May 2, 2016
Mambo Matatu Ya Kufanya Pale Unapohisi Umefanya Makosa Kwa Kile Unachokifanya.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kukosea. Na hakuna ambaye amewahi
kufanikiwa bila kukosea. Siku zote
mafanikio yanakuja kutokana na makosa madogo madaogo yanayojitokeza iwe tunayataka
au hatuyataki. Makosa haya ndio hutujengea uwezo wa kutusaidia kufikia kwenye
mafanikio makubwa. Kama kuna sehemu umekosea, huna haja ya kulaumu, zaidi
jifunze kutokana na makosa yako na kisha songa mbele.
Kwa
hiyo kama makosa ni muhimu kutufikisha kwenye mafanikio? Kwa nini ulie,
uhuzunike au kusonononeka sana kutokana na makosa yako? Kama ndicho umekuwa
ukikifanya amka kutoka usingizini si wakati wa kukatishwa tamaa na makosa yako.
Kitu cha ziada unachotakiwa kufanya ni kuyatumia makosa haya kukusaidia
kufanikiwa. Kivipi? Twende pamoja kujifunza nini cha kufanya pale unapokosea.
1. Yaone makosa hayo kama ngazi ya
mafanikio.
Kama
umefanya kosa, usije ukafanya kosa tena lingine kwa kuruhusu makosa yako
yakakukatisha tamaa. Ikiwa utaruhusu makosa ya kukatishe tamaa naweza sema kwa
lugha rahisi huo ndio utakuwa mwisho wako. Siku zote, jaribu kuyaona makosa
yako kama ngazi ya kukusaidia kufanikiwa. Unapokosea kitu, jifunze na kisha
endelea mbele. Kama utayaona makosa kwako ni ngazi ya kukusaidia, ni wazi pia
utafanikiwa kweli.
Jifunze kutokana na makosa yako. |
2. Kubali kwamba umekosea.
Mara
nyingi kwa wengi huwa sio rahisi kukubali eti kwamba wamekosea. Sasa ili uweze
kufanikiwa inatakiwa uwe mwepesi wa kukubali kwamba chanzo cha makosa yote hayo
kimetokana na wewe, hata kama sio. Kwa kukubali hivyo hiyo itakusaidia sana
kuweza kujirekebisha na kuchukua hatua nyingine za kukusaidia kufanikiwa. Wengi
wanaokubali makosa yao mapema na kukubali kujifunza siku zote huwa ni watu wa
kufanikiwa.
3. Usikubali tena kurudia makosa hayo.
Jambo
lingine la kufanya mbali na hayo mawili tuliyojifunza hasa pale unapokosea,
usikubali tena kurudia kosa hilo. Kama usipokubali kurudia makosa yako
itakusaidia sana kufanikiwa. Kitendo cha kurudia makosa yale yale siku hadi ni
dalili nzuri mojawapo inayoweza kutuonyesha kwamba huwezi kufanikiwa. Muda wote
kuwa makini sana, usirudie makosa ambayo umeshawahi kuyafanya kipindi cha
nyuma. Ikiwa utarudia utakwama sana.
Kwa
kujua na kuyanyia kazi mambo hayo matatu, yatakusaidia kuyatumia makosa yako
vizuri na hatimaye kuweza kufanikiwa.
Tunakutakia
mafanikio mema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu;-
0713 048035,
Email;-
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.