May 11, 2016
Siri 7 Za Kuwa Mfanyabiashara Mkubwa.
Inawezekana kila wakati umekuwa ukijiuliza ni kwa jinsi gani
utaweza kutoka katika hali ya kufanya biashara ndogondogo au biashara ya kati hadi kuwa mfanyabiashara mkubwa. Leo katika Makala haya nitakwenda kukueleza bayana
siri ambazo kama utaamua kuzitumia utaweza kuwa mfanyabishara wa mkubwa.
Ni lazima ujue kuwa mfanyabiashara ni lazima kuwa na imani. Imani ambayo ninazungumzia hapa ni kuamini sasa kitu ambacho hakipo. Huenda ukawa hujanielewa, tulia ili nikueleweshe ukweli ni kwamba ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa ni lazima uamini kwamba kitu hicho kitakuwa kweli, kwa hapo baadae. Kuna usemi unasema ya kwamba imani ni bora kuliko matendo, maana yake amini kwanza.
Kuwa na imani thabiti ambazo zitakufanya ujipe moyo wa ushindi na wenye mawazo chanya ya ushindi juu ya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Endapo utakuwa na imani nusunusu ni lazima utashindwa kutimiza jambo lako. Kanuni ya biashara inasema ya kwamba kama unahitaji Mafanikio makubwa matokeo yake huwa hayaonekani mapema na madhara yake huwa hayaonekani mapema pia. Huo ndio ukweli lazima ujiulize nikifanya jambo hili na nisipofanya matokeo yake ni nini?

Ukijiuliza maswali
haya lazima uyapatie majibu ya kina yenye kuleta majibu sahihi. Kama
nilivyosema hapo awali ya kwamba kuwa mfanyabiahara mkubwa ni Kuwa na imani,
hivyo ni vyema ikumbukwe ya kwamba kuwa mfanyabiashara wa mkubwa usitegemee mwanzoni mwa biashara yako kutengeneza faida, ila jiandae kupokea
hasara ambazo ndizo changamoto zenye kukuletea mafanikio makubwa mbeleni. Unawezaje sasa kuwa mfanyabiashara mkubwa?
Zifuatazo Ndizo Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa.
1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Zifuatazo Ndizo Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa.
1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la
kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi
nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia
kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni
lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa
mnunuzi na muuzaji?au je unataka kuwa
msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.
Fanya utafiti wa soko. |
2. Fanya
uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la
tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri
juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya
washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua
washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia
kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi
kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.
3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa
kukuongoza na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa
wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika
kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari
wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika
kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai
wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua
mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.
4. Tambua biashara inayokua.
4. Tambua biashara inayokua.
Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya
tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda
miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi
gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa
kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara
inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo
kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima
tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au
bidhaa.
5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na
juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako
uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na
lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara
yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa
baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.
6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.

7. Jenga
mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.
Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni
baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa.
Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.
Mwandishi; Benson Chonya.
Email; bensonchonya23@gmail.com
Simu; 0757-909942
Mwandishi; Benson Chonya.
Email; bensonchonya23@gmail.com
Simu; 0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.