbukumbu. Kwa
jinsi utakavyoendelea hivyo, utajikuta ukibadilisha maisha yako kwa sehemu kubwa
sana, hiyo nikiwa na maana utaishi kitaalamu na kisomi zaidi.
Kama
utazingatia mambo hayo matatu na kuyafanyia kazi kama nilivyotangulia kusema
hapo awali uwe na uhakika utafanikiwa na hakutakuwa na mtu wa kukuzia.
Tunakutakia
siku njema na ansante sana kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya
kujifunza.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.