Feb 13, 2017
Jinsi Ya Kufanya Mambo Magumu Kuwa Rahisi.
Ni
rahisi kufanikisha jambo lolote, ikiwa jambo hilo utataanza kulifanya mara moja
na kuacha kusubiri.
Ni
rahisi kujifunza kitu kipya kwenye maisha yako, ikiwa utaamua kweli kujifunza
kila siku.
Ni
rahisi kutoka kwenye kushindwa, ikiwa kama utachukua jukumu la kujaribu tena na
tena.
Ni
rahisi kusogea hapo ulipo kimaisha, ikiwa utaweka nia na juhudi kubwa ya kutaka
kutoka hapo ulipo na kwenda ngazi nyingine kimafanikio.
Ni
rahisi kuwa na watu wanaokutia moyo, ikiwa wewe utaamua kuwa wa kwanza kuwatia
moyo wengine kufanikiwa.
Ni
rahisi kuweka akiba na kuanza kukuza utajiri, ikiwa kuanzia leo utaamua kuanza
utekelezaji.
Ni
rahisi kukamilisha lile jukumu ambalo linasemwa sana kwamba, haliwezekani,
ikiwa wewe utaligawa jukumu hilo na kuanza kulifanyia kazi.
Ni
rahisi kuongeza kipato chako, ikiwa utajifunza kuwekeza hata kama ni kidogo
katika maisha yako.
Ni
rahisi kuyafanya maisha yako yakawa na maana, ikiwa kila siku utachukua jukumu
la kufanya mabadiliko kidogo kidogo.
Maisha
yako yanaweza kuwa kama unavyotaka yawe wewe, ikiwa wewe kwanza utachukua
jukumu la kuyafanya maisha yako yakawa rahisi.
Acha
kufanya mambo au maisha yako yakaonekana magumu sana hasa kwa zile hali ambazo
ulikuwa unaweza kuzibadili kabisa.
Kumbuka,
Ni rahisi kuanza jambo jipya, ni rahisi kujaribu tena pale uliposhindwa, ni
rahisi kufikiri jinsi utakavyofanya maisha yako yakawa bora zaidi, sasa jiulize
ni wapi unaposhindwa?
Kwa
jinsi unavyofanya kidogo kidogo kwa yale mambo yanayoonekana magumu, siku hadi
siku, kuna wakati utakamilisha mambo hayo magumu na hutaweza kuamini.
Kila
wakati Jifunze kufanya mambo magumu kuwa rahisi.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.