Feb 20, 2017
Chanzo Cha Hofu Nyingi Ulizonazo Na Zinazokuzuia Ushindwe Kufanikiwa.
Wapo watu ambao ni waoga sana kuwajibika hasa
linapokuja suala la kufanya kile kitu wanachotakiwa kufanya. Utakuta ni watu wa
kusingizia sana hiki au kile, kwamba siwezi kufanya kwa sasa, kwa sababu hii au
ile.
Kwa mfano, utakuta mtu anataka kuanzisha biashara ya
aina fulani, ambapo ukiangalia kama ataanzisha biashara hiyo, itamsaidia sana
mtu huyo kuweza kuingiza kipato kikubwa na cha ziada.
Hata hivyo, kitu cha kushangaza au cha ajabu kwa
sababu ya hofu ama wasiwasi tu, mtu huyo atajikuta anatoa visingizio vingi sana
mpaka kushindwa kuanza biashara hiyo, ambayo ilitakiwa ainze mara moja.
Kitu usichokijua, kisaikolojia unaposhindwa kufanya
jambo fulani kwa sababu ya hofu za mara kwa mara, mawazo yako ya ndani, mawazo yanayoumba
au kupelekea mambo hutokea, huchukua hofu hiyo na kuihifadhi na kuifanya kama ‘ulemavu’ wako.
Kwa hiyo kila unapojaribu kufanya jambo jipya utakuta
wazo linashuka haraka sana ndani yako, ‘Je
ukishindwa itakuwaje? Si unaona wengi sana huwa wanashindwa hapo,’? Utashangaa
ubongo wako una hofu sana, hata pengine bila kujua kwa nini?.
Lakini ukiangalia,
hiyo yote inatokana na hofu ndogo ndogo ambazo ulizibeba sasa zimekaa kwenye
mawazo yako ya kina na imekuwa kama ndio ‘ulemavu’ wako wa kiakili yaani 'psychological disorders', sasa kila kitu ukitaka kukifanya
unakuwa una hofu.
Kitu cha kujiuliza kwa nini watu wanakuwa na hofu
sana hasa pale wanapotaka kuanza jambo fulani? Chanzo hasa huwa nini?
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea hofu moja
kwa moja kwenye maisha yako na kushindwa kuchukua hatua sahihi za majukumu
yako.
1. Kuogopa
kukosea.
Utakuta hapa hofu inazalishwa sana kwa sababu ya
kuogopa kukosea. Utakuta mtu anakuwa ana wasi wasi mwingi hivi jambo hili
lisipokwenda sawa itakuwaje? Mwisho wa siku kila kitu hufika mahali kimekwama.
Soma; Aina Nne Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako.
2. Kuogopa
kushindwa.
Zishinde hofu zako, ili ujenge mafanikio makubwa. |
Pia kuna watu ambao wanajawa na hofu kwa sababu ya
kuogopa kushindwa. Kwa watu kama hawa kwao wanaona inakuwa ni bora wasifanye kabisa kuliko
wakafanya halafu wakashindwa. Kwa lugha rahisi watu wenye hofu hii huwa hawafanikiwi.
.3. Kutokujiamini.
Unaposhindwa kujiamini, elewa kabisa huwezi kufanikiwa
katika kitu chochote. Kujiamani mara nyingi ndio msingi wa mafanikio. Waangalie
watu ambao wanajiamini utakuta ni watu
ambao wanamafanikio wakati wasiojiamini hawana kitu maishani mwao.
4. Kuogopa
ushindani.
Mwingine utakuta anashindwa kuanza jambo analotakiwa
afanye, inaweza kuwa biashara au kitu chochote eti kisa kwa sababu ya kuogopa
ushindani. Kwa jinsi anavyoogopa ushindani anajikuta hawezi tena kufanya kitu.
5. Kukosa
hamasa.
Pia ni rahisi sana kuanza kuingiwa na hofu kama umekosa
hamasa ya kile unachokifanya. Ni muhimu sana kuwa na hamasa ili ikusaidie
kukujaza ujasiri wa kufanya hicho unachokifaya kwenye maisha yako.
6. Mawazo
hasi.
Kama una mawazo sana kama vile ‘aah mimi sina uwezo wa kufanikisha hili, huu mradi sio saizi yangu,’
uwe na uhakika hutaweza kufanya kwa ujasiri, hapo utakuwa unajijaza hofu
mwenyewe zitakazo kufanya ushindwe tu.
Kimsingi, kuogopa kushindwa, kuogopa ushindani, kugopa
kukosea, kukosa hamasa, mawazo hasi na kutokujiamini ni moja ya sababu
zinazokufanya wewe uwe na hofu kubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua na kila la kheri katika kufikia
mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi,
karibu kwenye kundi la Whats App ili
tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha
ikifuatia na jina lako kwenda 0713
048035 ili uanganishwe.
Ni wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.