Oct 4, 2016
Siri Kubwa Ya Mafanikio Yako Ndio Hii.
Maisha ni muunganiko wa mambo mengi
sana, yapo yale mambo ambayo hujenga na ambayo hayajengi. Mambo hayo ya
kukujenga wewe katika ulimwengu huu yapo machache sana, lakini mambo ambayo hayakujengi
haya yapo mengi sana.
Kwa kutokujua hili na hapo ndipo
ambapo wengi huangukia. Na katika mambo hayo ni yale ambayo ni ya kukutatisha
tamaa mara zote. Lakini kwa kuwa wewe ni mpiginaji wa kimaisha siku ya leo
nataka nikwambie ya kwamba siri kubwa ya mafanikio yako ni ipo kwenye kubadili
ratiba ya utendaji wako wa kazi.
Siri kubwa ya kuweza kufanikiwa ni
kuweza kubadili namna ya utendaji kazi wako. Unashindwa kufanikiwa kwa kiwango
cha juu kwa sababu umeshazoea kuishi kimazoea. Watu wengi tumelelewa katika
maisha ya kimazoea.
Tunaishi maisha yaleyale ambayo tumekwisha yazoea kiasi kwamba hatuwezi
kufanya vitu vingine, lakini kama ambavyo nimezoea kusema ya kwamba maisha
hubadilika yenyewe kama endapo utaamua leo kubadili namna ya utendaji kazi
wako.
Badili utendaji wako wa kazi. |
Kunielewa vizuri katika hili
ninalosema nitakupa kisa ambacho kilimkuta rafiki yangu wa karibu sana.
Yupo rafiki yangu mmoja
alinipigia simu siku moja na kuniambia ya kwanza biashara yake imekuwa
ngumu sana, na kila malengo ambayo hupanga huwa hafikii, hivyo alipenda
nimshauri jinsi ya kuweza kufikia malengo yake.
Nikaamuliza huwa unafungua na kufunga
biashara yako saa ngapi? ndipo akanijibu ya kwamba huwa anafungua saa mbili
asubuhi na kufunga biashara yake mida ya saa mbili usiku.
Hapo ndipo nikagundua ya kwamba alishazoea
kufanya biashara kimazoea, ndipo nilipomwambia ya kwamba abadili muda wa
kufungua biashara na pia aongeze muda kufunga biashara yake.
Nikamwambia afanye tathimini kwa muda
wa miezi miwili kisha anipe majibu, baada ya miezi miwili kupita akanitafuta
tena akanipa tathimini ya kwamba ananishukuru kwani ushauri wangu umemsaidia
sana. Ndipo nikamwambia aendelee kufanya hivyo.
Nimekupa ushuhuda huu, ili uweze
kukujenga na pia uweze kutafakari juu ya utendaji wako wa kazi. Siku zote siri
kubwa ya mafanikio ya mtu binafsi upo katika kuheshimu matumizi sahihi ya muda.
Ni lazima ujue ya kwamba mtunza muda
ni wewe hivyo ni vyema ukazingatia ile kauli ambayo husema ya kwamba muda ni
mali. Pia uweze kujijengea ile tabia ya kuwa kwanza kuamka na pia mtu wa mwisho
kulala.
Hata hivyo ni vyema ukautumia vyema
muda ambao unao kuweza kufanya vitu vya msingi ambavyo vitakufanya kila siku
uweze kutimiza lile kusudio lako la kuja hapa dunia.
Fanya muunganisho wa kile ambacho
unakifamu na kukiweka katika matendo, hapa maana yangu ni kwamba kwa kila jambo
ambalo unajifunza kupitia makala mbalimbali ziweke katika matendo, kwani endapo
utafanya kinyume chake itakuwa ni bure.
Mwisho niweke nukata kwa kusema ya
kwamba hakuna mtu atakayezuia mafanikio yako usipokuwa wewe mwenyewe.
Na: Afisa mipango Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.