Feb 22, 2017
Maeneo Unayotakiwa Kuwajibika Sana Ili Kujenga Mafanikio Makubwa.
Kati
ya kitu ambacho unatakiwa uelewe katika safari yako ya mafanikio ni kwamba,
mafanikio yoyote unayoyatafuta yanaanza na wewe. Hiyo ikiwa na maana, hakuna
mtu mwenye hamasa kubwa ya kufikia mafanikio yako zaidi ya wewe.
Kwa
hivyo, hiyo inatuonyesha kwamba ili ufanikiwe, unatakiwa kuwajibika katika
maisha yako kwa nguvu zote na kwa asilimia zote. Ikiwa hutafanya hivyo
utajiangusha mwenyewe, maana hutaweza kufanikiwa.
Kupitia
makala haya nataka nikupe dondoo za kukusaidia kujua maeneo ambayo unatakiwa
uwajibike kwa uhakika ili upate mafanikio unayoyahitaji. Bila kupoteza muda tufuatane
pamoja katika makala haya kujifunza;-
1.
Wajibika kufanya maamuzi sahihi.
Kabla
hujafanya kitu chochote ni lazima ufanye maamuzi. Na kufanya maamuzi ya kuweza
kubadili maisha yako kuna wakati huonekana ni kitu kigumu sana.
Lakini
hakuna namna nyingine zaidi ya kujua unatakiwa ufanye maamuzi yatakayobadilisha
maisha yako. Pia inatakiwa ujue bila
kufanya maamuzi bora ya kukufanikisha itafika mahali utakwama.
Wajibika katika kila eneo la maisha yako kwa ukamilifu. |
2.
Wajibika kuweka mipaka ya maisha yako.
Ikiwa
unataka kufika kule unakotaka kufika kimafanikio lazima ujue jinsi ya kuweka
mipaka kwenye maisha yako. usiruhusu maisha ako yaingiliwe na kila mtu
anavyotaka. Weka mipaka maeneo muhimu.
Jifunze
kuweka mipaka kwenye matumizi ya pesa zako, nguvu na hata muda wako pia. Usiogope
kuweka mipaka yoyote ile, ni muhimu kufanya hivyo ili kupata mafanikio. Kama hutajiwekea
mipaka itakusumbua sana kufanikiwa.
3.
Wajibika kukabiliana na mabadiliko.
Tunaishi
katika dunia inayobadiilika sana. Ili kuweza kwenda sawa na dunia hii inatakiwa
ifike mahali ukakubali kuwajibika ili ikusaidie kwenda sambamba na mwendo kasi
wa dunia.
Kama
hutaweza kukabiliana na ushindani, elewa kabisa utashindwa. Njia bora ya kuweza kukabiliana
na ushindani ni kujifunza kila siku na kujua maisha yanataka nini kwa sasa.
4.
Wajibika kuwa mkarimu.
Ni
rahisi kufika ngazi ya juu kimafanikio ikiwa wewe mwenyewe utakuwa mkarimu. Unapokuwa
mkarimu unajenga uaminifu mkubwa kwa watu na hiyo inakusaidia kushirikiana
katika mambo mengi ikiwa pamoja na biashara.
Kiuhalisia
hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata kiurahisi kama ikiwa hutaweza kuwajibika
katika hayo maeneo. Kila wakati hakikisha unawajibika vizuri katika maeneo hayo
ili ujenge mafanikio makubwa na ya uhakika.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.