Feb 1, 2017
Amua Kuwa Hivi Katika Kuyasaka Mafanikio.
Mwandishi fulani wa masuala ya
mafanikio jina tunalihifadhi kwa sababu za kiufundi aliwahi kuandika ya kwamba "awezavyo mtu akilini mwake ndivyo
alivyo". Ukifikiria kwa umakini bila kuiruhusu akili mgando katika
kuwaza utajua ya kwamba usemi huo ni ukweli kabisa.
Unajua ni kwanini ukweli huo ni
ukweli? ipo hivi miongoni mwa na sababu ya sisi kuendelea kuwa katika hali ya
umaskini kila wakati, inatokana na vile ambavyo tunaweza na kuamini katika
akili zetu. Wengi wetu tumekuwa na mawazo mgando ambayo yamekuwa hayana
msaada wowote katika kupiga hatua za kimaendeleo na kimafanikio.
Mawazo hayo mgando yamekuwa
yakitendeka na mwisho wa siku tumejikuta tukiwalamu watu wengi ambao
wanatuzunguka ikiwemo serikali, ndugu jamaa na marafiki. Licha ya kuendelea kulaumu
mawazo hayo mgando yamekuwa ni kizuizi katika safari ya mafanikio.
Hivi hajawahi kukutana na mtu anasema
ya kwamba hawezi kufanikiwa milele? Hii
ni kutokana na mtu huyo amekwishakata tamaa? Bila shaka umewahi kukutana
na aina hii ya watu, kama hajawahi kukutana na watu wa aina hii huenda
ukawa ni wewe.
Amua kuwa wa tofauti katika kuyasaka mafanikio yako. |
Lakini ukweli ni kwamba hatma ya
maisha yako inatokana na wewe mwenyewe vile ambavyo ameamua kuwaza na kuchukua
hatua ya kile ambacho unawaza. Vilevile maisha ya kimafanikio yatakuwa na
nafasi kwa upande wako endapo "utaaamua kuwa wewe"
Kuwa wewe ni ndo siri kubwa ya
mafanikio yako, hata siku moja usiruhusu mtu awaze juu yako, au
uamue kuwaza vitu vingine ambavyo watu wengine wanawaza. Tunashindwa kufanikiwa
kwa sababu vitu ambavyo tunavifanya kuna mtu alisema tufanye kwa sababu
vinalipa.
Wafanyabiashara wengi wamekuwa
wanalalamika ya kwamba biashara ngumu kwa sababu waliona mtu fulani amefanya na
wao wakaamua kufanya, lakini leo hii wanalalamika ya kwamba biashara ni
ngumu. Sababu ya kutokea kwa hali hiyo ni kwamba hawajafanya kuwa wao ila
wameamua kufanya mawazo ya watu wengine.
Lakini ikumbukwe ya kwamba masuala ya
kimafanikio kwa upande wako yatakuja kama utaamua kuwa wewe kwa kufanya kitu
ambacho kitatoka nafsi mwako. Kwani kufanya hivi utakifanya kwa moyo wako
wote na si vinginevyo.
Nimalize kwa kusema acha mawazo
mgando amua kuwa wewe ama hakika utafanikiwa. Mwisho nikutakie maisha mema
yenye mafanikio tele.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.