Feb 14, 2017
Hizi Ndizo Mbinu Zitakozokupa Mafanikio Kwa Wakati Sahihi.
Asilimia kubwa ya maisha ya watu
duniani midomo yao hutamka ya kwamba wanataka kufanikiwa. Lakini ni idadi ndogo
sana kati ya idadi kubwa ambao wanapata mafanikio hayo. Ikiwa ni pamoja ya
kwamba watu wote tunaishi katika mazingira ambayo yanafanana.
Tukiangalia wote tuna masaa 24 kwa
siku, wote tunatumia hewa safi ambayo hatulipii hata senti moja kwa ajili
ya hewa hiyo, watu wote tunaishi katika maeneo ambayo mazingira yake yana
kila aina ya rasimali ambazo kama tutaamua leo kuzitumia vyema zina uwezo wa
kubadilisha maisha yetu.
Swali linakuja sasa ni wapi ambapo
panatutofautisha kati ya watu wenye mafanikio na wasio na mafanikio? Ikiwa wote
tunaishi mazingira ya aina moja.
Kitu kikubwa ambacho kitakusaidia
kupata aina hiyo ya mafanikio au kujua ni wapi panapotutofautisha ni kujitambua.
Hapa ndipo ilipo siri ya mafanikio na ambayo unatakiwa uielewe.
Kujitambua ni sehemu ambayo kila
msaka mafanikio lazima aijue vyema. Kujitambua huwa na uhusiano
mkubwa uliopo kati ya kitu ambacho unahitaji kukifanya. Kujua ni kile
unachokitaka ndo siri ya kupata mafanikio yako.
Watu wengi kutokana na changamoto za
kimaisha wamekuwa wapo tayari kufanya jambo lolote, mfano hivi hajawahi
kukutana na mtu anakwambia yupo tayari kufanya jambo lolote?
Bila shaka umewahi kukutana na mtu
huyo, ila ukweli ni kwamba kufanya hivi ni kuchelewa katika safari yako
ya mafanikio na mafanikio. Kwani ukitaka kufanikiwa ni lazima ujue kila
unachotaka kufanya kutoka nafsini mwako.
Unaweza kujiuliza maswali haya ili
kuweza kujitambua na hatimaye kupata mafanikio yako.
1. Wewe ni nani?
2. Unataka kufanya nini?
3. Umetoka wapi?
4. Upo wapi?
5. Na unaelekea wapi?
Maswali hayo yote msingi wake wa mkuu
ni kujiuliza lengo lako la kuja duniani ni nini?
Ukipata majibu ya maswali hayo
tafadhari nakuomba uyaandike katika daftari lako na kuyachukulia hatua
mathubuti, kufanya hivyo kila wakati ni hatua za kuweza kufanikiwa.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.