Feb 24, 2017
Linda Muda Na Mafanikio Yako Kwa Kusema HAPANA.
Moja ya jambo muhimu unalotakiwa kulifanya ili
kuweza kufanikiwa ni kule kujenga uwezo
wa kusema HAPANA hasa kwa mambo ambayo hayaendani kabisa na malengo ya maisha
yako.
Wengi wetu mara nyingi ni watu wa kukubali karibu kila
kitu katika maisha yetu, hasa pale tunapoambiwa na wengine kwamba tufanye kitu cha
aina fulani. Huwa si watu wenye uwezo wa kusema hapana.
Kwa kawaida unaposhindwa kusema hapana kwa yale
mambo ambayo hayaendani na malengo yako, unakuwa ni mtu kama ambaye unapoteza muda
sana.
Sasa basi, kama usipoweza kusema hapana, ujue kabisa
utapotezewa sana muda wako na watu wengi ambao watakuwa wanataka ufanye mambo
yao. Hivyo, utake usitake hapa ndipo unalazimika kujifunza kusema HAPANA.
Jifunze kusema hapana ujenge mafanikio yako. |
Kila wakati linda muda na mafanikio yako kwa kusema
HAPANA. Kama usipoweza kusema utapoteza muda wako na hata mafanikio yako kwa
ujumla na hilo litakuwa halina ubishi.
Ili uweze kufanikiwa katika hili, zipo HAPANA kubwa
za aina tatu ambazo unatakiwa uzijue na kuzizingatia ili uweze kupata mafanikio.
Sema hapana
kwako wewe mwenyewe.
Watu wasio na mafanikio ni wazito sana kusema
hapana kwa mambo ambayo hayawasaidii. Angalia mambo unayoyafanya yanakusaidia
kufanikiwa au la. Kama mambo hayo hayakusaidii kufanikiwa, sema hapana tena ya
herefi kubwa.
Kwa mfano kama kuna jambo unataka kulifanya leo,
halafu unajisikia uvivu uvivu unataka kulifanya kwa wakati mwingine, sema
hapana nitafanya leo leo. Usikubali kitu chochote kikukwamishe katika hili,
sema hapana.
Sema hapana
kwa watu wengine.
Acha kuona aibu kama kuna jambo ambalo unaambiwa na
huliwezi, sema hapana kwa jambo hilo. Jiulize ukimkubalia kila mtu kitu
anachotaka kwako itakuwaje? Nafikiri utakuwa kama mtumwa wao.
Angalia hata matajiri wakubwa hawakubali kila kitu.
Sema hapana kwa wengine pia. Mwanzo linaweza likawa zoezi gumu kidogo kwako
lakini siku zinavyozidi kwenda utazoea na utamudu.
Sema hapana
kwa dunia.
Ili uweze kufanikiwa unatakiwa uyajue makusudi yako
vizuri yaliyokuleta duniani. Ukishajua hivyo, kataa kitu chochote ambacho
unaona hakiendani na malengo yako hata kiwe kizuri sana.
Hapa inabidi ujue kusema hapana hata kwa fursa zote
ambazo zipo nje ya makusudi yako. Ng’ang’ania kitu kile ambacho umekusudia
kukifanya, acha kuyumbishwa na mtu au kitu.
Hivyo ndivyo unavyoweza kujifunza kusema hapana na
kujenga misingi imara ya maisha unayotaka.
Badili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi,
endelea kujifunza kupitia mtandao wako bora wa dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku.
Chukua hatua na kila la kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.