May 12, 2016
Njia Huru Za Kimafanikio.
Miongoni
mwa kauli ambazo nilikuwa nasikia wakati nakua nilikuwa nasikia wanasema maisha
ni kama kioo ukicheka na yenyewe yanacheka. Kwa kipindi hicho sikuwahi kujua
wanamaana gani watu waliyokuwa wanasema hivyo. Ila kwa bahati nzuri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyoelewa walikuwa wanamaanisha nini.
Kwa utafiti wangu
nimegundua ya kwamba katika maisha ya kusaka mafanikio ni lazima ujishughulishe
kwa kutumia nguvu, kipaji, juhudi na maarifa ili uweze kupata mafanikio hayo.
Na endapo utafanya kinyume chache utazidi kulaumu na kuishia kusema ndoto zangu
ni kuwa mtu fulani na vitu kama hivyo.
Mwandishi mmoja
anayeitwa Charles Nduku aliwahi kuandika katika kitabu chake cha ‘my plan, my life’ kwa kusema acha Kuota
ndoto bali anza kufanya.
Kwa kipindi kirefu umekuwa unasema nataka kuwa hivi na vile. Kumbuka ya kwamba huu sio mda wa kusema maneno hayo. Ila muda wakuanza kutekeleza malengo yako. Watu wengi wapo vizuri zaidi kwa kusema kuliko kutenda, na ukichunguza vizuri watu hao hufa na ndoto zao. Badili mtazamo wako na kuwa ni mtu wa vitendo dhidi ya maneno.

Utaweza kubadili
mtazamo wako na kuwa mtu wa vitendo ikiwa lakini utajifunza kutumia njia huru
za kimafanikio. Kwa kusoma makala haya utajifunza njia hizo huru za mafanikio
ambazo zitakufanya ufanikiwe. Naamini una hamu ya kutaka kuelewa ni njia zipi
huru za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia. Karibu na twende pamoja kujifunza
njia hizo.
1. Tafuta nafasi.
1. Tafuta nafasi.
Kwa kile
ambacho unataka kuwa tafuta nafasi ya kutenda jambo hilo. Watu wengi kama
niliposema hapo awali ni wazuri wa kusema kuliko kutenda. Kwa mfano kuna watu
wanasema nataka kuwa muigizaji utamsikia akisema tu nataka kuwa muigizaji ila
hatafuti nafasi ya kuwa muigizaji. Halikadharika hata wewe mwenye kitu cha
tofauti, fanya kitu hicho na usiishie kusema tu haitakusaidia. Endapo utaishia
kusema tu jiandae kufa na malengo yako.
Katika kutafuta nafasi ni lazima ujiulize nafasi hiyo ninayo au sina , kama sina naipata wapi? Ni nini kitu ambacho kinahitajika katika nafasi hiyo ninacho au sina kama sina nina kipata wapi? Ukipata majibu ya maswali hayo lazima uweze kufanikiwa.

Tengeneza nafasi. |
2. Tengeneza jina.
Katika jambo ambalo unalifanya ni lazima utengeneze jina ambalo watu wataweza kukufahamu kwa kile ambacho unakifanya. Utengezaji wa jina hutokana na kutengeneza huduma bora kwa watu wengine. Kwa mfano kuna siku nilikuwa katika harakati zangu za hapa na pale nikawa akapita mtoto mdogo ni kamuuliza yule mtoto et nitapata wapi chipsi mtoto yule akanijibu nenda kwa mpemba, wakati najiuliza ni kitu gani kinamfanya huyo mpemba mpaka watoto wadogo wamfahamu, nilipofika hapo kwa huyo mpemba ndipo nilipopata jibu. Ya kuwa ubora na usafi wake ndio uliomfanya atengeneze jina. Jina hilo ndilo linalomtengenezea wataja wengi.
Nadhani pia utakuwa unawafahamu watu wenye majina makubwa ambao wanazalisha vitu vyenye ubora kwa hapa nchini. Kama ndivyo hivyo ni wakati wako na wewe kuweza kutengeneza jina kwa jambo ambalo unalifanya. Ifike wakati mtu akitaka kitu fulani hata ukimuuliza mtu yeyote hata awe mtoto mdogo awe anakufahamu kutoka na kile unachokifanya. Kama ilivyo leo kwa watu wengi maarufu unaowafahamu..

Ukiyafanya
hayo hapo ndipo pesa zitapokuja kwa kasi zaidi. Mbinu hizo huru za kimafanikio
wengi waliofanikwa ndizo ambazo walizozitumia. Zitumie leo uwe tajiri mkubwa.
Mwandishi: Afisa Mipango Benson chonya .

Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.