google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 6, 2016

Ukweli Kuhusu Pesa Utakaokufanya Uwe Tajiri Au Maskini.

No comments :
Kwa kawaida, ili uweze kupata pesa, mbali na kanuni za pesa, upo ukweli unaotakiwa kuujua kuhusu pesa ili ufanikiwe. Kwa kuujua ukweli huu, unao uwezo wa kukufanya ukawa tajiri au kwa kushindwa kuujua ukweli huu ni rahisi pia kuwa maskini.
Ukiangalia watu wanaofanikiwa kipesa kwa namna moja au nyingine wanajua kweli nyingi kuhusu pesa. kwa upande mwingine, watu wengi wapo katika hali mbaya za kiuchumi na kukosa pesa kwa sababu ya kushindwa kuijua pesa vizuri na kweli zake jinsi zinavyofanya kazi.
Sasa ili uweze kufanikiwa kwenye eneo la pesa zipo kweli tatu ambazo unatakiwa uzijue na kuzifanyia kazi.
Kwanza, ili uweze kupata pesa ipo thamani ambayo ni lazima uweze kuitoa. Hautaweza kupata kiasi chochote cha pesa ikiwa hakuna thamani yoyote unayoitoa. Kwa hiyo kiwango cha pesa ulichonacho kipo sawasawa na thamani unayoitoa.

Toa thamani kubwa, utapata pesa.
Hebu jaribu kufikiri moja ya matajiri wakubwa dunia, ni kitu gani wanachokifanya cha ziada na ambacho kinawafanya wapate pesa? Ukichunguza utagundua ni thamani kubwa wanayotoa kwa yale wanayoyafanya kila siku.
Kwa mfano tukimuangalia kila mmoja wetu anaujua au anatumia mtandao wa ‘facebook’. Sasa, mmiliki wake ambaye ni Mark Zuckerberg ni moja ya matajiri wakubwa sana duniani akiwa kwenye orodha ya kumi bora kwa sasa. Ukiangalia ni nini kilichomfikisha hapo ni ile thamani anayoitoa kwenye biashara yake.
Kila kukicha watu wanapofurahia na kutumia ‘facebook,’ ndivyo ambavyo Mark Zuckernberg anazidi kuwa tajiri. Hiyo yote inaonyesha kwamba pesa ni ishara ya thamani fulani inayotolewa. Hivyo ili uweze kupata pesa ni lazima rafiki, uweze kutoa thamani kubwa kwa namna yoyote ile.
Kama hujanielewa vizuri ngoja nikuulize swali hili? Hivi ulishawahi kujiuliza kwa nini wale wote wanaoshinda bahati nasibu mara nyingi huishia kuwa maskini yaani zile pesa zinakuwa kama hazijawasaidia kitu? Ama wakati mwingine pesa hizo huonekana kama zina mkosi zimepotea tu kiaina?
Kama hujawahi kujiuliza hivyo usipate tabu, jibu ni rahisi tu, ni kwa sababu pesa walizopata haziendani na thamani waliyotoa, hivyo ni lazima zitapotea tu, hata kwenye mazingira ambayo hayakutegemewa. Ni ngumu sana kuweza kutunza pesa ambayo haiendani na thamani uliyotoa.
Hili pia hutokea sana kwenye zile pesa za kupewa ambazo hujafanyia kazi, nazo huisha sana kwa sababu kama hii. Kama unafikiri natania pita barabarani halafu mtu akupe shilingi laki moja uone kama utadumu nayo sana, kwa wengi huisha mapema mno.
Kwa hiyo kila unapofikiria suala la kuongeza kipato, ili uweze kufanikiwa katika hilo usianze kufikiria juu ya pesa. Fikiria ni namna gani jinsi unavyoweza kuongeza thamani kwenye maisha ya watu na yale unayoyafanya. Kwa jinsi utakavyozidi kuongeza thamani pesa itakuja tu kwako na hilo sio suala la kuuliza.
Kumbuka siku zote pesa ni ishara ya thamani. Kama hutoi thamani kubwa utapata pesa kidogo. Matokeo hayadanganyi, kanuni za mafanikio hazidanganyi, labda wewe udandanye kwa kukataa ukweli huu. Na ikiwa hautafanya hivyo kwa kutoa thamani hiyo, itakuwa ni sawa na mtu kukimbia kivuli chake.
Je, ni ukweli gani mwingine kuuhusu pesa unaotakiwa kuujua ili uwe tajiri? Fuatana nami katika mwendelezo wa makala haya kwa siku ya kesho bila kukosa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com  


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.