May 31, 2016
Misingi Mitano (5) Unayotakiwa Kuifahamu, Ili Kujihakikishia Kipato Cha Kudumu.
Kati
ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi katika hii dunia ni pesa. pesa hiyo
imeanza kutafutwa toka enzi za mababu na mababu mpaka leo. Juhudi za kutafuta
pesa hadi kuipata zimekuwa ni kubwa sana kila kukicha. Kutokana na matokeo ya
juhudi hizo, hiyo yote imekuwa ikitudhirishia au kutuonyesha kwamba kumbe pesa
ni sehemu ya maisha yetu, tena maisha ya kila siku.
Lakini
pamoja na juhudi kubwa za kuitafuta pesa hiyo bado lipo kundi kubwa la watu
ambao wamejikuta wakiikosa pesa hiyo. Harakati zote za kuamka asubuhi na mapema
na hata kuchelewa kulala kwa sababu ya pesa zimekuwa ni kama kazi bure kwa
sababu hawaipati. Watu hawa wamekuwa wakipishana na pesa karibu kila siku,utafikiri
wao wanalaana na pesa hiyo hadi washindwe kuipata.
Hebu
jaribu kuangalia kwenye eneo unaloishi jinsi pilika pilika za kutafuta pesa
zilivyo nyingi. Lakini cha kushangaza pamoja na juhudi na pilika pilika hizo
bado ni wachache wanaoipata pesa na kuwahakikishia kipato cha kudumu. Wengi
wamekuwa wakitafuta sana pesa na kuishia maumivu na mateso ya kutokuipata. Sina
shaka hali hii unaijua vizuri ya wengi kuendelea kukosa pesa ingawa wanaitafuta
sana.
Kutokana
na mazingira haya wapo ambao huanza kuamini wamelogwa. Na wengine pia huanza
kuamini wana mikosi au laana. Je, kitu cha kujiuliza hizo ndizo huwa sababu
halisi za wao kukosa pesa? Ukifatilia kimsingi, hizo sio sababu halisi za wao
kukosa pesa, bali sababu hizo hutumika kama kisingizio. Watu hao kitu
wasichokijua mara nyingi hushindwa kuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya
kukosa misingi ya kuwaongoza.
Ndio.
Naona unashangaa, inawezekana hata wewe ukawa kwenye wimbi la kutokuwa na
kipato cha kudumu kwa sabau ya kukosa misingi ya kukuwezesha kuwa na kipato
hicho. Kama unafikiria natania, kwa nini huna kipato cha uhakika na kudumu
mpaka sasa? Nafikiri sasa, utakubaliana nami kwa kile ninachosema. Je, unajua
misingi hiyo ni ipi unayotakiwa kuwa nyo ili kujihakikishia kipato cha kudumu?
1.
Bajeti.
Hatua
ya kwanza itayokuhakikishia wewe uwe na kupata cha kudumu ni kujijengea
utaratibu wa kuwa na bajeti yako. Bajeti hiyo itakuongoza kujua pesa yako
inatoka wapi na pesa yako inaenda wapi. Lakini
si hivyo tu, unapokuwa na bajeti inakusaidia pia kujua ni lini na wapi
uweze kuwekeza pesa yako. Hivyo ni njia mojawapo muhimu sana ya kukuhakishia
kipato cha kudumu kwenye biashara na maisha yako kwa ujumla.
Pesa unayopata hata kama ni kidogo, wekeza. |
2.
Kuwekeza.
Njia
nyingine bora ya kukupa kipato cha kudumu ni kuifanya pesa yako ikuzalishie.
Hakuna namna nyingine ya kuweza kuifanya pesa yako ikuzalishie zaidi ya kuweza.
Kama una kitega uchumi kimoja, ongeza na kingine cha pili, cha tatu na
kuendelea. Watu wenye mafanikio wana vipato vya kudumu kwa sababu wamewekeza
katika maeneo mengi. Halikadhlika, nawe unatakiwa kufanya hivyo ili kuwa na kipato
cha kudumu.
3.
Kuweka akiba.
Kati
ya kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni
kujiwekea akiba. Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata, jifunze kuweka
akiba. Akiba hiyo itakusaidia katika kuwekeza kwenye miradi mingine mingi baadae,
lakini si hivyo tu pia ni njia mojawapo ya kukutengenezea kipato cha kudumu.
Kama inatokea umeishiwa ni rahisi kuweza kuchukua pesa kwenye akiba yako kuliko
kukopa kopa hovyo.
4.
Kulipa madeni mapema.
Ni
vyema ukajua mapema ili kujiweka salama katika safari yako ya mafanikio,
jifunze kulipa madeni mapema. Unapokuwa unalipa madeni mapema inakusaidia sana
kutokukuvurugia mambo yako mengi. Kama una mkopo benk au sehemu nyingine, lipa
mapema ili uanze kuwa huru kutafuta pesa zako mwenyewe ambazo zitakupa uhuru
mkubwa wa kimafanikio. Kama unadaiwa
kila wakati si rahisi sana kuendelea na kuwa na kipato cha uhakika.
5.
Kuwa mjasiriamali mpambanaji.
Hautaweza
kuwa huru kipesa na kujijengea kipato cha kudumu, kama leo hii hutaweza kuamua
kuwa mjasiriamali mpambanaji. Amua kuwa mjasiriamali mpambanji unayetaka kutengeneza
matokeo na sio mjasiriamali wa kulalamika kila siku. Hakuna mafanikio
yanayoweza kuja au kupatikaa kwa kulalamika. Kama kuna changamoto zitatue na utafika
mbali kimafanikio kipesa.
Kabla
ya kuweka kalamu yangu chini, naomba utambue kwamba kama hutojiwekea misingi
hiyo imara ya kipesa, suala la kupata pesa na kuwa na kipato cha kudumu
litakusumbua sana. Usishangae ukawa mtu wa kufukuza pesa siku zote za maisha
yako bila mafanikio. Zingatia hili sana na chukua hatua.
Ansante
kwa kunifatilia na pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia mtandao
wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.