May 26, 2016
Tunaposhindwa Kulinda Tunachokipenda Huvuna Maumivu.
Wazazi
wana nafasi gani kwenye kutuamulia maisha yetu ya uhusiano? Jibu la swali hilo
linategemea mambo mengi. Mojawapo ya mambo hayo ni malezi yetu, na namna
tulivyopata nafasi ya kukua kiufahamu nje ya malezi. Lakini ukweli ni kwamba,
wazazi wana nafasi ya ushauri tu, kuhusu maisha yetu ya uhusiano. Lakini kwa
bahati mbaya, wazazi wengi hujipa nafasi kubwa na mamlaka zaidi na watoto wengi
huwaruhusu wazazi wao kuchukua nafasi hiyo.
Hebu
tuchukulie kwa mfano mzazi ambaye anamkatalia mtoto wake wa kiume asimuoe binti
aliye nyumba ya tatu kwa sababu ya kuona tu binti yule ni mfanyakazi wa ndani. Kwa
tafsiri ya haraka haraka mzazi huyu anakuwa amemwona binti yule kama nusu mtu
na asiyefaa kitu. Naye mtoto wa kiume pengine kwa kusikiliza ushauri wa mzazi
anaweza kukubali lakini baadae inaweza ikawa majuto kwake ikiwa ataoa mwanamke
ambaye atamtesa ingawa kiuhalisia anakuwa ametoka familia tajiri.
Lakini
pia huwa inatokea sana kwa wazazi wanapoona mtoto wao awe wa kike au kiume
akiwa amependana na mtu ‘choka mbaya
kimaisha’ kwa wengi huwa sio rahisi kukubali mahusiano hayo na kujikuta
kuweka vizuizi vingi sana kwa watoto ili wasiweze kuoana. Hapa watoto wasipokuwa
makini hujikuta wamekubali walichoelezwa na wazazi wao na matokeo yake hujikuta
kwa pande zote mbili kujuta kutokana na kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo
sahihi.
Linda unachokipenda, kisipotee. |
Hali
kama hizi zipo sana katika jamii zetu. Kuna wengi ambao ndoa zao zinaingiliwa
sana na wazazi au hata ndugu zetu na pengine tu hata marafiki zetu na kujikuta
hata kukosa uhuru. Hali kama hii inapokutokea na ukajikuta umekosa uhuru wa
kuonyesha ukakamavu wa kuonyesha kile unachotaka kwenye mahusiano au ndoa yako
utaumia sana. Utahisi dunia sio sehemu salama kwako kwa sababu ya kuhisi kama
ndugu wanakuonea kila wakati. Kama hili limewahi kukutokea pole sana.
Naamini
umeshawahi kusikia mikasa kama hii ya kuingiliwa kwenye mahusiano. Wengi wetu
mara nyingi tunafundishwa namna ya kuishi na wake au waume zetu, kama tuendelee
kuwa nao au tuwaache. Huwa tunawasikiliza wazazi, ndugu au marafiki na kuvunja
uhusiano. Baadaye, kwa maumivu makubwa tunakuja kubaini makosa tuliyoyafanya. Tunajaribu
kuunga palipokatika. Huwa inawezekana, ingawa mara nyingi haiwezekani tena.
Unaweza
ukasambaratishwa kwenye mahusiano au ndoa yako na ndugu zako pasipo kujua na
matokeo yake kuleta majuto makubwa sana. Na majuto hayo unaweza ukaendelea
kuamini pengine ungedumu kwenye uhusiano wako wa mwanzo ungekuwa upo salama
kimafanikio na kindoa pia. Lakini ulipo ‘moto’
umewaka kutokana na kwamba upo sehemu ambayo siyo sahihi. Ni kitu ambacho
kina uwezo wa kukuuma sana siku zote na ukajikuta umeharibu kila kitu ikiwa
pamoja na mafanikio sababu ya uhusiano.
Kumbuka
kwamba, wewe ndiye unayetakiwa kusema na kuamini kwamba, umempenda fulani. Wewe
ndiye unayetakiwa kulinda uhusiano wako kwa msimamo wa hali ya juu. Wengine wanakuwa
wana uhuru wa kutoa maoni kuhusu penzi au mpenzi wako, lakini hawana ruhusa au
nafasi ya kuamua kuhusu hatma ya penzi lako. Ikiwa kwa namna moja au nyingine
utashindwa kulinda kikamilifu kile unachokipenda, elewa utavuna maumivu tena
makubwa sana.
Tunakutakia
mafanikio mema katika ndoa na maisha. Pia endelea kujifunza kupitia mtandao
wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.