Feb 7, 2017
Sababu Ya Bidhaa/ Huduma Kushindwa Kufanya Vizuri Katika Mzunguko Wa Kibiashara.
Bidhaa ndiyo alama ambayo inayomtambulisha mfanyabiashara fulani
katika biashara. Kwa mfano leo ukiona bidhaa fulani unajua kabisa ni nani
ambaye ametengeneza bidhaa hiyo. Lakini siku zote ni kwamba ili tuweze kukua
kibiashara ni lazima tutafute upekee wetu katika biashara husika.
Watu wengi tunafanya biashara lakini hatutafuti utofauti
wetu na wafanyabiashara wengine, na kufanya hivyo kumesababisha biashara nyingi kufa
kabla ya wakati.
Na hizi baadhi ya sababu ya kufa kwa bidhaa au huduma katika
mzunguko wake;-.
Ubora hafifu wa bidhaa.
Kuwepo kwa ubora hafifu katika bidhaa au huduma yeyote ambayo
unaitoa hiyo ndo chanzo cha kufa kwa biashara nyingi. Hivyo kwa kuwa
unasoma hapa kwa lengo la kupata mawazo chanya ya kukuza biashara
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora kila
wakati.
Kuzalisha bidhaa bora kila wakati ndo chanzo cha kukuza biashara
yako na hatimaye kupata faida kubwa. Hivyo ikumbukwe ya kwamba ukitaka
kujitofautisha na wafanyabiashara wengine hakikisha ya kwamba unazalisha
bidhaa bora.
Uhaba wa njia mathubuti za usambazaji.
Hii ni sababu nyingine
ambayo inachangia bidhaa nyingi kushindwa kukua katika soko ni kuwepo kwa uhaba
wa njia mathubuti za usambazaji wa njia za kutosha wa bidhaa kutoka kwa
mfanyabiashara kwenda kwa mteja.
Hivyo kama kweli unataka mafanikio ya kibiashara Unachotakiwa
kufanya ni hakakikisha unafanya vizuri katika suala zima la usambazaji wa
bidhaa yako kutoka kwako kwenda kwa mteja. Kama una uwezo pia wa
kusambaza bidhaa kwa kumpelekea mteja wako huduma mahali ulipo.
Kupanda kwa bei kiholela .
Sababu nyingine ambayo husababisha bidhaa kufa kabla ya
wakati ikiwa sokoni ni pamoja na kupanda na kushuka kwa bei ya huduma au
bidhaa. Kufanya hivyo ni dalili tosha ya kuwayumbisha wateja wako.
Hivyo ili kuweza kushinda vikwazo ambavyo vitasabaibisha kufa
kwa biashara yako hakikisha unakuwa na utaratibu maalumu. Ikiwezekana wajuze
wateja wako juu ya upandaji wa bei mwezi mmoja kabla ya bei ya bidhaa yako
kupanda.
Na kufanya hivyo kuyafanya mteja wako ajisikie huru kama ni sehemu ya ufalme, maana kuna usemi husema mteja ni mfalme.
Na kufanya hivyo kuyafanya mteja wako ajisikie huru kama ni sehemu ya ufalme, maana kuna usemi husema mteja ni mfalme.
Kutoa huduma au bidhaa isiyohitajika kwa watu.
Mara nyingine umekuwa ukilalamika ya kwamba inawezekana ukawa
umelogwa katika biashara yako, hii ni kutokana umekuwa huoni faida.
Lakini ukweli ni kwamba hakuna ambaye amekuloga zaidi ya kujiloga mwenyewe.
Hivyo ili uweze kukua katika biashara yako kama nilivyoeleza katika makala haya unatakiwa kufanya uchunguzi wa kile ambacho wateja wako wanaohitaji kwa wakati sahihi.
Hivyo ili uweze kukua katika biashara yako kama nilivyoeleza katika makala haya unatakiwa kufanya uchunguzi wa kile ambacho wateja wako wanaohitaji kwa wakati sahihi.
Ukifanya uchunguzi wa kile ambacho wateja wako ambacho
wanaohitaji utasababisha kufanya ongezeko la mauzo na wateja kwa ujumla. Hivyo
hakikisha unatoa huduma sahihi kwa wakati sahihi ama hakika biashara yako
itafanikiwa.
Ndimi afisa Mipango :
Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.