Sep 30, 2016
Mbinu Za Kukuza Biashara Ndogo.
Ni
ukweli usiofichika zipo changamoto nyingi sana hasa pale unapukuwa unaanzisha
biashara na kuitaka ifike mahali ikue na kujitegemea. Pamoja na changamoto
nyingi kama za masoko au ushindani pia huwa ipo changamoto nyingine ya namna ya
kukuza biashara yako.
Wafanyabiashara
wengi wadogo inakuwa inafika mahali hujikuta wako palepale miaka nenda rudi bila
kupiga hatua kubwa mbele. Hiyo yote hutokea hivyo kwa sababu wanakuwa wamekosa
maarifa ya kukuza biashara zao kwa namna moja au nyingine.
Kwa
kusoma makala haya inakusaidia kujua mbinu zitakazo kusaidia kama wewe ni
mfanyabiashara mdogo kuweza kukuza mtaji wako taratibu na kufika mahali na wewe
ukawa na biashara yako kubwa kama wengine unavyowaona.
Je,
mbinu hizo ni zipi? Fuatana nami mwanzo hadi mwisho kuweza kuzijua mbinu hizo
na kuzifanyia kazi.
1.
Jitume sana.
Inawezekana
biashara yako ikawa ni kuuza matunda. Pia inawezekana biashara yako ikawa ni ya
uchuuzi yaani kutoa badhaa eneo moja na kuzipeleka eneo lingine kuziuza.
Sasa
unapokuwa na biashara ndogo kama za namna hii, ili uweze kufanikiwa ni lazima
ufanye kazi kwa bidii sana na kujituma kwa nguvu zote bila kuchoka.
Kuwa mbunifu. |
Ikiwa
hautafanya hivyo ni lazima hautapiga hatua na biashara yako itakufa. Unajua ni
kwa nini itakufa? Ni kwa sababu katika kipindi hiki biashara yako inapokuwa
ndogo inataka uangalizi wa hali ya juu sana ili iweze kukua.
Hivyo,
utalazimika kujituma sana na kufanya kila aina ya jitahada ambazo zitapelekea
kuifanya biashara yako ikaweza kukua na kufika mahali ikajitegemea yenyewe.
2.
Kuwa mbunifu.
Mbali
na kujituma kapindi ambacho unakuwa una biashara ndogo, jitahidi uwe mbunifu.
Unapokuwa mbunifu inakusidia sana kugundua ni kitu gani ambacho wateja wako
wanataka au ni kipi ambacho hawataki. Hiyo ni njia bora sana itakayokusaidia
kuboresha pale kwenye mapungufu na itakusaidia sana pia kuweza kuikuza biashara
yako.
3.
Sikiliza malalamiko ya wateja.
Ni
vyema pia ukawa ni mtu wa busara kuweza kusikiliza kile ambacho wateja wako
wanakisema katika kipindi hiki cha kukuza biashara yako. Hiyo itakusaidia
kutimiza matakwa yao na itakupelekea kuwa na wateja wengi ambao watasaidia kuifanya biashara yako ikue.
4.
Tafuta msaada.
Katika
kipindi cha kukuza bishara yako na kuifanya iwe kubwa, acha kujaribu kuishi
kama kisiwa. Tafuta msaada wa ushauri kwa wale waliofanikiwa wakusaidie
kimawazo wao walifanya nini hadi wakafikia huko waliko sasa.
5.
Punguza utegemezi kwenye biashara yako.
Pia
unapokuwa unaikuza biashara yako acha kutegemea sana pesa unayoipata kwenye
biashara yako ndiyo iendeshee maisha yako. Jaribu kuwa na pesa nyingine,
vinginevyo bila kufanya hivyo unaweza ukaua kila kitu bila kujijua.
6.
Jifunze kukuza mtaji.
Kwa
namna yoyote ili biashara yako ikue na ikafika mahali inajitegemea unalazimika
sana kujifunza mbinu za kukuza mataji
wako. Hilo ni somo ambalo unatakiwa ulizingatie sanaa na kujiuliza kila wakati
ni nini kifanyike ili mtaji uweze kukua.
kwa
kifupi, hayo ndiyo baadhi ya mambo machache yanayoweza kukusaidia kuweza kukuza bishara yako kama
unaanzia chini.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.